Bungeni: Musukuma na Spika Ndugai waiomba Serikali kuruhusu waganga wa jadi kuruhusiwa kutibu Corona, wadai imani za Kimagharibi ndio kikwazo

Hivi kwa nn watu wa mkoa wangu hawakupambana ili tuwe nchi huru kuliko kuwa katika nchi moja na hivi viazi mbatata?

Mkwawa fufuka tupiganie nchi yetu
 
..Going back to the root.....

Msukuma, tupige na ramli kabisa ili tujue ni nani katuletea hili janga...dawa zipo!!
 
Huyu microphone, mbona yeye alienda kutibiwa ki-magharibi na kutumia Bn?? Alishindwa nini kutumia hizo dawa za mitishamba??

Halafu wanashindwa nini kumtibia kienyeji mbunge mwenzao anayeumwa CORONA??

Serikali haijakataza kujitibia, ila wasije watu kuanza kulaumu wametapeliwa..hawakawii!

Everyday is Saturday.................. :cool:
 
Msukuma, ameitaka Serikali kuwapa nafasi Waganga wa jadi katika kutumia dawa zao kutibu watu wanaougua Corona.
Tunapata tabu kuwaelewa waheshimiwa wanaposema "Waganga wa jadi" hao waganga wa jadi wanaokusudiwa ni wepi??


Kwa sababu, tumezoea sana kukutana na vibao hasa kwenye nguzo za umeme au simu na wanaandika mpaka namba zao za simu wazi wazi.... Utakuta pameandikwa..


'Mganga wa jadi kutoka Sumbawanga'

Anasaidia ushinde kesi, ufaulu mitihani, mvuto wa mapenzi, kumtuliza mke, pete ya bahati, na maneno kama hayo !!!

Kiukweli hawa wanahamasisha uovu na ujinga ktk jamii zetu na wanakula ela za wajinga.

Sasa labda nadhani waheshimiwa wanakusudia watabibu kwa dawa za kiasili.

Dawa za kiasili naam ni nzuri na tunaomba wapewe chance ya utafiti, ili tujue je ni miti gani au majani gani kwa kiasi gani yanaweza kusaidia kupambana na corona.
 
Hivi wakuuu mlitegemea waseme wameiomba serikali kuacha kuamini mambo ya kienyeji? Nchi ilishaingiliwa hiii! Tulishaingia cha kike ile nyie hamjaelewa tu, kwa sasa watu Wa aina hiii wakishamuelewa namba moja anapenda nini wao kesho yake wanamtangulia mbele kwa kile kile anachokipenda hahahahahhahaah nchi imeishaingia chooo cha kike hakiamungu.

Yaani kwa sasa hivi watu wanafanya utafiti wakishagundua kuwa namba moja anapenda nini wao kesho yake wanamtangulia mbele hahahaahahahah yani maaaana yake nikuwa namba moja akipendelea nchi iwakubali wachawi wao kesho watapendekeza yanayo fanana na wachawi hahahahaha tumeingiliwa kiukweli, kesho namba moja akionesha kupendelea kuuuwa watu, kesho yake akina burembo watajitokeza kusema zito auwawe huku akipigiwa makofi ya hatariiii na marehemu rwakatare hahahahaha tumepatikana.

Ndio maaana watu wamepata vyeo kwa kutekeleza ayapendayo namba moja ila Yule msaniii wa Tandahimba aliempongeza namba moja kwenye Wimbo wake na hatimae kilichofuata ni kuitwa kwenye hafla za namba moja Kwa maelekezo ya namba moja yeye Yule msaniii akaahidiwa kupewa ubunge sasa nikuwa aliekuwa Mbunge wa Jimbo hilo akaona isiwe taaabu ngoja nae apongeze na kuunga juhudi Halafu sasaeitaeleweka mbele kwa mbele Nani atapewa hiyo nafasi maaana wote wamepongeza hahahahhahahahha tumepatikana, tuliiingia cha kike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alianza mkaidi mwenyewe, kwa hiyo siwashangai vidagaa navyo vikija na mawazo haya sio, katika kipindi hiki sicho..
20200423_213256.jpg
 
Mbunge wa Geita, Joseph Msukuma, ameitaka Serikali kuwapa nafasi Waganga wa jadi katika kutumia dawa zao kutibu watu wanaougua Corona.

Amesema akili za Waafrika wengi zimejazwa imani za Magharibi kiasi cha kudharau tiba za asili zilizotumika enzi na enzi.

Aidha, hoja hiyo iliungwa mkono na Spika Job Ndugai, aliyesema yupo Msomi mmoja ameandika dawa zinazoweza kutibu virusi vya corona lakini kutokana na imani za mila za Magharibi hakijapewa kipaumbele.


Waganga wa ramli hawataweza kutibu Corona. Watatuletea aibu isiyo kifani sababu ya matambiko yao ya kishetani.

Dunia haijasahau mauaji ya albino. Wasije wakaanza kuua watu wenye vipara au mimba au watoto au chochote kile.

Waganga wa kienyeji hawana nafasi ya kutusaidia kwa lolote katika kupata muafaka wa maendeleo ya Taifa letu
Wanatuletea laana za ulozi wao
 
Back
Top Bottom