Bungeni: Ripoti ya Jairo yawasilishwa, wabunge wachachamaa!

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975
Mwenyeketi wa kamati ya nishati na madini january anamalizia kuongea na baada ya hapo spika atamwita mwenyekiti wa kamati ndogo ya bunge iliyoundwa kuchunguza sakata la Jairo. Tuendelee kujuzana.

UPDATED:

Jairo, Luhanjo na Ngeleja wabanikwa Bungeni!


Spika Makinda

Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza sakata la malipo ya mamilioni ya shilingi kwa watendaji wa Wizara ya Nishati ili kusaidia bajeti ya wizara hiyo ipite katikati ya mwaka huu imewasilishwa Bungeni na kuonesha kuwa malipo hayo hayakuwa halali na ulaghai mkubwa umefanyika na hivyo kutaka wahusika wawajibishwe.

Taarifa hiyo imesema kuwa baada ya kupitia ushahidi wote na kuwahoji watu mbalimbali imehitimisha kuwa "utaratibu wa uchangishaji wa fedha uliofanyika katika Wizara ya Nishati na Madini haukuwa na uhalali wowote kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Kanuni za Fedha za Umma." Ripoti hiyo pia ilimtuhumu Katibu Mkuu Bw. Luhanjo kutosema ukweli kuhusu utaratibu huo. "Kamati Teule imeridhika pia kwamba huo siyo utaratibu wa kawaida kama ilivyoelezwa na Katibu Mkuu Kiongozi katika Taarifa yake kwa Umma kupitia Vyombo vya Habari kuhusu Uchunguzi wa Awali" imesema ripoti hiyo.

Ripoti hiyo imeeleza pia kuwa fedha zilizotumika kutekeleza agizo la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo hazikutoka kwenye bajeti yoyote iliyowekwa kwa ajili hiyo bali zilichotwa kutoka katika akaunti mbalimbali zilizokuwa zimetengewa fedha. "Nyaraka za matumizi halisi zinaonyesha kuwa fedha zilizokusanywa zimetumika kwa ajili ya malipo ya posho ya kujikimu kwa watumishi 69 wa Wizara, posho ya vikao kwa watumishi 243 waliokuwa Dodoma, manunuzi ya chakula, manunuzi ya vifaa vya kuandikia, malipo ya Takrima kwa Waziri na Naibu Waziri na manunuzi ya mafuta kwa ajili ya magari, matumizi ambayo yangeweza kugharimiwa na kasma husika za Wizara bila kuhitaji kuchangisha" imebainisha ripoti hiyo.



SOMA HABARI HII KWA KIREFU ZAIDI

Attachment chini ni Report ya Kamati ya kuchunguza sakata lenyewe:
 

Attachments

  • KAMATI TEULE-yaJairo.pdf
    427.3 KB · Views: 883
Jamaa tayari ameshaanza kusoma taarifa, ameanza na shukurani kama kawaida.
 
Naona mwenyekiti ameanza kusoma,kama kawaida kumshukuru Lt Kanal Kikwete,mke wake,watoto wake na wapiga kura wake
 
ameanza kwa kumshukuru Mungu,kikwete,makinda,wapiga kura,mke wake na watoto,matha,mch.natse.taarifa ina kurasa 150.
 
wakati wa njadala betrice salileta barua iloyotokwa kwa jairo akitaka wizara zilipo chini ya wizara zichangie pesa ya kupitisha bajeti ya nishati na madini
 
Jairo akipona leo basi serikali yetu sitaitofautisha na haja kubwa
 
Jamaa ana speed ya kufa mtu, amedai ripoti ina zaidi ya kurasa 130, bado anarejea michango ya wabunge na nini kilisababisha kamati kuundwa kwamba iliibuliwa na zitto na kuboreshwa na sendeka
 
kabwe zito alitoa maelezo na kuchangiwa na watu wengi ambapo olesendeka aliomba iundwe tume teule ya bunge ya kuchunguza hili sakata.kwa kutumia kanuni ya 117 ya bunge.mia
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom