Bungeni: Taarifa ya tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne yasomwa

mbona hizi alama ni sahihi, hata vyuoni wanatumia hiyo kitu?. Wewe umesoma wapi?. Ulitaka alama 21-40 iwe C?.

Mkuu naona utakuwa umekunywa viroba, Au labda ww una umri kama wa lemutz lakin mimi NECTA naijua kwani si miaka mingi imepita ambapo nimeshuhudia maafa ya hili baraza la mitihani.
 
alama za miaka ya nyuma hizi hapa.

F: 0-20
d: 21-40

c: 41-60

Hata kama alama ziweje bado sio suruhisho kwani mwanafunzi ili awe katika nafasi nzuri ya kujiendeleza kielemu bila zengwe apate angalau credit tatu ambazo kwa kiwango ulicholeta wewe zinaanzia 41 potelea mbali hata kama walitumia viwango vipya yaani D inaanzia zaidi 35 angalau basi division four zingekuwa nyingi kama ni hivyo maana kwa mwanafunzi ambae amefundishwa inakuaje masomo yote apate chini ya 35 ina maana hakuna hata masomo mawili ambayo anapata zaidi ya 35 na kupata divison four? (maana ukipata D mbili tu ni division four hivyo kwa waliopata zero hao ni vilaza maana kama issue ni viwango vya ufaulu haina mashiko maana haiwezekani masomo yote wewe ukapata chini 35 na kila siku unakwenda shule, kinachotakiwa hapo ni kuangalia sababu ya kufeli maana kuna ambao hawana waalimu na kuna wengine wana waalimu lakini bado wamefeli)
 
Mkuu CHAMVIGA leo mpaka mwili umetetemeka aiseee, kuna ndugu yangu huku alijinyonga na watu wakalia sana, sasa sijui hao waliokufa itakuwaje?
Haki inatafutwa kwa kupigana sio kwa kujiua mwenyewe, then what? Ingawa inauma kupoteza hao ndugu zetu lakini tuangalie na yule aliyeandika mashairi, mchora mazombi angejinyonga ungesema naye alionewa.
 
Last edited by a moderator:
0-20 =F
21-40 =D
41-60=C
61-80=B
81 -100=A kwa zamaszetu

Pamoja na kwamba viwango vya ufaulu hasa hicho cha daraja la F kilikuwa chini bado wanafunzi wengi enzi hizo walikuwa wanapata Division 3, division two na one nazo zinakuwepo huku division zero zikiwa chache mno na four nazo zinakuwa chache
 
Huu ni ushenzi aisee hapa siasa iwekwe pembeni na tukiruhusu siasa kuingia kwenye elimu yetu tutaharibu hii nchi,mimi nina mtoto wa mama yangu mdogo kapata division 4 nikampeleka akarudie akapewa mtihani wa form two akapata alama 42 kati ya mia sasa kama mtu huyu mtihan wa form two karudia akapata ivyo unakuja ku standardize ili iweje? Waache ujinga huu mkubwa wanaotaka kufanya
 
Hiyo ndiyo tuliyotumia sisi enzi zetu za miaka ya tisini mwanzoni.

Wakati huo:
B= 61-80

A=81-100

Hata mie na walimu wangu tulidhani ndiyo hivyo lakini hizi hazijawahi kutumika mahali popote Tanzania

 
usiteswe na mainstream info,,mitaala ipo,ka unataka uhakika kamuulize mwanao ushaiona syllabus atakujibu,,,nime proove kwa macho yangu,,tena ni mipya yaani ya 2012
Mkuu hivi siku hizi Syllabus ndiyo imekuwa Curriculum?
 
watu wengine kwa ubishi,,alama ndo hizo unazopinga,,,
Sio Kosa lako, Hata mimi niliamini hivyo. Mbaya zaidi hata walimu wangu walijuwa hivyo. Sikushangai kudai kuwa D inaanzia 21. Mwenye waraka au andiko lolote la NECTA atuwekee humu tusiishie tu kuamini kitu ambacho hakijawahi kuwepo.
 
ccm watu wazima kabisa akili zimekuwa kama watoto, wameshusha viwango vya ufaulu bado wanetu wamefeli... sasa wanashusha viwango vya usahihishaji ili ionekane wanetu wamefaulu... wanataka kumridhisha nani kama sio kutupumbaza sisi wenye watoto waliofeli? Upuuzi wa serikali umeshapita kiwango cha watu wa kawaida kuuelewa, ni wakati wetu kuamka na kusema tunachotaka maana itafika mahala watasema wanetu wasifanye mitihani waendelee tu kusoma... na sisi pia tutaridhika kwa kuona wanetu wanasoma mpaka vyuo vikuu lakini watamaliza na degree wakiwa hawajui hata kuandika majina yao..!
 
