Bungeni tumepeleka wawakilishi au kina Yuda Eskariot? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bungeni tumepeleka wawakilishi au kina Yuda Eskariot?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jul 29, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 23,310
  Likes Received: 32,100
  Trophy Points: 280
  Ukitafakari mwenendo wa bunge letu na nini wajibu wao kwa umma utagundua bunge letu kwa kiasi kikubwa limesheheni kina Yuda Eskariot na si wawakilishi na watetezi wa watanzania.Tafakari mambo haya:-
  1.Wabunge kupokea rushwa na kusaliti watanzania
  2.Kuweka mbele maslahi ya chama badala ya wapiga kura wao
  3.Wabunge kupitisha maazimia ya bunge kwa mbwembwe na kutosimamia utekelezaji wake
  4.Wabunge kuungana kutete serikali badala ya kuisimamia na kuishauri
  5.Bunge kupitisha miswada au kurekebisha sheria ambazo zinakuwa kandamizi kama hii inayohusu mifuko ya jamii alafu wao wapitishaji(wabunge) haiwahusu
  6.Watu kufa kutokana na mgomo wa madaktari,ajali za meli na mengineo alafu bunge linazuiwa kujadili
  7.Mbunge kutotembelea jimbo lake mpaka wakati wa uchaguzi na kuishi mbali na jimbo lake
  8.Mbunge kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja baada ya kulalama ktk kuchangia.

  Kazi kwenu wapiga kura.Mimi mwenzenu najiandaa kuama nchi.
   
 2. m

  magohe JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kwani kuna bunge hapo? Au limejaa wagonga meza tupu,wala rushwa,wapenda posho kwani ukitaka kuamini tazama mahudhurio yao kwa sasa walipoambiwa mtu atachukua posho iwapo atahudhuria asubuhi na jioni na yale ya awali kabla ya sheria hiyo,watoa mipasho badala ya hoja kama akina mwigulu,lusinde na komba huku wengi wao ni partsan wenye kushabikia mambo bila kufikiri na matokeo yake kupitishwa kwa baadhi ya sheria na mikataba mibovu mfano mifuko ya jamii(nssf) iliyoibuka hivi karibuni kwa watumishi,wateteaji wa mishahara yao binafsi na si kutetea maslahi ya watumishi wengine km vile madaktari,walimu,polisi na wengine wengi ambao kimsingi ndio wanaowatumikia wapiga kura majimboni mwao kwa ukaribu zaidi.
  Hao ndo wabunge wa tanzania bana!! na laiti kama wananchi wote tz tungekuwa watu wa kudadisi kwa undani basi tusinge thubutu hata siku moja kujitokeza kuchagua uozo huu na kuacha nchi bila ya kuwa na mhimili huu kati ya ile mitatu inayoongoza nchi.it is a ridiculous parliament in its silly season with Definitely silly members of parliament who I never seen them acting like this to their voters elsewhere in the world except tz.shame on them!!!!
   
Loading...