Bungeni: Maswali ya 'papo kwa papo' kwa Waziri Mkuu

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Leo ni Alhamisi dk 30 zijazo tutamshuhudia waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda akijibu maswali ya Papo kwa papo kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sina shaka maswali ya leo yatakuwa na msisimko wa aina yake na huenda majibu pia yakawa ya funika kombe mweanaharamu apite.

Masuala mengi yanalitikisa Taifa sasa:

Posho za Wabunge
Tume ya Maadili ya Viongozi
Baadhi ya Wabinge CCM kuonekana kuikubali hoja ya Upinzani
Mkanganyiko wa Bajeti na mengine mengi

Tupo katika Luninga tunasubiri
 
Leo ni Alhamisi dk 30 zijazo tutamshuhudia waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda akijibu maswali ya Papo kwa papo kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sina shaka maswali ya leo yatakuwa na msisimko wa aina yake na huenda majibu pia yakawa ya funika kombe mweanaharamu apite.

Masuala mengi yanalitikisa Taifa sasa:

Posho za Wabunge
Tume ya Maadili ya Viongozi
Baadhi ya Wabinge CCM kuonekana kuikubali hoja ya Upinzani
Mkanganyiko wa Bajeti na mengine mengi

Tupo katika Luninga tunasubiri

Wabunge kushutumiwa kudai RUSHWA katika Halmashauri kadhaa.Ni hatua gani zinachukuliwa.
 
Katibu...Maswali kwa Waziri Mkuu wapo watu tisa kila chama watu watatu watatu na Spika anasema hana lengo kuchakachua leo...Maswali kwa Ufupi why. Mbowe hayupo leo...anaanza mnyaa
 
Mnyaa: ananukuu katika Ibara ya 73: kazi za wabunge ...wabunge watalipwa mshahara na posho..Ibara ya 23 kila mtu anawajibu wa kufuata na kutii katika..anahaoji tabia iliyoingia sasa, na kuleta fitna kwa wabunge na wanachi wao..waziri mkuu anasemaje?
 
Nakupa bigup GR Tupatie update live za mwaswali na majibu bungeni maana sisi wengine tumefichwa vibandani hatuoni TV yoyote huku tunacheza na vi IPOD tu mwanawane.
 
Waziri Mkuu: Stahili za wabunge zipo kwa mujibu wa katiba kwa manufaa ya watanzania

Posho zipo makundi mawili..

1. Zile ambazo katibu mkuu hawezi kuzirekebisha
2. Zile ambazo katibu mkuu anaweza kuzirekebisha

Hivyo zile ambazo zinatokana na katiba ambazo katibu Mkuu hawezi kuzirekebisha lazima zifuate utaratibu wa katiba kuzirekebisha

Mfano diwani halipwi mshahara analipwa posho, pia askari anapewa ration allowance ambayo napewa kwa ajili kutekeleza majukumu yake

haya kwa wabunge sasa
 
Kwa hiyo watui ambao wanafanya kazi kwa muda mrefu na hawawezi kupewa overtime Bunge linawapa Posho kwa nia njema kabisa ambayo imeridhiwa katika katiba na wabunge ni sehemu ya ongezeko hilo

''Unajua kuna maneni mengi na kana kwamba ni jambo kubwa, hiki ambacho manapigia kelele kuhusu wanachopewa wabunge wanakitumia hata hawajavuka mlango wa Bunge unatoka tu hapo mlangoni unagongana na mpiga kura anataka msaada''

Kawa hiyo zimekuwa za manufaa sana kwa wabunge

Hii ni jambo ambalo linawasaidia sana wabunge

''Kuzikataa si kama utaonekana mzalendo sana lets be hinest with ourselves, nimekuwa mbunge kwa muda mrefu nayajua haya na hakika watanzania watatutuelewa''

Swali la nyongeza

Nini hatua ya serikalai kwa wanaojaribu kuvunja na kuvuruga hatua hii

Waziri Mkuu: hakuna sababu, Kabwe si wa kwanza kwa hiyo Mnyaa usinizulie tatizom ingine kwa utani kidogo

Mi najua CDM wengi wnamezea mate posho lakini wafanye niii

Duuuuuuu
 
Waziri Mkuu: Stahili za wabunge zipo kwa mujibu wa katiba
kwa manufaa ya watanzania : Posho zipo makundi mawili..1. Zile ambazo katibu mkuu hawezi kuzirekebisha 2. Zile ambazo katibu mkuu anaweza kuzirekebisha

Hivyo zile ambazo zinatokana na katiba ambazo katibu Mkuu hawezi kuzirekebisha lazima zifuate utaratibu wa katiba kuzirekebisha

mfano diwani halipwi mshahara analipwa posho
pia askari anapewa ration allowance ambayo napewa kwa ajili kutekeleza majukumu yake

haya kwa wabunge sasa

Umekuwa mbunifu mpaka umenikuna sehemu.
Endelea Mkuu kutupakulia ...ehe ...anasemaje kuhusu sitting allowancess
 
Swali la Pili

Kwamba wakimbizi kutoka Rwanda na Burundi watahamishiwa Lindi na Mtwara kama ni kweli kwa nini hasa wakati tayari wana uraia na wanaweza kushi mahala popote Nchini?

Pili tunajua athari za wakimbizi kama uharibifu wa Mazingira na uhalifu wa kutumia silaha kwa nini wapelekwe lindi na Mtwara

PM
 
PM : Nimekuwa nikilisikia pia hilo....HOW????????
Zipo jitihada za kuwarudisha wale ambao wangependa kurudi na pia kuwapa hifadhi watakaopenda kendelea kuishi Nchini na wamepatikana Laki moja na sitini

Nia ni kuwafanya waweze kuintegrate katika maisha ya kawaida kama raia wengine na watasambazwa Nchi nzima kasoro mikoa iliyobeba mzigo huo kwa kipindi chote (Kigoma na Mtwara)

Zoezi halijaanza ila kuna maoni kuwa tulitazame upya licha ya kuwepo fikara tofauti kutoka jumuiya ya kimataifa kwa hiyo bado lianfanyiwa kazi
 
Katibu...Maswali kwa Waziri Mkuu wapo watu tisa kila chama watu watatu watatu na Spika anasema hana lengo kuchakachua leo...Maswali kwa Ufupi why. Mbowe hayupo leo...anaanza mnyaa

CCM = 3
CDM = 3
CUF = 3

Vyama vingine spika havitambui? au NCCR + UDP + TLP =CCM+
 
Cuf hawajapenda suala la Posho kususiwa na Cdm +Nccr

Hivi mapato ya Serikali ya Zanzibar yanachangia kulipa wabunge wa Jamhuri ya Muungano Tanzania? Isije kuwa wanakuta tuu kutuongezea umaskini huku Tanganyika wakati Zanzibar maisha yana unafuu
 
Back
Top Bottom