Bungeni: Maswali ya 'papo kwa papo' kwa Waziri Mkuu

Pinda ameonesha kwamba hafai kuwa hata mkt wa kijiji na mi naona kuendelea kumuuliza pinda maswali yanayojibiwa na MAKINDA ni kupoteza mda mi naomba kipindi cha maswli ya pinda kifutwe mpaka hapo tutakapo pata mtu mwenye uwezo wa kujibu maswali kama waziri mkuu. Ninaumia sana hasa ninapomuona pinda na makinda wanachezea maisha ya wtz kwa kutoa majibu ya kitoto kwenye mambo makubwa.
 
Hivi mapato ya Serikali ya Zanzibar yanachangia kulipa wabunge wa Jamhuri ya Muungano Tanzania? Isije kuwa wanakuta tuu kutuongezea umaskini huku Tanganyika wakati Zanzibar maisha yana unafuu
Hiyo ndio athari ya Kuukumbatia Muungano usiokuwa na Faida, Zanzibar wachangie nini? na nyie ndio mliouwa Serikali yenu ya Tanganyika na Kujikomba Katika Muungano.
 
Swali kutoka kwa Lissu,takwimu za haki za binadamu zinasema kuwa polisi wa tanzania wanangoza kuua raia bila kuchukuliwa hatua yoyote.kati ya mwaka 2007 mpaka juzi polisi wameua raia 27 katika kanda maalum ya tarime na rorya,je serikali inampango gani wa kuwachukulia hatua za kisheria au nayo inahusika katika mauaji?
 
Anaimaliza CCM kiaina.Kama wananchi wa Tarime wameangalia alichokuwa anakifanya wakati Mh Lissu na Esther Matiko walipomuuliza maswali Mh Waziri Mkuu, CCm na serikali yake watapata taabu sana kuitawala wilaya ile. Kesi zilizoko mahakamani hazina uhusiano na maswali yale.
 
Analipwa ziada kutimiza hayo dhidi ya wapinzani

Ni ukweli usiofichika huyu mama kawekwa pale kwa maslahi ya chama zaidi na MAFISADI kwa sana.
Kama kuna mtu wa kunibishia hili tuwasiliane mojakwamoja thru private E-mail Adss.
 
Swali la Mwisho, wizara ya Fedha kisha ule muuongozo ulioombwa hapo awali utapata baraka za Spika kama alivyoahidi.

Maswali mawili ya Nyongeza kisha tupate muongozo, sina Shaka na Kiu yako TASO itakuwa inajibiwa hapa maana kama alivyohoji Shossi, Lissu atakuwa anamwaga Data na kuthibitisha kuwa hajabahatisha
 
Kabla waziri mkuu hajajibu speaker akaingilia kati nakusema kuwa hilo swala lipo mahakamani na kuna lawama tumepewa kuwa sisi bunge tunaingilia mihimili mingine ya dola, mwisho wa majibu ya speaker.
 
Leo katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, wabunge ambao ni walafi wa Posho walijaribu kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya 73 inayotamka kuwa "Wabunge wote wa aina zote watashika madaraka yao kwa mujibu wa Katiba hii, na watalipwa mshahara, posho na malipo mengine kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge". Mbunge aliyeuliza swali hio ni Habibu Mnyaa wa CUF na alifanya hivyo ili kuhalalisha posho ya sitting Allowance wanazolipwa wabunge kwa ajili ya kukaa na kushiriki vikao vya bunge ambazo ni tofauti na posho ya kujikimu wawapo mkoani Dodoma kuhudhuria viako vya bunge. . Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikubalaina na maelezo mbunge kuhalalishao wizi wa fedha za umma kwa njia ya malipo ya posho kwa kazi amabzo wabunge wanalipwa mishahara na kaendeleza nginjera kuwa fedha huwasaida wabunge kutatua shida mbali mbali za wananchi; na zo na kutoleoa mfano watumishi wa serikali wanaolipwa posho wakati wa matayarisho ya bajeti kuwa ni haki yao kwa kuwa wanafanya kazi masaa ya ziada.

SWALi; Je kama tutaendeleea na utaratibu wa kuwalipa watu posho kwa akazi zile zile wanaopokea mishahara, nini kwanini madakatari nao wasilipwe consultation allowance, waalimu teaching allowance na wakulima farming allowance?

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa tanzania ibara ya 27 (2) inatamka kuwa "Watu wote watatakiwa na sheria kutunza vizuri mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja, kupiga vita aina zote za uharibifu na ubadhilifu, na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambao ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao".

