Bungeni: Maswali ya 'papo kwa papo' kwa Waziri Mkuu

Ndio maana speaker huwa anamkingia kifua MP asijibu baadhi ya maswali. Anajua alivyo mtupu na ananavyotia aibu.
 
Huna kifungu? Taja. Haliruhusiwi kwa mujibu wa nani, sheria gani, nani kasema?

Usitoe authoritative statements kama huna hakika. Na usiseme unasubiri ufafanuzi wa Spika, Spika sio authority wa sheria za Tanzania, hata Pius Msekwa ashasema huyu Makinda tatizo hakwenda law school!

Bunge linakatazwa kujadili swala lililoko mahakamani?

Kwa hiyo nikitaka Bunge lisijadili Budget nikimbilie mahakamani nikafungue kikesi about some tax law iliyomo kwenye budget proposal halafu nita foreclose parliamentary debate on the budget!
You wish.

Kabla waziri mkuu hajajibu speaker akaingilia kati nakusema kuwa hilo swala lipo mahakamani na kuna lawama tumepewa kuwa sisi bunge tunaingilia mihimili mingine ya dola, mwisho wa majibu ya speaker.

Walipo lizungumzia swala la mauji ya arusha hicho kifungu hakikuwepo au walikuwa hawakijui au mambo yamekuwa magumu hasa baada ya kugundua wanachemka waache unafiki....

Tusipoangalia CCM itatutawala kimabavu sasa, maana ukweli ni kuwa hakuna kesi yoyote kama hiyo mahakamani ila kwa upeo mdogo na kutokuangalia mbali kwa hawa viongozi wa CCM wanafanya mambo kama watoto! CCM imebaki na watu wachache sana wanaojuwa nini kinatakiwa kufanywa, hawa wakina makinda wamejichokea kuliko hata maiti.
 
chozi la pinda kwa mauaji ya albino lilikuwa si la kweli bali alibanwa kwa hoja kwasababu wapo watu wanaoishi maisha magumu mpaka wanapoteza uhai halafu yeye anatetea posho
 
hawa jamaa hawataki kukubali kwamba wanatuibia,yaani kazi tuliyowachagua watuwakilishe ni ya kukaa pale mjengoni,na ambayo tunawalipa mshahara na posho nyingine za kutosha,bado pia wanapata posho za kujikimu wakiwa mjengoni,sasa hizi sitting allowances za nini??????wizi mtupuuuuu
 
Mh. Pinada kwa hili umesononesha taifa!
Waziri mkuu wakati akijibu swali la mheshimiwa fulani, alisema kuwa posho wanazogawiwa bungeni ni kwa ajili ya kugawa fedha hizo kwa wapiga kura wao.

(source Majira 17/06/2011).


Hawajui kuwa huko si kusaidia jamii, lakini yeye anaonesha kuwa hiyo ndo kazi ya posho wanazopokea!. Je hii kitu gaini, si rushwa iliyotanuka?

Kazi ya serikali ni kutumia ‘budgetary instruments' katika kujenga mfumo wa uchumi na kuinua hali na kipato cha watu (distribution of wealth). WABUNGE NA MAWAZIRI KUGAWA FEDHA ZA POSHO KWA WAPIGA KURA (OMBA OMBA). SASA HII NDO STAILI YA KUINUA UCHUMI WA NCHI, MSAADA WA UFAHAMU P/SE.
 
kweli tunaishi kimjini mjini! ni wangapi wanafaidika na hiyo posho? Pinda must resign
 
Jibu kama hilo lingetoka kwa Mbunge kama Kapt Komba na wengine wa aina yake singeshangaa lakini kutoka kwa PM? loh, ni maajabu na inasikitisha
 
aibu tupu. waziri wangu.
Amedhalilisha kazi ya wabunge, hasa wale waliokuwa wanapigania posho hizo
Kimsingi kazi za mbunge ambazo mie ningezipenda ni pamoja na kuloby kupata resources na kuzitumia kwa priorities zilizopewa kipaumbele na jimbo lake.
sio priority za familia au mtu binafsi.

masikini we,
tutaona mengi mwaka huu!!
 
Sikujua kama POSHO si za anayepewa - yeye ni conduit ya kuwafikishia wapiga kura wake...ngoja nimwahi mbunge wangu ili anikatia na mimihuo mgao wetu
 
mi ngoja nimpigie wangu anitumie kwa M-Pesa mana nina namba yake ya simu. Na ole wake anizengue nampeleka kwa pinda
 
Kwa kweli nimeishiwa nguvu na majibu ya Pinda. Amejibu tu bora jibu na ametuthibitishia watanzania kuwa nchi hii ina wenyewe. Ni majibu ya kukatisha tamaa watumishi wengi na anameshangaza sana. Nasema hivyo kwa sababu hakuna mfanyakazi Tanzania hii asiyeshikwa shati na ndugu au jirani, mtu wa kabila moja na hata matapeli wakimweleza kuwa nimefiwa, ninaumwa, nataka kurudi kwetu na sina nauli nk. Kama hili linahalalisha kupewa posho basi wafanyakazi wote wanastahili kupewa posho.

