Uchaguzi 2020 Bungeni: Rais Magufuli amteua Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu, Bunge zima(Wabunge 350) wampigia kura za ndiyo

Sorry bud. Mimi siyo Chadema. Get to know this. Hiyo ilijulikana tulisikia kwenye media kama walivyosikia wengine. Hivi mfano inawezekanaje mgombea akapata kura 179 na mpinzani wake kura 31 halafu anakuja mtu asuyejulikana anabandika matokeo anageuza 31 kuwa 370 na 179 kuwa kura 6?

Huko ndiyo kupangwa. Mimi ni mtanzania mzalendo na mpendwa haki niliyezaliwa miaka ya kuheshimika na Wizi i na ukandamizaji huwa siungi mkono.

Mtu yoyote mzalendo aliyebahatika kuzaliwa miaka hiyo na kushuhudia amani na upendo iliyokuwepo Tanzania ikiwa ya mfano dunia nzima hawezi kufurahia Tanzania ya sasa hata kidogo.
Hata kama wewe sio chadema au wewe ni mpenda haki, ingekua vizuri ujiulize swali hili, inakuaje baadhi ya wapinzani walijua imepangwa CCM itashinda lakini bado wakaendelea kushiriki mchakato wa uchaguzi mwanzo mpaka mwisho??

Naamini kama wewe ni mpenda haki ungejiuliza hivyo.

By the way, sio kila kitu unachosikia kwenye media ni cha kweli, mengine ni propaganda za wapinzani.
Ningekua na ushahidi au ningeshuhudia hicho ulichokisikia kwenye media, basi ningeunga mkono maoni yako.
 
Yaani hakika nimefurahi mno. Majaliwa ni best PM. Ana busara nyingi, mnyenyekevu na mtendaji.

Hongera sana Mh. Rais kwa kumuamini tena Mh. Majaliwa.
Ana busara saaana aisee na uzuri yeye ni kiongozi wa kwanza ambapo waliochukua form za ubunge jimboni kwake kupitia upinzani walitekwa na kupigwa sana, wakanyanganywa na form zao na jamaa akapita bila kupingwa na wala hakuwahi kukemea tabia hio.

Na baada ya tukio hilo ukawa ndio mchezo wa CCM kupiga wapinzani, kuwanyanganya form na kupita bila kupingwa.

Hakika Majaliwa ana busara saaana yaani kama mfalme Selemani vile.
 
Karibu

Spika Ndugai amesoma Katiba kuelezea namna Waziri Mkuu anavyopatikana.

Chanzo: ITV
========

Mpambe wa Rais tayari kawasili kwenye ukumbi wa bunge akisindikizwa na askari wa bunge akiwa amebeba bahasha yenye jina la waziri mkuu ajae.

Baada ya spika Ndugai kuipokea amempa kazi katibu wa bunge kuifungua na spika Ndugai anaweka sahihi kukiri kuipokea na kumrudishia mpambe wa Rais.

Rais John Magufuli kwa mujibu wa katiba amemteua mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zoezi litakalofuata ni wabunge kumpigia kura kumthibitisha kuwa waziri mkuu wa Tanzania.

Wabunge 350 wamepiga kura, hakuna kura ya hapana pia hamna iliyoharibika hivyo wabunge wote 350 sawa na asilimia 100 wamempigia kura za ndiyo na rasmi kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

=====


Je, Kassim Majaliwa ni nani?

Majaliwa Kassim Majaliwa, ambaye anaendelea na wadhifa wa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa muhula wa pili, alizaliwa tarehe 22 Desemba mwaka 1960 yaani miaka 60 iliyopita.

Kitaaluma ni Mwalimu aliyepata elimu yake ya Ualimu katika chuo cha ualimu cha Mtwara mwaka 1991-1993, na baadae kujiendeleza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Stockholm nchini Sweden.

Kutoka mwaka 1984 mpaka 2006 amehudumu katika nafasi mbalimbali kama mwalimu na kiongozi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT). Mwaka 2006 Majaliwa aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya na kisha akajitosa kwenye siasa za ushindani mwaka 2010 alipogombea na kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi.

Baadaye aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa serikali ya awamu ya nne.

Bw Majaliwa ameidhinishwa kuwa Waziri Mkuu na Bunge baada ya jina lake kuwasilishwa bungeni na mpambe wa rais John Magufuli na kupigiwa kura ya ndiyo na wabunge wote 350 waliokuwepo ukumbini. Anatarajiwa kula kiapo hivi karibuni ili kuanza rasmi majukumu yake.

Majaliwa alikuwa Waziri Mkuu katika kipindi chote cha miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Magufuli uliokamilika mwezi uliopita. Endapo atadumu katika wadhifa huo kwa kipindi chote cha pili cha rais Magufuli atakuwa Waziri Mkuu wa pili kuhudumu kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo. Fredrick Sumaye, ndiye mtu pekee mpaka sasa aliyehudumu kwa miaka 10 mfululizo kama Waziri Mkuu wa Tanzania kutoka mwaka 1995 mpaka 2005 chini ya rais mstaafu hayati Benjamin Mkapa.

Majaliwa alikuwa Waziri Mkuu katika kipindi chote cha miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Magufuli uliokamilika mwezi uliopita.

