Elections 2010 BUNGENI: Upinzani upo ndani ya kambi ya upinzani?

Tonge

JF-Expert Member
May 7, 2010
696
12
Kwa mtazamo wangu nimeyapokea matokeo ya uspika (makinda kura 265 na marando kura 53) kama kuna upizani ndani ya kambi ya upinzani ambao ulianza wakati wanachagua kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.

Nimesikia CUF nao watachagua kiongozi wao licha ya chadema kumchagua mbowe kutokana na kutimiza masharti kwa kanuni za bunge.

Huu ni mpasuko ndani ya kambi ya upizani na haswa huletwa na CUF, niwaombe wabunge wa upinzani kukaa ili waweze kutoa hizi tofauti zao, maana kama wanataka kuibomoa CCM lazima wawe kitu kimoja.
 
Hakuna kukaa.nasema mawazo haya ni potofu.cuf wana ndoa na ccm,nccr kadhalika,tlp ndo usiseme.udp mnajua.chadema nenda mwenyewe.jenga upinzani hadi kieleweke.nafurahi wapinzani feki wameonekana mapema.chadema mwendo mdundo.
 
Tatizo CUF wanajiona wako serikalini baada ya Kupata umakamu wa Rais na baadhi ya mawaziri ZNZ (wananguvu sawa na CCM kwa nini wawe chini ya CDM), siajabu kuona wanaungwa mkono na NCCR chama cha Mr Mbatia.

Baada ya Oparesheni Sangara kutoa mafanikio makubwa kanda ya ziwa CDM waje na Oparesheni KIBUA au Oparationi KAMBA mikoa ya kusini ili kutoa adabu 2015.
 
sijue kupingana pingana ndio nini maana upizania ndani ya upinzani, CUF v/s Chadema kunani au kimojawapo CCM-B, kwanini wasielewane ndio maana hat wakati wa kampeini vijembe vyote vya kafu vilielekezwa kwa chadema hii sio shwali kabisa kuleta ukombozi wa walala hoi, sitawashaangaa kuwa chama kimojawapo kinakamilsha matakwa ya CCM
 
Mimi naona ni vizuri sana kwa chadema kwamba upinzani umejipambanua mapema. Hiyo itawasaidia kujua wanatakiwa kugangamala kwa kiasi gani. Ingekuwa mbaya sana kama mafisi yaliyovaa ngozi ya kondoo yangeendelea kuonekana machoni pa Chadema kama kondoo lakini sasa waliovaa ngozi ya kondoo wameshajidhihirisha kuwa ni mafisi. Sasa ni rahisi kwa Chadema kupanga mikakati na mbinu nzuri zaidi za ukombozi kwa kuwa wanawajua maadui wanaowazunguka na nguvu zao.
 
Nimepigwa butwaa almanusura nizirai baada ya kuona idadi ya kura alizopata spika Maran....Aaaah samawani mgombea spika Bwana Marando,inaonekana kuna kukomoana bungeni au kutumikia wananchi?Inaonekana vyama vingine vya upinzani havijampa Marando kura why????
 
chama cha upinzani tz ni chadema peke yake.chadema itasimama zaidi ikiwa peke yake kuliko hawa ccm b wanaojichimbia kaburi. Umaarufu wa cuf bara unashuka kwa kishindo, subiri uone 2015 zanzibar watapata chama halisi cha upinzani na hapo ndio tutafanya hitima ya cuf.
cafu kwa bara ni mfu..
 
CUF wana makubaliano na CCM kuendesha serikali huko zanzibar. Hatujui limit ya makubaliano hayo. It is politically dangerous to have a complete faith on them without depth knowledge of their agreement.
 
CUF lazima wakubali kuwa lazima wawe chini ya CHADEMA

kuna mchanganyiko wa kikatiba, CUF wameunda serikari na CCM Zanzibar, hakiwezi kuwa chama pinzani bara. hayo ndio matunda ya kufanya mambo chini ya meza wenyewe, huku bara wataungana na CCM kujibu hoja za chama cha Upinzani pekeeee Chadema,
 
Jamani kumbukeni kwamba hata Zanzibar CUF waliingia kwenye makubaliano baina yao na CCM. Na hawakushirikisha chama chochote kingine.

Nawashangaa ambao mnaamini kuwa CUF wanaweza kuwa na ushirikiano na Chadema ktk bunge la JMT wakati huo huo kuwa na ushirikiano na CCM katika baraza la wawakilishi Zanzibar! Only a foul will buy this idea. Kumbukeni CCM ni ile ile ya Zanzibar na Bara na vile vile kwa CUF.

