Bungeni: Waziri Membe aiponda taarifa ya Wenje aihusisha na JamiiForums

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071
Kasema ni wahuni wachache walioitengeneza!

Taarifa yenyewe katika JF ni hii hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/216505-waingereza-wamnanga-rais-kikwete.html

Sehemu ya hotuba ya Wenje, ambayo Membe anadai imetolewa JF. Asijochua Membe ni kwamba hawezi kupata details hizo kwenye mtandao wa Gazeti la The Guardian la Uingereza, kwa sababu mjadala huo ulifungwa. Ofcourse ukitembelea mtanda wao wana tabia ya kufunga comments za mjadala fulani.

Lakini kinachodhihirika hapa ni kwamba kabla ya Kambi ya Upinzani Bungeni kutoa hotuba yake leo bungeni, Membe hakuwa informed kabisa na jinsi wazungu wale (si wawili tu kama alivyosema Membe) walivyomnanga Rais wa Jakaya Kikwete.

Yaani katika discussions zote zilizoibuka wakati ule wazungu wakitoa maneno makali juu ya rais wetu, serikali hii haikuwa na habari, Membe hakuwa na habari, mpaka leo iliposomwa bungeni! Mbona ilijadiliwa kuanzia katika mtandao huo, kisha ikaja hapa JF, kisha kwenye forums zingine nyingi.

Lakini pia Membe kaonesha mapungufu na uwezo mdogo katika kujibu hoja za wapinzani kulinda hadhi ya Rais Kikwete na Tanzania kwa ujumla nje ya nchi. Badala ya kujibu hoja, akakimbilia kutumia fallacies kibao...eti source ya Wenje ni JF, so what is wrong with the source katika hili kwa mfano?
Mheshimiwa Spika, wakati wa Mkutano wa Davos, hasa wakati ambapo aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown alipokuwa akiongoza mdahalo juu ya Afrika, kuliibuka mjadala katika Mtandao wa Gazeti la The Guardian (itakumbukwa kuwa hili ndilo gazeti ambalo liliandika sana juu ya ufisadi wa rada uliofanywa na BAE Systems na baadhi ya viongozi wa serikali hii), Mheshimiwa Spika kwa faida ya bunge lako na Watanzania, tutanukuu baadhi ya maoni ya gazeti hilo; Baadhi ya maoni hayo ni kama ifuatavyo;

“Rais Kikwete wa Tanzania ni mmoja wa viongozi wa Afrika ambao dhaifu/pathetic katika nyakati hizi, ni kiongozi wa nchi ambayo ni moja ya nchi zenye utajiri wa mkubwa wa rasilimali duniani, lakini bado anaongoza duniani kwa kuomba. Kampuni nyingi za kigeni zinaijua Tanzania kama moja ya nchi yenye mianya myepesi ambayo unaweza ukaingia na ukachukua unachotaka bila kuulizwa chochote.


Nashindwa kabisa kuelewa juu ya akili za viongozi wa nchi hiyo ambao wanaabudu wazungu…nimefanya kazi katika nchi hiyo kwa miaka 8, nikiwa mtumishi wa UNDP. Niligundua jinsi uongozi wa nchi hiyo usivyokuwa na ufanisi na ulivyoathiriwa na rushwa. Mawaziri wake waliokula rushwa katika kashfa ya rada kutoka Kampuni ya BAE hawajawahi kushtakiwa mahali popote pale, pamoja na kuwepo kwa ushahidi ulio wazi dhidi yao.


Walipa kodi wa Uingereza lazima waache kuendelea kusapoti ziara za nje za viongozi hawa wala rushwa. Rais Kikwete hana sababu yoyote ya kwenda Davos kuomba misaada kwa mataifa ya nje. Nchi yake tayari ni ya tatu kwa kuongoza kupokea misaada. Anapaswa kuona aibu kusema mbele ya dunia nzima kuwa watu wake ni maskini. Watu wake kuendelea kuishi maisha ya umaskini…ni uzembe wa viongozi. Huo ni mzigo wake mwenyewe.



Watanzania wana matatizo yao, Waingereza nao wanayo ya kwao, lazima tutambue hilo. Hatuwezi kugharamia ziara zake za nje ya nchi. Anapaswa kutumia vyema rasilimali za nchi yake. Badala ya kuachia maofisa wake wala rushwa na wageni kuendelea kupora nchi yake, anapaswa kufikiria vyema asiendelee kuwa mtu wa ajabu duniani. Niliwahi kusoma katika moja ya magazeti ya Kenya yakidhihaki ziara zake nje ya nchi. Uchumi wa nchi Lebanon, Haiti, Palestina hata Rwanda ni mzuri kuliko Tanzania.



Kunapaswa kuwepo na sheria kuwazuia viongozi wote wala rushwa na watoto wao kuingia Ulaya. Simlaumu Kikwete, nawalaumu Watanzania kwa kuachia haya yatokee. Wanapaswa kuwajibika asilimia 100 kwa umaskini na matatizo yanayowakabili. Tusingependa waendelee kuombaomba, Wapo Waingereza hawana kazi, tungetumia fedha hizo (za misaada) kuwalipa malipo yao ya kutokuwa na ajira.” LindaCroucher

(www.guardian.co.uk/business/2012/jan/26/davos-2012-day-2)


Mheshimiwa Spika
, Tanzania iliyokuwa na sauti katika Mazungumzo baina ya Nchi za Kusini(Nchi zinazoendelea) na Nchi za Kaskazini (Nchi zilizoendelea) Tanzania iliyokuwa na sauti mstari wa mbele Kusini mwa Afrika, sasa imekuwa nchi ya kunyamaza kwenye masuala ya msingi kabisa kama haya. Kambi Rasmi ya Upinzani inauliza i-wapi sauti ya Watanzania katika anga la kimataifa? Serikali ya CCM imeipeleka wapi sauti hiyo ya Watanzania iliyokuwa ikiheshimika miaka ile wakati wa Mwalimu?



