Bungeni: TLP, CUF, UDP na NCCR Mageuzi navyo vyaungana

PayGod

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
1,259
57
Baada ya chadema, kutangaza kiongozi wao wa kambi ya upinzani bungeni, vyama vingine vinne vimeamua kuungana na kuwa na kiongozi wao huko bungeni vyama hivyo ni TLP, CUF , UDP NA NCCR MAGEUZI

source TBC1( MUKTASARI WA HABARI)
 
Huu ndiyo wakati ambapo huwa ninatukana ninaambulia kula ban.

Hao wanafiki, walamba-miguu ya mafisadi, kina Mrema wanakwenda kufanya nini bungeni.

Hivi?

Kishumundu iko Vunjo??
 
Siielewi vizuri hii, ina maana kutakuwa na viongozi wawili wa upinzani mjengoni au? This division will always tear us apart!
 
Wana JF nimepata habari kuwa CUF imesema haitashirikiana na CHADEMA kuunda serikali ya upinzni ramsi bungeni. Na wanasema wao watashirikiana na vyama vya NCCR Mageuzi na TLP kuunda kambi yao ya upinzani bungeni.

Source: Mlimani TV leo saa 1:30

Hiki nacho ni kituko gani wajamaa!!!! Huu ni wivu ama ni nini? Mimi nafikiri adui wa rafiki yako ni adui yako. Sasa bunge hili linaonekana kuwa kituko, kambi tatu zinazopingana?

Haya wana JF mnasemaje?
 
Halafu wakiitwa mapandikizi ya CCm wanatishia kwenda mahakamani, kwani chadema wamesema hawatawashirikisha katika kambi ya upinzani? mbona bunge lililopita kiongozi wa upinzani alitoka CUF na wala hatukusikia Chadema wakioungana na uDP kuupata kiongozi wao? hivi hii sio Mrema's make? enh I think Mrema and Mbatia wameanza kufanya kazi waliyotumwa!
 
Mzee wa Kilaracha akiwa Dodoma leo nadhani atawaunga mkono CCM kwa nguvu zote.

mrema-kimeo.jpg
 
Huu ndiyo wakati ambapo huwa ninatukana ninaambulia kula ban.

Hao wanafiki, walamba-miguu ya mafisadi, kina Mrema wanakwenda kufanya nini bungeni.

Hivi?

Kishumundu iko Vunjo??

kishumundu ipo uru jimbo la moshi vijijini. wanafiki lazima wawe na mnafiki mkuu!
 
CUF sasa ni tawi la CCM.
Inawezekana wameahidiwa kitu na JK. kinachowapa kiburi CUF ni kule Zanzibar tu.
 
chama cha mapinduzi kinashika hatamu!! mmeona sasa kuwa siasa si rahisi kisi hicho mnachoamini?? mlidhani upinzani ungetikisa kumbe sasa ndio unaotikiswa!!
 
WAO WALIWASHIRIKISHA MBONA NYIE MMEAMUA KUUNDA UPINZANI BUNGENI PEKE YENU? KWALI SINA PhD lakini sidhani kama hata mngekuwa nyie ndio mliwashirikisha wao then wao wakawatenga mtakubaliana nao kushirikiana ilhali wamewafanyia ubinafsi.
 
CUF sasa ni tawi la CCM.
Inawezekana wameahidiwa kitu na JK. kinachowapa kiburi CUF ni kule Zanzibar tu.

Let them go to hell. Hao ni ccm B na watakuwa wameshawishiwa kufanya hivyo kupunguza nguvu ya upinzani, imagine Mzee wakiraracha aungane na wengine yeye ndio atataka kuwa kiongozi. Hakuna shida Chadema ndio chama pekee cha upinzani hao wengine wako kimaslahi zaidi.
 
Wana JF nimepata habari kuwa CUF imesema haitashirikiana na CHADEMA kuunda serikali ya upinzni ramsi bungeni. Na wanasema wao watashirikiana na vyama vya NCCR Mageuzi na TLP kuunda kambi yao ya upinzani bungeni.

Source: Mlimani TV leo saa 1:30

Hiki nacho ni kituko gani wajamaa!!!! Huu ni wivu ama ni nini? Mimi nafikiri adui wa rafiki yako ni adui yako. Sasa bunge hili linaonekana kuwa kituko, kambi tatu zinazopingana?

Haya wana JF mnasemaje?
YALIANZIA WAPI???:smile-big: CHADEMA WALISHASEMA HAWAHITAJI USHIRIKIANO NA VYAMA VINGINE MARA HII MMESHASAHAU...:smile-big:
 
Am I dreaming? someone tell me this is not true? yaani tulianza kufikiri sasa wakati wa CCm umefika kumbe ndio kwanza kazi inaanza! ama kweli nimeamini Msaliti hana rangi!
 
