Bungeni Live: Waziri Mkuu ajibu maswali ya papo kwa papo!

Nashangaa sana kuona asubuhi hiiTBC hawaoneshi Bunge leo, maana nashindwa kabisa kuelewa TBC kama Luninga ya taifa ni kitu gani muhimu wanachopaswa kuonesha kama si bunge jamani? na hii sio mara moja, majadiliano ya katiba hawayaoneshi, si Kongamano la UDASA wala Public Hearing ya Mswada!

Nini kazi ya Television ya taifa jamani au kuna hitilafu? Tuambiane!

Ata radio ya taifa sisikii chochote. Mi nikajua leo hakuna bunge.
Mwisho wao umefika
 
wanaogopa kukutwa na yaliyomkuta Mzalendo na MWANAMAPINDUZI wa habari TIDO MUHANDO aliyefufua TBC kutoka kuzimu na kuirudisha duniani kisha wakamdhalilisha na kumuachisha kazi kisiasa.kisa "MCHAKATO MAJIMBONI" wanalinda ugali wao wakatolewa pale kesho unaweeza ukakutana nao wakitembeza kashata vijiweni
 
aysee nimetegeshea radio yangu hapa kazini hadi nimerekebisha saa kumbe hawako hewani!duuh......................tunarudi enzi za TANU sasa!

CJUI TZ 2NAKWENDA WAPI?................

wao CCM WALIJIANDAA TANGU JANA,SPIKA ALITANGAZIA WABUNGE LEO TBC TV&RADIO.HAITATANGAZA LIVE.(KUVUA GAMBA)
 
Pasco, thanks for always keeping us posted kwenye masuala ya Bunge... kwakuwa wengi tuko makazini (au nje ya nchi), na kuweza access bunge ni ngumu... tunaomba kama utakubali, uwe unatupa dondoo za yanayojiri

Nafahamu kwamba unaweza na nita-appreciate sana msaada huu kwa faida ya wanaoipenda Tanzania including mimi na wewe
:help:

Thanks, kama Pasco atapata dharura na pengine Infisibo awe anatupatia dondoo kama atakuwa na access na kinachoendelea bungeni live
 
Spika AMEMSAIDIA WAZIRI MKUU KUKWEPA SWALI KHS MUSWADA (ULIOSHINDWA) WA KATIBA,KWA KUJIBU KUWA MAPENDEKEZO NA MAONI YA WANANCHI YAMEWASILISHWA KWA SPIKA NA YANAFANYIWA KAZI.
*SPK AMEMNYIMA NAFASI MH LEMA KUMUULIZA PINDA KHS MGOGORO WA MEYA ARUSHA NA HATIMA YAKE *PIA AMEMNYIMA ZITTO HAKI YA KUMUULIZA W/MKUU SWALI LA NYONGEZA.
 
Spika AMEMSAIDIA WAZIRI MKUU KUKWEPA SWALI KHS MUSWADA (ULIOSHINDWA) WA KATIBA,KWA KUJIBU KUWA MAPENDEKEZO NA MAONI YA WANANCHI YAMEWASILISHWA KWA SPIKA NA YANAFANYIWA KAZI.
*SPK AMEMNYIMA NAFASI MH LEMA KUMUULIZA PINDA KHS MGOGORO WA MEYA ARUSHA NA HATIMA YAKE *PIA AMEMNYIMA ZITTO HAKI YA KUMUULIZA W/MKUU SWALI LA NYONGEZA.
 
Kinachoonekana Serikali inakimbia kivuli chake mwenyewe.