Mheshimiwa Spika
, hali ya Tanzania kupoteza sauti katika medani ya kimataifa pia ilidhihirika katika mkutano kuhusu mabadiliko ya tabia- nchi (COP 17) uliofanyika nchini Afrika Kusini; wakati nchi yetu ikiwa ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa mabadiliko ya tabia nchi kutoka hewa chafu inayozalishwa na mataifa makubwa (ambayo ndiyo tunayakimbilia kuomba misaada), Tanzania haikuweza kusema lolote. Tunaweza kukubaliana na watu wengine wanaotoa maoni kuwa ujumbe wetu katika masuala muhimu ya kimataifa kama hili ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia-nchi unahusisha watu wasiokuwa na ushawishi na diplomasia hitajika.



Mheshimiwa Spika,
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kuwa iwapo hatua za makusudi hazitachukuliwa kurejesha heshima na sauti ya Tanzania kimataifa maamuzi mengi yatafanyika yenye athari kwa wananchi wengi bila ushiriki wao thabiti kama yanayoendelea hivi sasa kuhusu Mikataba ya Kiuchumi na Nchi za Jumuia ya Ulaya (EPA) yenye madhara kwa wakulima na wenye viwanda nchini.
 
ni taarifa gani hiyo jamani?

attachment.php
 
Acha tu aiponde lakini ukweli umeshapatikana na unajulikana kwa kila mtanzania aayefuatilia siasa za nchi hii...

Maelezo yake(Wenje) kwamba ubarozi wa china unavuja kipindi cha masika na pia wanadiplomasia wetu huko china wanavunja sharia kwa kutembelea na gari zilitumika zaidi ya miaka 10 wakati sheria za China haziruhusu, hii utasema ni uropokaji?

Utawezaje kuhakikisha sharia za nchi hazivunjwi na raia wa china wakati sie tukiwa kwao tunazivunja sana...na ndio maana project za hapa bongo mpaka wanaohesabu vifusi kwenye barabara ni wachina...

LOL Shame Membe!!
 
Hiyo link ina uhusiano gani na Wenje?
Mkuu,

Si kama inahusiana na Wenje, bali Wenje alisoma maoni ya Waingereza dhidi ya Rais wetu; lakini kauli ya Membe kama ya Radhia Sweety, hawajaangalia SOURCE LINK na kufikiria.

Membe kakiri kuwa Guardian walifanya coverage ya JK vema akiwa Davos, jambo jema! Lakini kusema uki-google habari yenyewe unaishia JamiiForums ni kutoelewa search engines zinafanyaje kazi.

Maoni hayo yapo tovuti ya Guardian mpaka dakika hii na unaweza kuyaona kwenye link hii: Davos 2012: Day two, as it happened | Business | guardian.co.uk
 
Last edited by a moderator:
hayo yalikuwa ni maoni ya waingereza kwenye gazeti la the guardian. ..humu ndani(jf) hayo maini yaliletwa na mdau aliyeyasoma huko the guardian...membe anasema hayo ni maneno ya jf na yameanzia jf?!!! kweli!!???
 
Mkuu,

Si kama inahusiana na Wenje, bali Wenje alisoma maoni ya Waingereza dhidi ya Rais wetu; lakini kauli ya Membe kama ya Radhia Sweety, hawajaangalia SOURCE LINK na kufikiria.

Membe kakiri kuwa Guardian walifanya coverage ya JK vema akiwa Davos, jambo jema! Lakini kusema uki-google habari yenyewe unaishia JamiiForums ni kutoelewa search engines zinafanyaje kazi.

Maoni hayo yapo tovuti ya Guardian mpaka dakika hii na unaweza kuyaona kwenye link hii: Davos 2012: Day two, as it happened | Business | guardian.co.uk

Umeondoa kitufe cha Like. Maelezo yako mazuri ila sijui kama hawa makanjanja wanaelewa kitu lililopo ni kujihami hata ukimtaja jina lake, kwanza atalikana baadae kimya maana kesha jigundua amechamsha.
 
hayo yalikuwa ni maoni ya waingereza kwenye gazeti la the guardian. ..humu ndani(jf) hayo maini yaliletwa na mdau aliyeyasoma huko the guardian...membe anasema hayo ni maneno ya jf na yameanzia jf?!!! kweli!!???
Hapa ndo nami nimeshindwa kuelewa kama Membe alisoma hoja yenyewe na alielewa sababu ya watanzania kuhoji rais wetu kunangwa.

Kauli hii ilinishangaza, nikahisi labda kaambiwa tu, hajasoma! Kama alisoma basi alipitia bila kutafakari kwanini mantiki ya hoja hii, au aliisoma akiwa na majibu yake kichwani!
 
Back
Top Bottom