La kushangaza zaidi ni kuwa wabunge na viongozi wengine wanaopata mara nyingi posho za vikao ndo wanaopata posho za nyumba, usafiri, ulinzi mpaka wafanyakazi wa nyumbani na wanalipwa mishahara mikubwa.

Pia anadai wakati wa bajeti hawa watu hukesha. Tumkumbushe kuwa kuna walimu ambao kukesha imekuwa ni kazi yao. Kuna baadhi ya shule za sekondari zina mikondo kumi na mbili na zina mwalimu mmoja wa hesabu. Mchana huyu mwalimu anashinda akipiga kelele na usiku anakesha akiandaa vipindi, kusahihisha test na mitihani na bado anatakiwa asimamie utoro, usafi na nidhamu ya wanafunzi. Walimu kama hawa hata wakae vikao vya masuala ya shule huwa hawapewi hata thumni.

Naomba Mh. Pinda aeleze kuwa walimu wanapoenda kusahihisha mitihani wanakaa kuanzia asubuhi mpaka usiku wa manane kwa zaidi ya mwezi huwa wanalipwa kiasi gani kama per diem na kisi gani kama sitting allowance! Je, wanastahili?
 
Mizengwe Pinda HAFAI KABISA kuwa PM, ametoa jibu la aibu kabisa sijapata kuona. Kazi ya sitting allowance siyo kuzigawa, kama pressure ya kuombwa pesa, kila mtu anaombwa hata asiyefanya kazi, ndugu, jamaa na marafiki anaweza kukupiga mzinga kwa kujua tu kuwa una kipato. Iweje watanzania wengine mishahara na allowance zao zinakatwa kodi lakini siyo wabunge?

Mizengwe anahalalisha madaraja pasipo sababu za msingi, madaraja hayo ndiyo yatakayo itoa CCM madarakani. Mizengwe amelewa madaraka, hayuko pamoja nasi, ameungana na mafisadi kutumaliza watanzania wa kawaida. Siku inakuja hatabaki salama, mafisadi watamkimbia atabaki peke yake akilia na kusaga meno!
 
Jana nilichoka kabisa. Yaani Waziri Mkuu anasema posho ya sitting allowance anayopokea Mbunge huishia kuwapa omba omba wanaowabana wakitoka nje ya ukumbi wa bunge!!!! alafu baadhi ya wabunge wanapiga makofi kumpongeza. Kwahiyo serikali na Bunge zinapromote ajira ya omba omba!!? eti nyingine mbunge akifika jimboni anaombwa hela na wapiga kura wake.

Nadhani alisahau kusema Wabunge wanatoa SADAKA kubwa misikitini na makanisani!!!! Hivi watu wote tunaombwa hela na walemavu na hata watu wenye viungo vyote kamili huko mitaani, kwenye mabaaa, madukani, nk na tunawapatia watu hao tunapewa posho za kufanya hivyo??!! Kwanini Wabunge tu ndo wawezeshwe kufanya tendo hili la kiungwana/kibinadam??!!! Ni kweli huwa wanawasaidia hao wanaowaomba??!!


Kwa kweli nimeumia sana na majibu ya hivyo yanaonesha ni jinsi gani itatuchukua miaka mingi ili tuendeleee. Na kwakweli nimemdelete kabisa Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda kwenye kundi la watu ambao wana mawazo mapana ya kutuwezesha tutoke sehem moja kwenda nyingine katika kutafuta maendeleo endelevu ya nchi hiii. Kwanzia leo namuaona ni mtu wa kawaida sana sana anaechukulia mambo kiurahisirahisi na asiyejali na kufikiria namna ya kumaliza matatizo yanayoisibu nchi hiii.

Niliwai kushiriki debate enzi zangu za nikiwa shule iliyokuwa ina challenge izi compasion centres and NGOs. Tuliconclude kumpa mtu elfu moja au kumi sio suluhisho la kudumu la kumtoa mtu huyo kwenye matatizo. Ni bora ukajua tatizo la mtu huyo na kupanga namna ya kushirikiana nae ili kumfanya uyo mtu aweze kutengeneza elfu moja au kumi ya kwake mwenyewe.

Kumpa ni kumfanya awe mtumwa wako kwamba aendelee kukupigia magoti kila siku kama vile wewe ndo MUNGU wake unayempa kudra ya kila siku. si kuna usemi unaomaanisha badala ya kumpa maskini samaki wa kula siku moja mfundishe na muwezeshe aweze kuvua samaki yeye mwenyewe??!! Provided the fishes are there in a lake/river/ocean!! Hata huu msemo Mh. Pinda haufaham?

Kila wakati ninapomsaidia mtu kwa kumpa mia tano au elfu moja au hata mia moja huwa nampa kama ambavyo ningempa mtoto anunue ice cream au pipi ale afurai sio kwamba ndo chakula chake cha siku.

Kazi tunayo wandugu.
 
Back
Top Bottom