Bungeni: Mbunge Nicodemus Maganga (Mbogwe) adai Askari Maliasili wanaua Raia

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Mbogwe, Nicodemus Maganga amesema katika Jimbo lake, Askari wa Maliasili wamekuwa na tabia ya kukamata watu na kuua akihoji, "Miongozo inaruhusu kumkamata Mtu na kumuua?"

Hata hivyo kabla ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja kumjibu, Spika Tulia Ackson akasema, "Umesema mambo mazito hapa kwamba watu wanauawa huko. Peleka swali la msingi ili yaletwe majibu mahususi kwasababu hatutaki kusikia habari za watu kuuawa kwenye Hifadhi"
 
Mabadiliko utawala Yana faida zake, Zama za Jiwe mbunge wa CCM hawezi inua pua.
 
Vita ya majangili na askari wa wanyamapori sio ya kuiongelea, askari nao wanauwawa sana wakiotewa
 
tena askari maliasili huwa anafanya ukatili huo huku akilia...
mtu hadi auliwe na askari wa wanyamapori jua kuna jambo sababu usifananishe TAWA na hawa askari bogus wa kulinda raia na malizao!!
siku ukitembelea game reserve ukaona majangiri vitu wanafanyia wanyama utatokwa machozi wee..wanyama wengi wamekuwa viwete..
kumbuka hapa duniani binadamu na wanyama hakuna mwenye haki zaidi ya mwengine!
 
Back
Top Bottom