Uteuzi wa Majaliwa hii leo haukusthua wengi kama alivyoteuliwa mara ya kwanza miaka mitano iliyopita. Wachambuzi wengi walitarajia Majaliwa kurejea katika nafasi yake, mosi kutokana na kauli ya rais Magufuli na pili kutokana na utendaji wake. Mwishoni mwa wiki iliyopita, Rais Magufuli alizungumza wakati wa tukio la kuapishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, kwamba viongozi wa serikali hawatakiwi kuwa na hofu ya nafasi zao kwa sababu mafanikio yaliyopatikana katika miaka mitano iliyopita yalitokana na ufanisi wao pia.

Ingawa alisema kutakuwa na mabadiliko makubwa katika baraza jipya la mawaziri, ni vigumu kutenganisha mafanikio ya utawala wa Awamu ya Tano na utendaji wa Waziri Mkuu. Katika mawaziri wote wa serikali ya Rais Magufuli, Majaliwa - kama kiranja wa mawaziri wengine, ndiye pekee ambaye nafasi yake inafungamanishwa moja kwa moja na Rais katika utendaji.

Bw Majaliwa anatokea kusini mwa Tanzania eneo ambalo mtu wa mwisho kutoka ukanda huo kuwa waziri mkuu alikuwa Mzee Rashid Kawawa aliyekuwa Waziri Mkuu miaka ya mwanzoni ya uhuru. Yeye nimtu wa 11 kuwa Waziri Mkuu tangu Tanganyika ilipopata uhuru ambapo Waziri Mkuu wa kwanza alikuwa Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Majukumu ya Waziri Mkuu


Waziri Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania atakuwa na madaraka juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa kila siku wa kazi na shughuli za Serikali, atakuwa na madaraka ya kuongoza shughuli za serikali Bungeni.

Atakuwa na madaraka ya kutekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo rais ataagiza yatekelezwe.

Pia Waziri Mkuu atakuwa na madaraka ya kumshauri rais kuhusu uteuzi wa Mawaziri.

Anayo madaraka ya kumshauri rais kuhusu uteuzi wa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri.

Waziri Mkuu huyu ni mpenzi wa mchezo wa mpira wa miguu, na pia amesomea ualimu wa mpira. Katika kipindi cha mwaka 2010-2015 alikuwa Kocha wa timu ya soka inayoundwa na wabunge.
Hata Mbunge wa CHADEMA naye kamkubali? Kwa hiyo anakubaliana 100% kuwa uchaguzi haukuwa na kasoro? Basi. Mbombo ngafu.
 
Ana busara saaana aisee na uzuri yeye ni kiongozi wa kwanza ambapo waliochukua form za ubunge jimboni kwake kupitia upinzani walitekwa na kupigwa sana,wakanyanganywa na form zao na jamaa akapita bila kupingwa na wala hakuwahi kukemea tabia hio.

Na baada ya tukio hilo ukawa ndio mchezo wa CCM kupiga wapinzani,kuwanyanganya form na kupita bila kupingwa.

Hakika Majaliwa ana busara saaana yaani kama mfalme Selemani vile.
Hiyo roho chafu inatoka kwa jiwe
 
Obvious choice. Kwanza hatuhitaji kubadilishabadilisha mawaziri wakuu kila baada ya miaka mitano maana ni gharama kuwatunza.

Na wote hawana maamuzi thabiti zaidi ya yale yanayotoka kwa mwenye Nchi.
Sasa aliyeleta mada hii...alitegemea kuna mtu asipige makofi...? Usipopiga makofi, ukirudi nyumbani ukakusanye vyako uende kenya, kama unamazingira fulani hivi unakimbilia ubelgiji......
 
Huyu dingi sina shida nae, mwenye kuleta matata ni yule mwenye kichwa kama kabyureta
 
Wote kijani ulitegemea kura ya hapana hapo.
Maana ubunge ni wa CCM na sio wa mbunge akienda kinyume kufurushwa ni lazima
 
Ana busara saaana aisee na uzuri yeye ni kiongozi wa kwanza ambapo waliochukua form za ubunge jimboni kwake kupitia upinzani walitekwa na kupigwa sana, wakanyanganywa na form zao na jamaa akapita bila kupingwa na wala hakuwahi kukemea tabia hio.

Na baada ya tukio hilo ukawa ndio mchezo wa CCM kupiga wapinzani, kuwanyanganya form na kupita bila kupingwa.

Hakika Majaliwa ana busara saaana yaani kama mfalme Selemani vile.
Mkuu nimeshaomba toba nisamehewe. Sikuwa najua kilichotokea huko jimboni kwake. Ninatamani moderator afute Ile post yangu ya kumsifia. So sad
 
Bunge la Ulaya na Jumuia ya madola itatoa hatma ya haya yote...hizi zote ni mbwembwe tu mtoto bado hajatoka tumboni...unaweza kufanya yote utakayo hata kuwaymtangazia majirani si mbaya!!
 
Mkuu nimeshaomba toba nisamehewe. Sikuwa najua kilichotokea huko jimboni kwake. Ninatamani moderator afute Ile post yangu ya kumsifia. So sad
Kwa kuongezea Majaliwa alimvimbishia Rais Mstaafu kuhusu Ubunge wa Nachingwea. Mstaafu alikuwa anataka atangazwe aliyeshinda ambaye ni Dr. Mmoto wa CHADEMA lakini Maja akagoma akasema wamtangaze wa Kijani
 
Back
Top Bottom