TANGU JANA WAMECHAKACHUA, MHE TUNDU LISSU ALIKUWA ANAWASILISHA MABADILIKO YAKE MAZURI SANA KWENYE MUSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA MBALIMBALI, Nadhani walijua angewafunika, jamaa alikuwa alikuwa na michango ta msingi sana lakini kwa sababu tu itaonekana mpinzani ndiye aliyeleta hayo mabadiliko waliyapiga yote chini. SASA WANAFANYA MAKUSUDI TBC isirushe matangazo ya Bunge maana wanaogopa kuumbuka
 
mbowe kamuuliza waziri mkuuu kwa kuwa mswaada umepigiwa kelele na wananchi na wasomi na wanazuoni na wana harakati pia kwamba ufanyiwe marekebisho je yeye kama kiongozi wa serikali bungeni anawaeleza nini watanzania juu ya kuondoa huo mswaada ukafanyie marekebisho ndipo waziri mkuu akajibu kuwa kamati imesha kaa na kulizungumza hilo na ripoti itapelekwa kwa spika ili naye aweze kumshauri waziri mkuu kwamba wafanye nini na katika majibu hayo ndipo mbowe alipo pewa nafasi ya kuuliza tena swali na ndipo alipo muuliza waziri mkuu kwa nini asiwatangazie moja kwa moja wananchi kuwa huo mswaada unarudi kufanyiwa marekebisho na ndipo waziri alipojibu na kusema tufuate kanunu na taratibu na ripoti itatolewa
 
kwa kweli bungeni kulikuwa mtata leo hasa wabunge wa chadema walipo nimwa haki zao wazi wazi na spika na wakachachama na kuomba muongozo wa spika ni mengi ningependa kuyaletta hapa ila muda unaniacha kidogo nikirudi nitawapa mambo yalivyo jili bungeni leo lakini pia nataka kusema makinda kwa tabia yake ya kukibeba chama tawala waziwazi iko siku itafika mwisho
 
TBC Wasiogope wajaribu kuthubutu kama alivyo thubutu TIDO MHANDO ama kwa hakika wananchi walio wengi wamepoteza imani kwa TBC ni chombo kimebaki cha wasanii fulani.
 
Hiki chombo sasa kimekuwa ni chombo cha kipuuzi sana na hakuna la maana kinachofanya kuuhabarisha umma kuhusu masuala ya bunge. *****fu zao:disapointed:
 
Katika maswali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu Pinda leo asubuhi spika wa bunge Anna Makinda aliamua kuruka jina la Mh G Lema ambaye alitakiwa kumuuliza waziri mkuu ila kwa mshangao wa wengi G Lema hakupewa fuksa hiyo na ikabidi aombe mwongozo lakini kama kawaida Spika Anna Makinda akamchinjia baharini.

My take:
CCM INAKIMBIA KIVULI CHAKE MWENYEWE

Nawasilisha
 
Katika maswali ya papo kwa papo kwa Waziri mkuu Pinda leo asubuhi spika wa bunge Anna Makinda aliamua kuruka jina la Mh G Lema ambaye alitakiwa kumuuliza waziri mkuu ila kwa mshangao wa wengi G Lema hakupewa fuksa hiyo na ikabidi aombe mwongozo lakini kama kawaida Spika Anna Makinda akamchinjia baharini.

My take:
CCM INAKIMBIA KIVULI CHAKE MWENYEWE

Nawasilisha


Huyu Spika sijui kama atamaliza miaka mitano...that Bunge is too much for him....we will really Miss mzee sita ..
Lakini waliosimama kuanguka kwake nao wameangushwa ndani ya chama so Spika inabidi asome alama za nyakati...
 
Ipo siku huyu mama atagundua kuwa anatwanga maji kwenye kinu, nguvu ya umma ni kubwa sana na inaelewa nini kinafanyika! Godbless Lema ni mtu hatari hataiacha ipite hivi hivi au taarifa za kiintelenjisia vilisha baini angetoa chozi nini tena?
 
nimeangalia leo ajamtendea haki hata kidogo lakini watanzania wanajua kinachoendelea bungenia akili zao ni timamu na wanajua wancho fanya na maamzi siku wakiamua kuyachukua mtastaajabu sana
 
Ilikuwa ni MPANGO MAALUM LEO WA KUKWEPESHA MASWALI MUHIMU TOKA CDM.
*GL ALIKUWA AMEPANGA KUMUULIZA W/MKUU HATMA YA SAKATA LA MEYA WA ARUSHA NA MSIMAMO WA SERIKALI.
*NA TBC ILIACHA MAKUSUDI LEO KURUSHA LIVE ILI ISIJE KUONEKANA LIVE KAMA INGESHINDIKANA PLAN "A"
 
Back
Top Bottom