Bungeni: Spika anapaswa kuwa mwanasheria ili kudhibiti kazi zake vyema.

mwitaz

JF-Expert Member
Feb 19, 2012
315
93
Baada kutafakari kwa kina kirefu kuhusu shughuli za Bunge la Jamhuri ya Tanzania nimegundua kuwa kuna udhaifu mkubwa ambao inanilazimu kusema kuna ulazima wa kubadilisha katiba ili kutia sharti ambalo litamruhusu mtu aliyosomea na kubobobea katika Sheria ndiye atakayepaswa kugombea Uspika wa Bunge ili kufanya kazi za Bunge kwa umahiri.

Tazama mfano mmoja hai unaonekana katika ujumbe wa Mhe. J. Mnyika katika mtandao wa www.facebook.com ufuatao hapa chini:-

"Kwanini niliomba
muongozo-Sakata la
Mgomo wa Madaktari
Leo, Juni 22, 2012 nilitaka
kuomba muongozo wa
Spika kwa mujibu wa Kanuni 49 (2) baada ya
Waziri wa Afya kutoa kauli
juu ya utekelezaji wa madai
ya madaktari.

Kanuni hiyo
inataka kauli isiwe ya
kuzua mjadala lakini aliyoyaeleza waziri juu ya
uboreshaji wa maslahi ya
madaktari yanazua mjadala
kwa kuwa yanatofautiana
na majibu ya Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda aliyoyatoa bungeni jana, (Juni 21,
2012) na pia hayana uhalisi.
Mathalani, wakati serikali
ikidai imeongeza posho ya
kuitwa kazini (on call
allowance) toka Februari, 2012 na kutumia bilioni 7.9
kwa miezi michache,
imetenga kwa watumishi
wa Afya bilioni 18.9 tu kwa
mwaka mzima wa
2012/2013 kiwango ambacho hakitoshi.

Hivyo nilitaka kuomba
muongozo Spika awezeshe
kauli hiyo ijadiliwe kama
ilivyokuwa kwa kauli juu
ya fedha za rada.
Nakusudia kumuandikia barua Spika kushauri
aelekeze kamati ya bunge
ya huduma za jamii kauli
hiyo ya waziri.

Pia bunge halipaswi
kunyimwa fursa ya
kutumia mamlaka yake
kwa mujibu wa ibara ya 63
ya kuishauri na kuisimamia
serikali kusuluhisha mgogoro na madaktari ili
kuepusha mgomo wenye
athari kwa nchi na
wananchi kwa kisingizio
cha kusudio la serikali
kupeleka mgogoro mahakama kuu kwa kuwa
mpaka leo taarifa
iliyotolewa bungeni bado
hakuna shauri katika
kitengo cha kazi.

Hivyo,
Spika anapaswa kutoa jukumu kwa kamati husika
ya bunge kuendelea na
usuluhishi kabla ya serikali
kukimbilia mahakamani. Wabunge tupewe nakala ya
taarifa ya majadiliano ya
pande mbili yaliyochukua
zaidi ya siku 90 badala ya
kupewa hotuba ya nusu
saa ya upande mmoja wa serikali pekee.

Hata serikali ikizuia mgomo
wa wazi kwa zuio la
kimahakama ieleweke
kuwa mgomo wa chinichini
kwa watumishi wa afya
ambao una athari ya muda mrefu kwa maisha ya
wananchi nchini.

Mwisho, serikali ipunguze
matumizi yasiyo ya lazima
na ipanue wigo wa mapato.

John John Mnyika.
Mbunge Jimbo la Ubungo
(CHADEMA)
22 Juni, 2012
 
Mijadala ya bajeti huchukua asilimia kubwa ya muda wa vikao vya bunge yaani zaidi ya asilimia 70. Vituko vingi kama kufukuzana ukumbini au mbunge kuadhibiwa na bunge hutokea wakati wa bunge la bajeti.

Ni nadra sana kukuta mitafaruku hii kutokea kwenye vikao vile vya Novemba, February na Aprili ambavyo ni vika 10 kwa session na ndivyo vinavyopitisha miswada mingi kuwa sheria.

Hivyo, basi harakati nyingi ni wakati wa bajeti kama tunavyoona sasa. Na kama ni hivyo basi Spika anatakiwa awe na uelewa mkubwa wa mambo ya fedha na kama ni sheria basi ni kidogo tu.

Hivyo, kwa Anne Makinda ambaye ni mtaaluma mzuri wa accounts basi uspika ndiyo saizi yake.
 
Back
Top Bottom