Bungeni: Musukuma amvaa Luhaga Mpina kwa kueneza uzushi wa Bwawa la Umeme la Nyerere

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Dec 1, 2021
19,589
14,136
Wameanza kuumbuana.

Mbunge wa Geita Mjini Musukuma amemjia juu Luhaga Mpina kwa kumhusisha na kueneza uzushi Kuhusu Bwawa la umeme la Nyerere kwenye Clip aliyodai ilikuwa ikienea mitandaoni. Musukuma ameonya kutohisishwa kwenye uzushi usio na maslahi ya Nchi Kwa kuangushiwa jumba bovu 😆😆.

Musukuma amesifu Kazi nzuri iliyofanywa na Waziri Makamba chini ya uongozi mahiri wa Rais Samia.

My take,

Mtaendelea kuumbuana na mwisho mtawataja tuu waliowatuma.

======

1649423430562.png

Dodoma. Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku ‘Msukuma’ leo Ijumaa Aprili 8, 2022 ameeleza kuwa basi lake lililokamatwa kwa kosa la kuwa na samaki watatu linaozea kituoni lakini anashangaa aliyehusika na yeye analalamika.

Wakati Mpina akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, basi linalomilikiwa na Msukuma lilikamatwa likiwa na samaki na kutaifishwa. Wakati huo Serikali ilizuia uvuvi na usafirishaji wa samaki wadogo Ziwa Victoria.

Msukuma ametoa kauli hiyo wakati akichangia katika hotuba ya makadilio ya mapato na matumizi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara zilizochini yake ambapo amesema kuna watu huwa wanajisahaulisha wakisha kuwa nafasi za juu.

Hata hivyo Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson amekea kauli hiyo akisema siyo sehemu ya mjadala ulio mbele ya bunge na kumtaka mbunge kujielekeza kwenye hoja mahususi huku akimsihi kufuta kauli yake aliyosema message delivery (ujumbe umefika).

Msukuma amemtaja moja kwa moja mbunge wa Kisesa, Luhwaga Mpina kwamba amekuwa mtu wa kulalamika huku akimhusisha yeye (Msukuma).

“Mimi sitaki kuangushiwa jumba bovu, nimeona katika moja ya mitandao nahusishwa na kauli yangu kuhusu ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, nililisema kweli na nikafuata taratibu zote, lakini tuliomba kibali cha kutembelea ambapo nakiri ujenzi wake umekwenda mara tatu ya alivyoacha Magufuli (Rais John Magufuli wa awamu ya tano),” amesema Msukuma.

Katika hatua nyingine ametaja hoja ya kupanda kwa bei ya mafuta Tanzania akitaka Serikali ichukue hatua za dharura kama ilivyofanya katika mazao ya wakulima, lakini ameonya bila kufanya hivyo wakati wowote mafuta yatapanda tena.
 
Wameanza kuumbuana..

Mbunge wa Geita Mjini Musukuma amemjia juu Luhaga Mpina kwa kumhusisha na kueneza uzushi Kuhusu Bwawa la umeme la Nyerere kwenye Crip aliyodai ilikuwa ikienea mitandaoni..

Musukuma ameonya kutohisishwa kwenye uzushi usio na maslahi huku Akiisifu Kazi nzuri iliyofanywa na Waziri Makamba..

My take,

Mtaendelea kuumbuana na mwisho mtawataja tuu waliowatuma.

View attachment 2180464

View attachment 2180465

View attachment 2180466

View attachment 2180467
Mpina anwapiga pini hadi mnalialia tu , report ya CAG inasema kuwa bwawa liko 41% na lilipaswa kuwa 86% mwaka jana. Wewe unaletamavi yako hapa


USSR
 
Mpina anwapiga pini hadi mnalialia tu , report ya CAG inasema kuwa bwawa liko 41% na lilipaswa kuwa 86% mwaka jana. Wewe unaletamavi yako hapa


USSR
Sasa kwani kuna tatizo ripoti ikisema hivyo?

Ndio maana ya serikali kujibu hoja,Sukuma gang mmja keshaelewa sababu za kuchelewa wala hazihusiani na Serikali ya mama bali wapigaji waliokuwa wamewekwa na kiongozi wa malaika wa Sukuma gang.
 
Mpina na Msukuma wote wale wale tu wanafiki tu na wapiga deal

2025 watafutwe wabunge wengine kuchukua nafasi zao
 
Sasa kwani kuna tatizo ripoti ikisema hivyo?

Ndio maana ya serikali kujibu hoja,Sukuma gang mmja keshaelewa sababu za kuchelewa wala hazihusiani na Serikali ya mama bali wapigaji waliokuwa wamewekwa na kiongozi wa malaika wa Sukuma gang.

Kama kuna mtu alimpenda na kumheshimu na kumpa madaraka Basi Hakuna mkubwa zaidi ya Makamu Wake. Shida unachagua katika watoto wa baba mmoja ukidhani unascore a Point. Hakuna Mtendaji wa vitendo kama JPM. Hata unayozungumzia maujenzi wakati Bwana Kikwete Ni yeye ndo alikuwa mtendaji. Mkapa Ni yeye ndo mtendaji na pengine alipenda sana miundo mbinu kuliko chochote kile. Kabla ya kufa mlimwita so Kama una lolote linalokuuma Labda vyeti. Madawa au bangi zako tu. Singizia mengine. Kama kuna mwenye cheo zaidi ya Rais Tz Basi Wewe Ni kichaaaa.
 
Ndio aina ya siasa zake

Msukuma ana confidence akichangia hata mambo ya kitaaluma kuliko wana taaluma wenyewe

Usishangae Msukuma akiwa anachangia mambo ya Geology akawa na confidence kuliko Prof Muhongo

Mimi binafsi navutiwa na siasa za msukuma…anajisimamia

Akihisi Makamba kakosea anamchana…akihisi kaonewa anamtetea

Tatizo la Msukuma hana tofauti na kina Baba levo na Mwijaku. Siasa yake imekaa kimajungu na ku attack wenzie personally.

Kutokana na uropokaji wake, hata akiongea point anaonekana kaongea pumba.
 
Tatizo la Msukuma hana tofauti na kina Baba levo na Mwijaku. Siasa yake imekaa kimajungu na ku attack wenzie personally.

Kutokana na uropokaji wake, hata akiongea point anaonekana kaongea pumba.
Mpina na Msukuma mbona wote huwa Wana Mu attach personally Makamba na huwa hamsemi? Ila leo kamshambulia condom wa sukuma gang ndio mnajifanya kujitokeza mlikojificha 😀😀..

Acha inyeshe SSH ajue panapovuja .
 
Back
Top Bottom