Kama mlifuatilia kwa makini mwenendo wa Prof. Lipumba wakati wa kampeni, kutangazwa matokeo na kisha kuapishwa kwa Rais wa JMT ni wazi alikuwa against Chadema zaidi kuliko ambavyo alikuwa against CCM. Kifupi alikuwa akimpigia kampeni JK. Na hii yote ilitokana na kutotaka kuharibu ndoa yao (ulaji wao) na CCM kule Zanzibar.

In short, hizo ndo hulka za viongozi wa bara la Afrika. Wamejaa ubinafsi na uzandiki.

Maalim Seif ameshasahau watu waliomwaga damu na maelfu kukimbilia nchi zingine kama wakimbizi!!
 
Ni kitu bora kumtambua adui yako kuliko kutomtambua Chadema mwendo mdundo kama wamezira wenzao twala chagueni baraza la mawaziri kivuli timu yenu inatosha achana nao.
 
Nimesoma kwenye gazeti la Majira 12/11/2010 kuwa Mbowe aliongea na Hamad Rashid kuhusu umoja lakini Mbowe alimuuliza kuhusu muafaka wa Z'bar na Hamad Rashid akatoa sharti la umoja huo kuwa na vyama vingine viingizwe ndipo Chadema wakachomoa! Pia nafikiri kitendo cha Prof. Lipumba siku ya kutangazwa mshindi wa Urais kukabidhi ilani ya CUF 2010 - 2015 kwa CCM inamaanisha muungano wa CUF na CCM.

GAZETI HURU LA KILA SIKU:
 
Wapendwa msishangae hayo ndo majira ya kutuonesha kuwa kuna vyama vya upinzani ambavyo ni matawi ya sis em. Kwa nini CDM wasifanye Operation matowola Tabora?
 
CUF ni chama cha upinzani cha vyama vya upinzani. Kimeanza kuzeeka mapema sana na kwa kasi ya ujabu. Mpaka kufika 2015 si ajabu walio ndani yake watataka kujitoa ili waanzishe CUF nyingine au chama kingine.
 
Kwa mtazamo wangu nimeyapokea matokeo ya uspika ( makinda kura 265 na marando kura 53) kama kuna upizani ndani ya kambi ya upinzani ambao ulianza wakati wanachagua kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, nimesikia cuf nao watachagua kiongozi wao licha ya chadema kumchagua mbowe kutokana na kutimiza masharti kwa kanuni za bunge, huu ni mpasuko ndani ya kambi ya upizani na haswa huletwa na cuf, niwaombe wabunge wa upinzani kukaa ili waweze kutoa hizi tofauti zao, maana kama wanataka kuibomoa ccm lazima wawe kitu kimoja.

Bungeni kuna kambi mbili. Upinzani na chama tawala. So kama CUF na wenzao kama TLP hawako Upinzani, wao ni chama tawala (CCM). Full stop
 
KWELI hawa wabunge wa cuf,nccr, TLP naUDP ,ni watu wa maslahi. ni hovyo kabisa.yaani bora wapige kura kwa ccm!! tumewaona na sasa tunawatambua! mti wenye matunda ndio hutupiwa mawe. chadema itasonga hata bila nyie wanafiki
 
Kwa mtazamo wangu nimeyapokea matokeo ya uspika ( makinda kura 265 na marando kura 53) kama kuna upizani ndani ya kambi ya upinzani ambao ulianza wakati wanachagua kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, nimesikia cuf nao watachagua kiongozi wao licha ya chadema kumchagua mbowe kutokana na kutimiza masharti kwa kanuni za bunge, huu ni mpasuko ndani ya kambi ya upizani na haswa huletwa na cuf, niwaombe wabunge wa upinzani kukaa ili waweze kutoa hizi tofauti zao, maana kama wanataka kuibomoa ccm lazima wawe kitu kimoja.

"Tuna asilimia 12.5 ya wabunge na hiyo inatupa nafasi ya kuunda kambi ya upinzani bungeni," alisema Mrema. Sasa swali sijui hawakujua kuwa asilimia 12.5 zao zingeweza kuwafanya washinde uspika? na hata wale CCM waliokuwa hawakufurahishwa na Anna Makinda kugombea waliona uroho wa chadema wa madaraka wakaona hawa wameshachuku KUB wakichukua na Uspika itakuwa balaa nadhani Chadema ni chama kinachoshabikia suala la uditekta wenye upeo wale ma great thinkers changieni bila unazi wa vyama.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom