BUNGENI: Mbunge amlipua Mwenyekiti ya Halmashauri Simiyu kwa kuchelewesha Ujenzi Wa Mahakama ya Mkoa

Tajiri la Bitcoin

JF-Expert Member
Apr 9, 2017
1,087
643

Akizungumza bungeni jana wakati Wa kipindi cha maswali na majibu Mh Gimbi Dotto Massaba ambaye ni mbunge wa Vitimaalum CHADEMA-TANZANIA kutoka mkoa wa Simiyu, ameitaka Serikali kuona haya na kujenga Jengo la mahakama badala ya kutumia ukosefu Wa jengo hilo kama chanzo cha mapato kwa baadhi ya watumishi wa Serikali akiwemo Mwenyekiti Wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi mjini kwani jengo linalotumiwa na mahakama Simiyu kwa sasa ni lake na hivyo kusababisha mgongano mkubwa Wa kimaslahi baina yake na serikali.naomba kumnukuu

" Mh Spika! Machi mwaka 2012 waziri mkuu staafu Mh Pinda aliitangaza Simiyu kuwa Mkoa mpya!
Mpaka sasa naongea hapa ni zaidi ya miaka 6 imepita Mkoa ule hauna Jengo la mahakama ya Mkoa,
Jengo linalotumiwa kwa sasa ni jengo la Mwenyekiti Wa Halmashauri ya Wilaya Bariadi mjini ambae ndie Mwenyekiti Wa Full council na mjumbe Wa vikao vya RCC Mkoa Wa Simiyu ambavyo ndivyo vyombo vya maamuzi ya mkoa kitu ambacho ni kinyume na maadili ya Utumishi kwani huu ni mgongano Wa kimaslahi na kwa mantiki hii Wananchi wanaamini kucheleweshwa kwa ujenzi huu unamaslahi kwa wachache "

" Je nilini serikali itajenga jengo hili ilikuondoa adha kwa wananchi na mkanganyiko huu Wa kimaslahi kati ya Mwenyekiti Wa halmashauri na Serikali.?" aliuliza mapema jana Mh Gimbi Masaba mbunge Wa viti maalumu CHADEMA-Simiyu.

Aidha Mbunge huyo ameitaka serikali kujenga mahakama za Wilaya kwa Wilaya nne za Itilima,Busega, Bariadi mjini na Vijijini namnukuu
" Mh Mwenyekiti! Pamoja na hayo Simiyu pia tunaupungufu mkubwa Wa mahakimu Wa mahakama zote huwezi kuamini mkoani tunahakimu mmoja tu.

Kwa upande Wa Wilaya tunahakimu mmoja tu anayehudumia wilaya NNE za Busega,Itilima ,Bariadi Vijijini na Bariadi mjini ambako hakuna mahakama za Wilaya! "


" Je ni lini mahakama zifuatazo zitajengwa?

√.Mahakama ya Wilaya ya Itilima

√.Mahakama ya Wilaya ya Busega

√. Mahakama ya Wilaya Bariadi Vijijini

√. Mahakama ya Wilaya ya Bariadi mjini.

Ikiwa ni Sambamba na kuajiri mahakimu.

Katibu Wa Mbunge
Dodoma-Tanzania.
 
Back
Top Bottom