Una uhakika na ulichokiongea?
Mkuu, asilimia 100%....Huwa sibishi kitu nisichokijua...Kwa hili najuwa iko siku mambo yatakuwa hadharani na utaelewa kwanini naema hivyo....Jiulize kwanini Pass mark ya form II ni 30?? Kwanini wao NECTA D ianzie 21 si ni kituko hicho?
 
Haya yote yanawezekana TZ only, je wale ambao wameshajiunga na kidato cha 5 itakuwaje kama matokeo yao yamefutwa?
 
Mkuu, asilimia 100%....Huwa sibishi kitu nisichokijua...Kwa hili najuwa iko siku mambo yatakuwa hadharani na utaelewa kwanini naema hivyo....Jiulize kwanini Pass mark ya form II ni 30?? Kwanini wao NECTA D ianzie 21 si ni kituko hicho?
Nadhani hujui unachokiongea, kwani umeambiwa 21 ni F, mbona bado 30 ya FTSEE ni D na ipo ndani ya range ya D ile ile! Kinachotakiwa pale ni mwanafunzi wa FTSEE kama atapata alama D basi iwe ni ile ya juu kidogo kumuwezesha kupambana na masomo magumu kidogo ya ngazi inayofuata.

Usitake kulinganisha mtihani wa FTSEE na CSEE/ACSEE/DSEE/GATCE nk. Kwanza hata mamlaka zinazohusika na utungaji, usahihishaji na utoaji matokeo ni mbili tofauti.
 
Nadhani hujui unachokiongea, kwani umeambiwa 21 ni F, mbona bado 30 ya FTSEE ni D na ipo ndani ya range ya D ile ile! Kinachotakiwa pale ni mwanafunzi wa FTSEE kama atapata alama D basi iwe ni ile ya juu kidogo kumuwezesha kupambana na masomo magumu kidogo ya ngazi inayofuata.

Usitake kulinganisha mtihani wa FTSEE na CSEE/ACSEE/DSEE/GATCE nk. Kwanza hata mamlaka zinazohusika na utungaji, usahihishaji na utoaji matokeo ni mbili tofauti.

Naelewa sana ni nachokiongea kuliko wewe unavyodhani. Huo nimekupa tu kama mfano...Hoja hapo ni kama pass mark ya form II ni 30 Kwanini mnalazimisha pass mark ya form IV iwe 21?

Kwamba mitihani ya Form II iko chini ya Ukaguzi Kanda hilo nalifahamu pengine kuliko wewe unavyodhani unalifahamu...Hoja yangu D ya NECTA haijawahi kuwa 21 Tangu baraza lianzishwe.....

Kwa kukusaidia wewe na wale wanaoendelea kujidanganya rejea taarifa ya tume iliyoundwa KUHUSU KUSHUKA KWA KIWANGO CHA UFAULU WA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA 4 MWAKA 2010 katika ukurasa wa 87
.......

....."Utafiti pia umebaini kuwa kuna tofauti ya uelewa kuhusu alama za gredi zinazotolewa
kwa watahiniwa. Aidha, uzoefu wa miaka mingi unaonesha kuwa Gredi zinatolewa
kwa kuzingatia mlolongo wa alama zifuatazo: A (81-100), B (61-80), C (41-60), D (21-
40), F (0-20). Hata hivyo NECTA imethibitisha kuwa alama za gredi zinazotolewa kwa
watahiniwa huamuliwa na jopo la wasahihishaji wa somo husika kwa kuzingatia
kiwango cha ufaulu kwa mwaka husika na hivyo hakuna alama maalum zilizowekwa
kwa kila gredi. Pia NECTA ilibainisha kuwa gredi D huwa si chini ya alama 30
na A si
chini ya alama 70."


Katika maoni yake (Ukurasa 120) taarifa ya tume inasema......."Kuna tofauti ya taratibu zinazotumika kupata gredi katika mitihani ya Taifa na zile zinazotumika kupata gredi hizo katika mitihani ya shule. Hali hii inasababisha watahiniwa kutopata gredi stahiki, hivyo kuathiri ufaulu"

Sasa mnaosema D ni 21 nileteeni andiko vinginevyo mnajidanganya na kuendelea kudanganyika.

cc grafani11,
nyangi m.a
Suip

 
Aiseee!

Kusahihisha upya ili kuwe na "standardization"? Hii ni hatari kubwa sana...!
 
Back
Top Bottom