Bungeni: Luhaga Mpina amtoa jasho Waziri wa Nishati kutokana na tatizo la kukatika umeme

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,703
15,151
Mbunge wa Kisesa mh Luhaga Mpina leo wamewavaa vikali bungeni waziri wa nishati pamoja na naibu wake kutokana na tatizo la kukatika umeme na kuchelewa kujazwa maji kwa bwawa la kufua umeme la mwl Nyerere.

Mpina amehoji ni kwa nini waziri wa nishati January Makamba kwenye kamati alitoa sababu tofauti na hizi anazotoa bungeni za kuchelewa ujenzi wa bwawa? Amefafanua kwenye kamati alisema limechelewa sababu ya mkandarasi kuchimba handaki moja badala ya sita na bungeni alisimama na kusema bwawa limechelewa sababu crane ya kubeba tani 26 haipo na haijafika nchini.!

 
Makamba hamna kitu, anabebwa tu na hilo jina la baba yake ambaye nae sioni mchango wake wa maana kwa hili taifa zaidi ya ule mdomo wake. Magufuli alimtumbua for a reason, hamna anachojua zaidi ya kusafiri na kuongea na wazungu wakisaini mikataba yao ya kinyonyaji.
 
Kwa hiyo wewe unatakeje?
Huyo Mpina akiwa waziri hakuwahi kuulizwa maswali na hao wenzake?
Ninachojua Tanzania mwazili na watendaji wa serikali wengi ni waongo waongo tu.
Wanasagiana kunguni,yeye mpina alipokuwa wizara ya mifugo kafanya nini cha maana zaid ya kuua taasisi za tafuti za mifugo
 
Watu walizoea majibu ya kiujanjajanja ya Kalemani, full propaganda
 
Back
Top Bottom