Hivyo Mhe Zitto na wabunge wote wanaopinga wabunge kupitisha sheria za kuhalalisha malipo ya posho kwa wabunge kwa ajili ya shughuli wanaopolipwa mishahara wako sahihi kwa mujibu wa kifungu hiuki cha katiba kinachomhitaji kila mtanzania kupiga vita aaina zote za uharibifu na ubadhilifu na uendeshaji wa uchumi usiokuwa na umakini.

Kwa hali hiyo hoja za Mhe Habibu Mnyya hazikuwa na mshiko yoyote na zilizenge kulinda maslahi ya watu wachache dhidi ya watanzania walio wengi.

Nashauri watu lazima wawe na akili timamu na kuelewa na kufata Sheria za nchi yenu.

Suala la stahikhi za wabunge limebainishwa wazi katika Katiba ya JMT. Sasa ni wajibu wa wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi wote wa TZ na pamoja na mengine katika kazi zao ni Kutunga sheria BASI wanaweza kuiondoa sheria hiyo au kuibadilisha pale wanapoona inafaa.

Nafikiri wabunge wanawajibu kwa hilo kama kweli wana nia na sio danganya toto
 
Balali yupo hai?

Naibu waziri wa Fedha: Balali hamtamwona amekufa na mambo yake yote hamtayaoona

Spika: akiwatokea usiku mtasemaje

Kicheeko

anatambulisha wageni sasa sijui kapotezea muongozo au vipi? tunasubiri
 
Hiyo ndio athari ya Kuukumbatia Muungano usiokuwa na Faida, Zanzibar wachangie nini? na nyie ndio mliouwa Serikali yenu ya Tanganyika na Kujikomba Katika Muungano.

Mgogoro hapa ni ukusanyaji wa mapato kama alivyosema Mbunge wa Mji mkongwe Jumatatu...TRA ni kikwazo kwao wazanzibari wao wanakiona ZRB kama chombo na mhimili sahihi kukusanya kodi za wazanzibar.

Mkanganyiko huu wa ukusnayaji wa mapato bado haujaainsihwa vema kubaini kodi zipi ZRB wakusanye na Zipi TRA kwa ajili ya kuwekwa katika hazina ya muungano ambayo hata akaunti ya fedha hizo bado haijafunguliwa. Safari bado ipo
 
Hivi mapato ya Serikali ya Zanzibar yanachangia kulipa wabunge wa Jamhuri ya Muungano Tanzania? Isije kuwa wanakuta tuu kutuongezea umaskini huku Tanganyika wakati Zanzibar maisha yana unafuu

Kwa mara ya kwanza kabisa ndani ya forum hii kuona Mtanganyika anakubali na kuiita nchi yake Tanganyika. HONGERA SANA NA KEEP IT UP.

Jibu lako kama imewauma basi the door is open. Vunja muungano.
 
Swali la Mwisho, wizara ya Fedha kisha ule muuongozo ulioombwa hapo awali utapata baraka za Spika kama alivyoahidi.Maswali mawili ya Nyongeza kisha tupate muongozo, sina Shaka na Kiu yako TASO itakuwa inajibiwa hapa maana kama alivyohoji Shossi, Lissu atakuwa anamwaga Data na kuthibitisha kuwa hajabahatisha
muongozo wa lisu juu ya mauaji ya nyamongo kwa mauaji ya watu wa nyamongo
 
Muongozo sasa wa Lisu

Anaomba kupewa muongozo kuhusu yeye na Mh. Esther Matiko kuhusu kuuliza kuhusiana na Mauaji yanayofanyika katika mgodi wa Nyamongo

kwa kanuni ya 64 fasiri ya 1 C mbunge hatazungumzia suala lolote linalohusu kesi iliyoko mahakamani

Kwa mauaji haya mh. spika hakuna kesi yoyote iliyofunguliwa kuhusu mauji haya...Ni kweli sisi tumeshitakiwa kwa kosa la kuingilia shughuli za polisi nyamongo

Lakini toka mwaka 1972 hapajafunguliwa kesi yoyote kuhusu polisi kufunguliwa mashitaka, pengine kama sina taarifa sahihi

Tuaomba kufafanuliwa kuhusu kesi hizi kama zipo na kama hazipo tunaomba kupewa ufafanuzi kuhusu madai yetu

Muongozo
 
Back
Top Bottom