Buriani Abuu Semhando a.k.a Baba Diana

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
34245_1543415664235_1200297381_31541798_6218600_n.jpg

Marehemu Abou Semhando 'Baba Diana' enzi za uhai wake. Hapo ilikuwa katika show ya Old Skul viwanja vya Karimjee ambapo wakongwe wa muziki walikusanyika kutumbuiza

http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/msiba-mzito-twanga-pepeta

 
Abuu semhando-kagongwa na gari(benzi) akitokea kazini saa 9 usiku.yeye alikuwa kwenye pikipiki.mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.
Source:Asha Baraka/TBC-1
 
Wana jf,

Kuna taarifa kwamba yule mwanamuzioki wa siku nyingi wa bendi ya Twanga Pepete
ABUU SEMHANDO amefariki usiku wa kuamkia leo kwa kugongwa na gari lisilo fahamika.

mwenye taarifa zaidi atujuze.
 
Heee! ALITOKA WAPI? ALIKUWA NA GARI LKE? ALIKUWANA KINA NANI? POLE TANZANIA, POLE INDUSTRY YA MUZIKI MAANA WANAFUNGA MWAKA MFULULIZO, JANA TULIKUWA REMMY LEO BABA DIAN MHHHH!
 
Abuu Semhando mwanamuziki nyota wa bendi ya African Stars Twanga Pepeta hatunaye tena baada ya kugongwa na gari wakati akiendesha pikipiki kwenye majira ya saa kumi usiku.

Umauti ulimkuta Semhando wakati akijerea nyumbani kwake akitokea kazini ambapo bendi ya Twanga Pepeta ilikuwa ikifanya shoo eneo la Africana Mbezi Beach.

Mmoja wa wanenguaji wa Twanga Pepeta, Queen Suzi akiongea na Nifahamishe.Com alisema kuwa alikuwa akitaniana na Semhando wakati akipiga tumba lakini hakuwa mchangamfu muda wote.

Msiba upo Mwananyamala nyumbani kwake.

Source: http://www.Nifahamishe.com
 
Habari nilizipata asubuhi hii ni kwamba Abuu Semhando wa Twanga pepeta hatunaye baada ya kupata ajali ya pikipiki alfajiri hii akitoka kwenye maonyesho ya bendi yake ya Twanga pepeta.
Mungu aiweke mahali pema roho yake..ni pigo kubwa kwa muziki wa Tanzania!!!!!!!
 
Ooohhh God!!!!!!!!

Nikweli kabisa na amegongwa na gari ya kwanza iliyomtupa barabarani na bahati mbaya gari nyingine mbili zeikampitia na kummaliza.. akumbuka kumuona kwenye picha za msiba wa Dr. Remmy.... OMG

Kweli dunia mapito kama alivyosema Matonya

Dunia Mapito
Ahh dunia a
Bado nikiza, bado nikiza
Na marashi ya dunia siyasikii
Najihisi nipo kuzimu naishangaa

sayari hii Iliyojawa wanasiasa,

michezo na wasanii
Najiuliza wamekuja huku kutalii
Au wamesha hamia 'Dunia Haijirudii'
Mara nasikia swali kama la nguvu za hoja
Dandu ananiuliza, albamu zinajikongoja?
Vipi mmegonga kopi chini ya milioni moja?
Jibu zinalipa sio moja kwa moja
Steve 2K anauliza bifu zinaendeleaje?
Nimesha msamehe Castro ameshatoka Segerea?
Namjibu bifu lipo na vita vinanyongea
Castro bado anaoza, tuanzeni kumuombea
Complex naye anauliza 'albamu ile ya Wagosi
Walishagonga kopi ngapi hadi sasa kwa wadosi?
Namjibu tangu ufe mambo yote ni mikosi
Makundi yanavunjika duniani tunakumiss

Chorus 2x

Yea yie yie
Dunia Mapito jamaa
Tuwaombeeni waliokufa wende salama
Mi nawe tupo, hatujui siku yetu lini
Kinachotakiwa tuishi kwa amani duniani

Verse 2
Kulia nafuta chozi, kushoto lanidondoka
Nakosa raha TX Moshi nikimkumbuka
Muone ananiuliza muziki wa dansi ndio ushashuka?
Jibu bado upo Ila naamini pengo lako halitozibika
Mara kwambali nasikia sauti ya gitaa

Sauti ya gitaa inapigwa huku inaniita
Kumbe mzee wakale, hayati Bob Marley
Ananiuliza mziki wa reggae unaenda vipi?
Reggae bado ipo

Ziggy na Damian nahisi wanagonga copy
Marijaniiii Ananiuliza muziki wangu Unaimbwa sana duniani
Vipi familia yangu Inafaidika kitu gani?
Jibu mimi sina labda mwanao Marijani
Kiza ni kinene sioni pa kupapasa
Mara kwa mbali nawaona wanasiasa
Machozi yananitoka, chini nadondoka
Namuona Karume na Nyerere
Julius wananiuliza 'Muungano je unanafasi'
Nawajibu msiwe na wasi


Sasa Ari mpya, Nguvu mpya pia na Kasi
Ulimwengu mmeuacha dunia ndio inawamissi
Repeat Chorus 2x


RIP Babu
 
Back
Top Bottom