Bungeni wiki hii

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
Bunge la wakati huu limekuja kwa staili mpya. Ni jambo adimu sana kwa mtu mkubwa kama Waziri Mkuu kumwaga machozi ndani ya Bunge. Hii inaonyesha Waziri Mkuu hakukubaliana na kitendo cha vyombo vya habari kwamba yeye alikiri kwamba anayemuua albino nae auawe. Nina imani alikiri kwamba sheria kali zichukuliwe dhidi ya wanaowaua albino. Kwa mawazo yangu ni kwa nini anaemuua albino nae asiuawe?

Naombeni mchango wenu.
 
Bunge la wakati huu limekuja kwa staili mpya. Ni jambo adimu sana kwa mtu mkubwa kama Waziri Mkuu kumwaga machozi ndani ya Bunge. Hii inaonyesha Waziri Mkuu hakukubaliana na kitendo cha vyombo vya habari kwamba yeye alikiri kwamba anayemuua albino nae auawe. Nina imani alikiri kwamba sheria kali zichukuliwe dhidi ya wanaowaua albino. Kwa mawazo yangu ni kwa nini anaemuua albino nae asiuawe?

Naombeni mchango wenu.

Machozi ya Pinda yanazua maswali mengi kuliko majibu. Je anataka tuamini ndiyo ilikuwa mara yake ya kwanza kusikia habari hizo za mauaji? Je, wakati akiongea alijua mamlaka na madaraka aliyonayo katika kutatua matatizo ya wananchi kama msimamizi wa kila siku wa kazi za serikali? Je, machozi yanafuta kosa kama kweli alivunja katiba? Je, tunahitaji PM anayelia lia badala ya kutatua matatizo yetu? Maswali yanweza kuendelea... ila mimi binafsi sijamuelewa kwa sababu sijaona kama katoa ufafanuzi wa kauli yake. Au do tuamini kuwa kakiri na kuomba tumsamehe?
 
Last edited:
Kwa kweli ni jambo linaumiza sana kuona mtoto mdogo mwenye ulemavu wa ngozi anakatwa kiungo chake na kuvuja damu hadi mauti yanamfika.kwa binadamu yeyoye ukishuhudia vitendo hivi laziam utalia au machozi yatalengalenga kwenye macho yako.

Mh. PM Ameonyesha ni jinsi gani yeye kama binadamu suala hili la mauaji ya albino linavyomuumiza na jinsi serikali inavyoumia kuhusu hilo.

Hoja ya PM kule Kagera ilikuwa inamaanisha jinsi gani serikali inavyochukizwa na suala ili ya mauaji ya vikongwe na albino kwa imani za kishirikina.

ndiyo maana serikali imetamka hatakuwa tayari kumvumilia mtu yeyote yule atakayehusika katika suala hili kwa njia moja ama nyingine, kikundi kazi(task forces) zimeshaundwa kwa kufanya ushiriki shirikishi wa jamii kwa hili kama kuunganisha jeshi la polisi,usalama wa taifa,sugusugu n.k hizi zote ni jitihada za serikali kukomesha mauaji haya ya vikongwe na albino ambayo yanalitia doa kubwa sana Taifa letu ndani na nje ya nchi.

Hoja yangu kwa vyombo vya habari vitumie taalumu vyema kama maadili ya kazi yao inavyovitaka kwa kuchambua hoja na habari mbalimbali ili lengo kuu linalotakiwa kuwafikia wananchi liwafikia na si kuipotosha jamii.

Naomba waweke mbele maslahi ya taifa na watambue kuwa hoja zao zinawafikia wananchi walio wengi hivyo ni lazima ziwe za hekima na busara baadala ya ushabiki either wa kisiasa au interest zingine za kibiashara.

Nashukuru sana kwa ukomavu wa bunge letu hivi sasa kidemokrasia na hata kwa hekima na busara hususani za mh.spika na waziri mkuu,mambo yanakwenda swali.

Hata leo asubuhi mh.PM na spika wametumia busara na hekima kubwa kuiweka wazi hoja ya mh.Mzindikaya kwa wizara ya Utalii na maliasili, na hatima bunge kulidhia maazimio hayo binafsi na ya wizara husika kwa maslahi ya taifa letu.

Tuwe wazalendo na wenye kuweka mbele maslahi ya taifa letu kwanza then ndio tuweke ushabiki na inerest zetu binafsi.

nasisitiza wahabahari wawe wa kufuata maadili na taratibu za taaluma yao kama inavyoelekeza kwa maslahi ya taifa letu na wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

thx.
AM
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom