Bungeni: Naibu Spika alalamikiwa kumzunguka Spika Ndugai

Ukaribu wa mtu unatuhusu nn sisi wakati bunge linaendeshwa kwa kanuni na taratibu.
 
Ndiyo ubaya wa Rais kuteua mawaziri ndani ya wabunge, ni ukenge tu na wote wanaotetea uamuzi wa bunge kutorushwa live wanawaza kwa kutumia ushabiki wa kichama tu.Wanakera kama nini
 
Wabunge wa ccm wa ajabu sana, ni sawa na binti anayebakwa kila siku na kaka yake lakini hasemi lakini akishapata mimba ndio mambo yote hadharani. Tulia walijua ameletwa pale kwa sababu gani, lakini wakampitisha kwa kishindo. Sasa ngoja ujauzito utokee ndio watabaki na kulalamika kuwa ni wa ndugu yao
 
Wabunge wa CCM ni mzigo kwa Taifa maana hawajui wajibu wao.
Ni aibu kwa Ndugai mwanaume mzima unakuja kulialia kwenye mitandao maana yake nini? Safi sana hako ka mama kama kamempiga bao Ndugai! Huwa ananikera sana anapokuwa na upendeleo wa wazi!! Sasa yeye kama Mkuu wa bunge si atengue hayo maagazo ya hako ka mama?
 
Mie nilikuwa ninashauri hivi, kwa kuwa watu wengi wanatoka kazini saa 10 basi tbc ionyeshe live bunge la jioni kuanzia saa 10 hadi wanapofunga.halafu warushe recorded kuanzia saa tatu usiku kwa ajili ya mijadala iliyofanyika asubuhi. Hili likifanyika watu hawatakuwa na shida sana.nikweli wengi wetu asubuhi tunakua kwenye pilika lakini ile jioni mpaka mapema ya usiku usiozidi saa 4 kamikli jioni/usiku ndo mda mzuri wa kufuatilia.

Kama serikali inania safi basi ichukue huu ushauri kuliko inavyofanyika sasa
Tushasema haiwezekani,gharama ni kubwa,alafu bunge sio press conference , tanzania yangu mhhhh
 
Aisee agwe ndugai usikubali haka kabinti kakakufunika we ni mkongwe tangu kitambo. Halafu mi nilijiuliza ndugai huyu wa escrow tuliemtumainia kawaje kumbe anazungukwa. tumpe moyo huu mhimili upate heshma yake, agwee chibitee tupo pamoja rudisha bunge live
 
Teeeeeeeeh teeeeeeeeh teeeeeeeeeh, naona magamba mmeanza kuumbuana na baaadooooo
e8e40383e73e5ce85c4bd4603995591f.jpg
 
Huyu Naibu Spika ndivyo alivyo, ninyi mlitaka afanyeje wakati Ubunge alipewa kama Zawadi?

Tena hapa Serikali inajificha kwenye nyumba ya kioo
Ni Kweli Kabisa. Ndugai Alitumia Nguvu Ya Ziada Hadi Kumtandika Mtu Bakora Akazimia. Hawezi Kuwa Sawa Na Huyu Wa Kupewa
 
Kwani Bunge si linaendeshwa kwa sheria, taratibu na kanuni? Kama ndivyo basi ukaribu wa mtu na mtu hauwezi kuathiri shughuli za bunge.
Nani amekwambia kuwa nchi hii inaendeshwa kwa sheria mbalimbali na Katiba ya nchi?

Kama ingekuwa hivyo basi hivi leo Jecha angekuwa keshafungwa jela kwa kuufuta uchaguzi huru na wa haki uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana na kuitisha uchaguzi wake batili, machi 20 mwaka huu ambapo mamlaka hayo hakuwa nayo kabisa kisheria.

Hebu jiulize sababu za 'kipuuzi' zilizotolewa na serikali ya CCM kuzuia Bunge kuwa LIVE.

1. Eti ni gharama ya kurusha matangazo hayo LIVE ambayo ni shilingi bilioni 4 kwa mwaka ambapo ilidaiwa TBC haiwezi kumudu.

2. Eti ni kuzuia wananchi wasiangalie matangazo ya Bunge saa za kaz, ambazo wao wanadai ni kutokea saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni.

Tuanze na swala la kwanza, tumuulize Nape ambaye alidai sababu ya kutorushwa matangazo hayo LIVE ni gharama. Kama kweli sababu ndiyo hiyo, mbona hata zilipojitokeza asasi za kiraia zilizosema zitagharimia matangazo hayo ili wananchi wayaone matangazo hayo LIVE, bado serikali imeendelea kusisitiza kuwa matangazo hayo hayataonyeshwa LIVE?!

Pia ni kwa nini hata vituo binafsi vya TV vya Azam na Star TV zilivyokuwa vinaonyesha matangazo hayo LIVE, navyo vimepigwa STOP kutoonyesha matangazo hayo?!

Tuje kwa suala la 2 ambalo ilidaiwa muda wa kutoka saa 2 asubuhi hadi saa 10 jioni ni muda wa kazi kwa hiyo muda huo wananchi hawapaswi kuwa kwenye luninga zao na 'kupoteza' muda badala ya muda huo kuchapa kazi.

Kama kweli sababu hiyo ingekuwa na mashiko, tumuulize swali jepesi Nape, ni kwa nini hajaielekeza TCRA ivipige STOP vituo vyote vya Radio na TV visionyeshe matangazo yoyote majira ya asubuhi hadi jioni ya saa 10 jioni ambapo inadaiwa nini muda wa wananchi kufanya kazi, badala ya utaratibu wa Radio hizo na TV stations ambapo karibu zote zinarusha matangazo yao kwa masaa 24?!

Kutokana na sakata hili la kutoonyeshwa matangazo ya Bunge LIVE, imethibitisha ule msemo unaosema PENYE UKWELI UONGO HUJITENGA.......
 
Back
Top Bottom