Bungeni: Mjadala wa azimio la kumpongeza Rais Magufuli ununuzi wa korosho wamuondoa Msigwa bungeni

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ameamuru Mbunge wa Iringa mjini Rev. Peter Msigwa kutolewa nje kwa kutokiheshimu kiti. Msigwa alitolewa wakati wa Mjadala wa azimio la kupongeza Rais Magufuli juu ya ununuzi wa korosho.

Dr-YyvRXQAAr-Hg.jpg

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema), ametolewa nje ya ukumbi wa Bunge, wakati Bunge likijadili azimilio lililowasilishwa bungeni na Mbunge wa Singida Magharibi (CCM), Elibariki Kingu, la kumpongeza Rais John Magufulu kwa hatua aliyochukua juu ya kununua zao korosho.

Chanzo cha kutolewa nje Msigwa ilikuwa ni mchango wa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Jackline Ngonyani, ambaye alikuwa akichangia azimio hilo huku akiwaponda wapinzani.

Katika mchango wake alisema wapinzani wamekuwa mabingwa wa kupinga kila kitu kuanzia suala la makinikia na hata Mradi wa Umeme wa Mto Rufiji.

“Wakati wa suala la makinikia wapo tuliokuwa tunawaona wanazunguka hotelini huko kupanga mikakati ya kukwamisha, hoja ya kutengeneza umeme wa Mto Rufiji pia walipinga,” amesema.

Wakati Ngonyani akisema hayo, Msigwa alisimama akawa anazungumza jambo lilofanya Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson, kumtaka akae bila bafanikio.

“Msigwa wewe ni mchungaji, unajua kabisa Biblia inasema tuheshimu mamlaka mimi nazungumza wewe keti,” alisema.

Baada ya kujaribu kumsihi kwa muda bila mafanikio, alimuamuru kutoka nje, na alipokataa aliagiza askari wa bunge kumtoa nje.


Chanzo: Mtanzania
 
Back
Top Bottom