Mbunge wako amechangia hoja mara ngapi Bungeni?

Mtu_Mzima

JF-Expert Member
Oct 1, 2014
1,163
1,125
Ninaliona tatizo kubwa la kimawasiliano kati ya mbunge jimboni na mbunge bungeni.

1. Hebu jiulize, mmbunge wako wmamewahi kufanya mikutano mingapi jimboni kusikiliza kero za wananchi? Na je, aliziwakilisha kunakohusika na kuleta mrejesho?

2. Mbunge wako amechangia hoja mara ngapi bungeni katika mijadala inayoendelea bungeni? Kama alichangia ulizionaje hoja zake. Ndondo au pumba?

3. Mmbunge amewahi uliza swali lolote bungeni linalohusiana na shida za jimboni kwenu au ni mambo ya kufikirika tu?

4. Je, mara ngapi mbunge wako ameshiriki shughuli za maendeleo jimboni kwenu na kuchangia?

5. Hivi unajua mfuko wa jimbo? Umefanya nini unachokijua jimboni kwenu?

Hebu tujadili maana mimi huku kwangu majibu ya maswahi hayo sio mazuri kabisa na jamaa nasikia anajipanga kurudi uchaguzi ujao.
 
Sio kuchangia hoja tu. Anaweza kuwa anachangia pumba kwako kwa faida zake kisiasa.

Mfano mtu asiyetaja shida za maji, umeme, barabara, matibabu, elimu, mazingira safi ya utafutaji riziki, kisha anazungumzia mambo mengine kabisa, ana tofauti gani na aliye sinzia humo?
 
Back
Top Bottom