Nafikiri CHADEMA wanatakiwa kutambua kuwa watanzania wanawaangalia wao kwa uongozi wa upinzani bungeni. Na kiongozi mzuri ni yule mwenye kuunganisha watu wake. Bunge lililopita Hamad alikuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kwa nini wasimpe hata umakamu this time?. Mnawakatisha tamaa watanzania kwenye hili na mjue kuwa mvua huwa hainyeshi upande mmoja 2015 inaweza ikanyeshea upande mwingine.

Kumaliazika kwa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi ujao. CCM watatumia miaka mitano hii kuhakikisha CHADEMA kinakuwa hoi kabla ya 2015, believe me CHADEMA onesheni uongozi, acheni ubabe wabebembeleni CUF kwa mustakabali wa CHADEMA 2015
 
YALIANZIA WAPI???:smile-big: CHADEMA WALISHASEMA HAWAHITAJI USHIRIKIANO NA VYAMA VINGINE MARA HII MMESHASAHAU...:smile-big:
Oya wewe mkenya nini maana watanzania si unawajua ni mabingwa wa kusahau????????????? nakushangaa unalikumbuka hili nadhani ngoja waachiwe huo uwanja waweze kujitutumua vizuri........
 
Ukiangalia ndoa ya CUF na CCM kule Zanzibar ni vigumu sana kuamini kuwa CUF inaweza kushirikiana na Chadema kwenye kambi ya upinzani. I was skeptical kwa mara ya kwanza nilipoona eti CUF na Chadema watashirikiana. Labda kama CUF ni mbili. Lakini ikiwa CUF ni moja siamini kuwa CUF ile ile inaweza kuwa na alliance na Chadema.

CUF vile vile kwenye bunge la muungano wanajiona kama losers kwani wamepoteza nafasi yao ya kuwa main opposition party. Wamepoteza nafasi yao ya kuwa main opposition party kwa Chadema si CCM. Kwa hiyo naturally CUF haiwezi kumpenda Chadema. Hata ukiangalia kwenye uchaguzi, inaelekea strategy ya CUF na CCM ilikuwa inafanana na wameshinda wote maeneo ya pwani. Kwa hiyo in future ukiangalia vizuri kwenye kurunzi, CUF wanajiona kuwa hawako tofauti sana na CCM.

Hata kampeni zao unaweza kuona kuwa CUF hawakuwa against CCM kihivyo.

Jingine ni kuwa CCM wanauona wingi wa Chadema kama threat kwao. Hivyo wako tayari ku-extend mkono kwa chama kingine. Naturally NCCR alikuwa ni direct ally wa CCM. Kampeni za kawe zilithibitisha kuwa NCCR was more against Chadema kuliko against CCM. Hili ni la muda kidogo. NCCR kina MPs wanne tu. Kwa hiyo CCM kumvutia CUF upande wake ni kupunguza nguvu ya upinzani kwani wabunge 45 wa Chadema ukijumlisha na 30 wa CUF, opposition ilikuwa inakuja na wabunge 75. Hiyo si nguvu ya kupuuza kwa CCM hivyo kwao itakuwa vizuri Chadema wakibaki peke yao.

Overall ni kuwa katika Bunge lijalo opposition itakuwa ni chadema peke yao. Na hilo litawajenga zaidi. Hawa wengine kina UDP, TLP, NCCR na CUF obviously watahamia kwa CCM. Pepo zote za kisiasa zinaonesha hivyo.
 
WAO WALIWASHIRIKISHA MBONA NYIE MMEAMUA KUUNDA UPINZANI BUNGENI PEKE YENU? KWALI SINA PhD lakini sidhani kama hata mngekuwa nyie ndio mliwashirikisha wao then wao wakawatenga mtakubaliana nao kushirikiana ilhali wamewafanyia ubinafsi.

nashukuru mkuu umeiona point, chadema wanajiona vichwa juu kwa wabunge 45 tu wakati cuf in 34. bunge lililopita chadema walikuwa na 11 na walipewa nafasi ya naibu kiongozi wa pinzani leo cuf in 34 hakupewa hata nafasi ya naibu, eti wamekapa ka-zito, sijui wanakaogopa katavuruga chama? kusema kweli kama chama kinaweza kuvurugwa na kavulana kama zito, basi hakuna chama hapo na nashukuru Mungu hakikushinda uchaguzi. hata kama kura zilichakachuliwa, zitabarikiwa na Mungu, hikichama walahi kingeichakachua nchi nzima kwa ubinafsi. kueni kwanza (watoto wote mnaoishabikia chadema) mtayaona!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom