Bungeni: Mbunge wa CHADEMA amtimua mpangaji wake ambaye ni Askari Polisi, adai haoni maana ya kushirikiana nae, Waziri Lugola amtisha

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,763
4,330
Baada ya kauli ya Mbunge Sophia Mwakagenda (CHADEMA) aliyosema amemuondoa mpangaji ambaye ni Polisi kwenye nyumba yake kwa sababu haoni haja ya kushirikiana nae.

Waziri Kangi Lugola amemuagiza IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mbunge huyo na wengine wanaotoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani.

1573219057145.png


Kamwe Hasira zisitufanye Wanasiasa tukafanya Maamuzi ya Kimhemuko kisha tukazidi Kudharaulika na wenye Akili

Mpaka hivi sasa bado natafuta Mantiki ya Kumfukuza Askari Nyumbani Kwako ambako umempangisha kwa sababu tu za Kisiasa na Hasira. Askari Kufukuzwa kuna Uhusiano gani za matatizo ya Kiuchaguzi au ya Kisiasa? Hivi ukija kuwa Mzee na ukasikia nawe Mwanao ambaye labda amekuwa Askari nae akifanyiwa hivi kama Mama utajisikiaje?

Leo hii unaposema kuwa umemfukuza Askari Kwako kwakuwa huoni umuhimu wake hivi na Wao Askari ambao kwa bahati nzuri Sisi Wananchi tunawahitaji sana kwa Ulinzi na Usalama wa Mali zetu Siku ikitokea nawe ukapatwa na matatizo wakikususia na yakakukuta makubwa utamlaumu nani?

Kama unajinasibu kuwa Wewe ni mpenda Demokrasia na unapambania Haki za Watu unapomfukuza Askari Kwako ulikompangisha uliangalia pia na upande wake wa Pili wa Familia yake ambayo ni kama vile umeinyanyasa? Kwa Kitendo hiki unategemea Kweli upate hata Mwanachama Mmoja ndani ya hiyo Familia ambaye pengine Kura yake hiyo moja na nyinginezo zingeweza Kuitoa CCM Madarakani kama unavyotaka?

Ni kweli Askari wanaweza wakawa na Changamoto zao ila Kumfukuza Nyumbani Kwako halafu unakuja Kujisifia na Kuutangazia Umma wa Watanzania ni Uthibitisho wa aina ya Roho mbaya yenye Ukatili mwingi uliyonayo. CCM haitotolewa Madarakani kwa Kuwachukia Mapolisi bali itatolewa kwa Sera, Mipango na Mikakati thabiti.

Na kilichoniuma na kunisikitisha zaidi ni kwamba haya Maamuzi yamefanywa na Mwanamama ambaye nilikuwa naamini kuwa ndiyo Jinsia ambayo Kiasili imetawaliwa na Huruma kuliko hata Wanaume. Na hakuna Kitu kibaya kama Kutengeneza Bifu na Mapolisi na leo anaweza akafurahi ila natabiri mapema kuna Hatari naiona inaelekea kwa aliyemfukuza Askari Nyumbani Kwake.

Tujifunze Kutenganisha Hasira na Utu.
 
Mambo ya bungeni wanayaleta ya nini huku si walisema watajadili chumbani tusijue
 
#NipasheBUNGENI Baada ya kauli ya Mbunge Sophia Mwakagenda (CHADEMA) aliyosema amemuondoa mpangaji ambaye ni Polisi kwenye nyumba yake kwa sababu haoni haja ya kushirikiana nae.

Waziri Kangi Lugola amemuagiza IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mbunge huyo na wengine wanaotoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani.
 
#NipasheBUNGENI Baada ya kauli ya Mbunge Sophia Mwakagenda (CHADEMA) aliyosema amemuondoa mpangaji ambaye ni Polisi kwenye nyumba yake kwa sababu haoni haja ya kushirikiana nae.

Waziri Kangi Lugola amemuagiza IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mbunge huyo na wengine wanaotoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani.
Waziri huyu naye mpambavu tu, ama kweli kichwa bila akili ni mzigo kwa miguu! Kumwondoa mpangaji ni uvunjifu wa amani?
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom