Bungeni zijadiliwe hoja, kanuni, pongezi, miongozo, mipasho, utani, vijembe iwe home work | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bungeni zijadiliwe hoja, kanuni, pongezi, miongozo, mipasho, utani, vijembe iwe home work

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Analyst, Jul 22, 2011.

 1. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Habari zenu wakuu. Najaribu kutafakari Bunge letu na kukiri kwamba limechangamka sana lakini linaanza kukera kwa kelele ambazo mimi naona hazina maana sana. Angalieni usomaji wa kanuni kila dakika mbunge anapotaka kusema jambo na kanuni hiyohiyo kusomwa mara kadhaa kwa kitendo kilekile ndani ya kikao kimoja. Angalieni muda unaotumika kupongeza unaotumiwa na mawaziri na wabunge...baadhi wanawapongeza na kuwashukuru hadi familia zao, wapigakura wao na mbunge au waziri mwenza. Jamani...jamani ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia ya mawasiliano waheshimiwa hawa hawawezi kutumia simu, mtandao kumshukuru wake au waume zao hadi wapewe nafasi ya kuzungumza Bungeni? Haya ni matumizi mabaya ya muda wa kujadili mambo ya msingi. Eti waziri anamshukuru rais kwa kumteua wakati wa kikao cha bunge wakati wanakutana hata kabla ya kuapa kutumikia nafasi hiyo, kwa nini asimshukuru na kutoa ahadi zake huko? ....This is crazy!

  Angalieni mipasho, utani, kejeli, vijembe na jinsi mambo hayo yanavyopoteza muda wa Bunge na mwishoni wanaishia kupitisha bajeti haraka haraka pasipo kupitia baadhi ya vifungu kwa kisingizio cha muda kumalizika. Hauhitaji calculator kujua kwamba muda wanaotumia kina Lema, Chatanda, na wapenda vijembe wengine, unatosha kabisa kumalizia zile dakika zinazopungua kila bajeti zinapokuwa zinapitiwa kifungu nadi kifungu especially around saa mbili usiku.
  Napendekeza wabunge/mawaziri/spika/wenyeviti wasome kanuni wanapokuwa nje ya ukumbi na kuwa huru kuzitumia pasipo kupoteza muda mwingi kuzisoma wakati wa mjadala. Waheshimiwa hawa pia wakawashukuru wapiga kura wao wanapowatembelea majimboni kwao na si wakati wa kujadili mambo ya maana. Baadhi ya viti maalum wakianza kuzungumza utatamani uzime TV. Baadhi yao wanachojua ni mipasho, masimango, maudhi utadhani........... Jamani mambo mengine yafanyeni wakati wa mapumziko na si wakati wa vikao!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wewe sio analyst as far as the literal meaning of the subject concerns!
  Ni vema ukawa fair kwa kutaja source ya ulichopaste hapo juu!
  Hayo ni maongezi Live ya kipndi cha HOJA YANGU kilichorushwa Live na ITV usiku huu!
  Umemnukuu Mama Ananilea Nkya neno kwa neno na ku,paste hapa, halafu huweki source!
  Tujifunze kuthamini mawazo ya wenye Hekima kwa kunukuu maneno yao na si kufanya PIRACY!
   
 3. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Nashukuru kwa mawazo yako! Bahati mbaya hapa ninapoishi sipati ITV. Ni kweli, mimi siyo Analyst kwa maana unayoitaka wewe. I'm just a simple guy. Hata wewe naamini si Paka. Are you? God! ....These are just ID's! Didn't you learn about that when you joined the forum? Next time ukihisi mawazo ya mwanaJF mwenzako yanafanana kwa aina yeyote na source unayoijua wewe ukadhani amekopi bila admission ni vizuri ukasoma kazi/post zake nyingine kwa sababu napata hisia kwamba unajaribu kunihukumu kama nisiye na uwezo wa kupresent ninachokiwaza isipokuwa hadi nikopi ITV.
  Nasikitika kukujulisha kwamba sijatazama ITV na wala siyo mbovu kiakili kama wewe unavyodhani. I might not be the best but I believe and know that I'm good enough. Thanx anyway!....Paka!
   
 4. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Wabunge viti maalum kuwa mabingwa wa mipasho, utani, kejeli na vijembe ni kwa sababu wako humo mjengoni kwa kazi hiyo. Ni cheerleaders. Wengi, hasa wa CCM, hawana uwezo hata wa kuwa wajumbe wa nyumba kumi.
   
 5. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe kwa baadhi ya mambo uliyoyawakilisha hapa jamvin kuhusu hayo madudu wanayofanya badhi ya wawakilishi wetu.Kunajambo moja ambalo nimeligundua kutokana na kufuatilia hiyo mikutano ya bunge inayoendelea,inapotokea wabunge wa upinzani wanapokuwa wanatoa hoja nzito zinazoikaba koo serikali hapo ndio utaona wabunge wengi wa ccm wanapoomba mwongozo ili kujaribu kuinasua serekali,na sidhani kama ninahitaji kuwa na elimu kama ya malehem shekhe Yahaya kutabiri ya-kwamba bunge hili litavunja rekodi kwa wabunge kuomba mwongozo.Mwisho sidhani kama kuomba mwooga ni kitu kibaya ila wajaribu kuomba mwoongozo ulio na tija kwa wanao waongoza isiwe kwaajili ya maslai ya vyama vyao.
   
 6. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Halafu wajanja kweli, pindi Mbunge wa upinzani anaposimama na kuanza kuchangia utasikia spika anaanza kulalamika kuhusu muda. baadaye ndio utagundua kwamba muda mwingi umetumika kutuma salamu na kutaja majina ya wachangiaji, halafu imeshakuwa kama mchezo kila mtu siku hizi anaalika familia yake kutembelea bungeni ama kuwatumia hizo salamu na wakati utakuta walikuwa pamoja masaa machache yaliyopita, ni kama wapo kwenye mashindano vile.
   
Loading...