Bungeni viroja vitasikika!!!!

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Dec 13, 2009
3,407
266
tasunyata kama kinda,
ni spika wetu makinda,
sheria sasa zamdinda,
na hoja anazisunda.

wengi tumeshuhudia,
kwanza kilipowadia,
hasira kukusudia,
leo nimeshuhudia.

bunge limekosa spika,
viroja vitasikika,
aibu itawashuka,
kutuletea gebuka.

mengi tuliyoyahisi,
tutayasikia sisi,
makinda kajifilisi,
kweli mfupa wake fisi.

leo bungeni aibu,
kama za moto kababu,
ziwe mdomoni mwa bubu,
makinda akawa dubu
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom