BUNGENI: Waziri Ghasia awasilisha Bajeti yake; mishahara yapanda

Huyu mdada cjui mmama, anayesoma mapendekezo ya kamat ya sheria na katiba. Anasoma hyo hotuba km anasimulia hadith watoto wa std 1. Mapoooz! Ndo mana mzee wa kiraracha anaamua kupiga mbonji.
 
somo la maadili, mapambano dhidi ya rushwa na uongozi bora kuanzishwa shuleni na vyuoni!
 
hicho ndicho kitanzi cha TZ, yaani "MATUMIZI = KIPATO". Na ndiyo maana matumizi (posho) ni 80% ya budget na maendeleo ni sehemu ya kinachobaki, sasa hayo matumizi yanatoka wapi!?
Mshahara ukipanda wakati nchi haina umeme, Serikali itakusanya kodi toka vyanzo vipi ili hiyo mishahara ilipwe?
 
Wenyewe wanasema mshahara lazima upande, ofcoz umepanda!

Sasa huu mgao wa masaa 18 kama utaendelea ni hakika makusanywa ya kodi yatakuwa chini ya makadirio na hivyo malengo ya bajeti hayatafikiwa. Kitakachotokea ni makampuni ya ujenzi kukopwa ili pesa za barabara zitumike kulipa mishahara. Serikali ingefanya tuu maamuzi magumu mfano ya kufuta ajira zisizohitajika mfano kwenye nyuo vya elimu ya juu vya serikali idadi ya watumishi ambao siyo walimu ni kubwa kuliko walimu; ukienda vyuo binafsi ni kinyume chake
 
Huyu mdada cjui mmama, anayesoma mapendekezo ya kamat ya sheria na katiba. Anasoma hyo hotuba km anasimulia hadith watoto wa std 1. Mapoooz! Ndo mana mzee wa kiraracha anaamua kupiga mbonji.
Mi hata sijamwelewa anafanya nin.. Anazungumzia tume ya maadili ya utumishi!
 
Haya sasa wapinzani ndio wanatia maguu, 40.2% ONGEZEKO RASMI LA MSHARAHA TUTALIJUA!
 
mishahara hata ipande kwa 200% matatizo ya msingi yatakuwa pale pale - kinachotakiwa ni ufumbuzi wa kudumu. mfanyakazi wa kima cha chini hata ukimpa Tshs 500,000/ leo bado haitamtosha.

So ni vyema tufikiri core problems badala ya kungoka nyongeza ya 5% toka kwa waziri.

Core problem ni kudhibiti mfumuko wa bei kwenye bidhaa muhimu za vyakula, vifaa vya ujenzi na usafiri aka petrol, dizel na mafuta ya taa. mpo ma griti sinkazi?

Timu mizizi usitibu matawi, ungonjwa upo kwenye mizizi ndugu zangu msidanganyike na hizi bla bla.

 
mishahara hata ipande kwa 200% matatizo ya msingi yatakuwa pale pale - kinachotakiwa ni ufumbuzi wa kudumu. mfanyakazi wa kima cha chini hata ukimpa Tshs 500,000/ leo bado haitamtosha.So ni vyema tufikiri core problems badala ya kungoka nyongeza ya 5% toka kwa waziri.Core problem ni kudhibiti mfumuko wa bei kwenye bidhaa muhimu za vyakula, vifaa vya ujenzi na usafiri aka petrol, dizel na mafuta ya taa. mpo ma griti sinkazi? Timu mizizi usitibu matawi, ungonjwa upo kwenye mizizi ndugu zangu msidanganyike na hizi bla bla.
Ofcoz nakubaliana na wewe! Susan Lymo anasema tatizo ni mfumo wa mshahala, kwani wanaofaidika ni wenye mishahara mikubwa!
 
mheshimiwa mchungaji Yohana Natse Mb. wa Karatu anawasilisha hoja yake!
 
Mkuu hiyo %imepanda kwa mfanyakazi husika au fungu zima la mshahara ndo limepanda kwa 40.2%?.

Mkuu hiyo % ni ya fungu zima la mishahara. Kumbuka hapo kuna ajira mpya haswa upande wa walimu na madaktari, annual increments na malimbikizo ya nyongeza za nyuma ambazo hazikuwahi kulipwa. Ni juzi tu tumesikia walimu wanatishia kugoma sababu wanadai malimbikizo!!!!!

Hata hivyo usishangae kesho kwenye magazeti wanatoka na vichwa JK aongeza mshahara 40%!!!!!!
 
Mkuu hiyo % ni ya fungu zima la mishahara. Kumbuka hapo kuna ajira mpya haswa upande wa walimu na madaktari, annual increments na malimbikizo ya nyongeza za nyuma ambazo hazikuwahi kulipwa. Ni juzi tu tumesikia walimu wanatishia kugoma sababu wanadai malimbikizo!!!!!Hata hivyo usishangae kesho kwenye magazeti wanatoka na vichwa JK aongeza mshahara 40%!!!!!!
Nimekupata mkubwa!
 
Back
Top Bottom