KALYOVATIPI
JF-Expert Member
- Aug 11, 2011
- 1,414
- 197
Ni bora nisiwe mbunge au niwe mbunge sio kwa maspika kama hawa watanipiga ban kila kikao
Mbona unatokwa na mapovu kwa umtetea mwanaume mwenzako ? kulikoni ?
Baada ya kushuhudia malumbano hayo, sasa nimeamini, poasi na shaka kabisa kuwa serikali yetu ni mwoga mkubwa wa hoja.
Hivi kuna ubaya gani kulijadili suala hili? tena, katika mjadala serikali ingepata mawazo mazuri kutoka kwa wabunge jinsi ya kushughulikia masuala haya
Ni bora nisiwe mbunge au niwe mbunge sio kwa maspika kama hawa watanipiga ban kila kikao
Lisu anajua sheria na ana hoja mara ishirini zaidi ya Werema.atake asitake hata wakiingia darasani Lisu atamuacha mbali sana Werema.
Ulitaka Zero wa Ikulu achague mwanasheria mkuu wa serikali makini ili aikaange serikali?Kwa kifupi hatuna mwanasheria mkuu wa serikali yaani ni zero kabisa.
Mkuu PrN-kazi asante sana kwa taarifa hii japo imenitia kichefuchefu.katika kutengeneza mazingira kukwepesha ombi la Lissu juu ya kutoa hoja ili kujadili ajali ya mali iliyotokea juzi, AG- Werema ametumia kauli tata na ya matusi ikiashiria kwamba Lissu japo ana nywele lakini huwezo wa kufikili hana. jambo ambalo limezua mjadala hasa baada ya Lissu kuomba utaratibu na kumtaka Naibu Spika amwamulu AG-Werema afute maneno yake na Naibu Spika kakataa kukubaliana na Lissu; kuona hivyo Lissu kahamua kutoka nje kitendo hicho kimeitikiwa na baadhi ya Wabunge.
Nilikuwa naangalia bunge wakati mwanasheria mkuu anamtetea spika juu ya uamuzi wake wa kukataa ombi la Tundu lissu kutoa hoja ya kuahirisha bunge ili kujadili ishu ya ajali ya meli. Kwa kweli kwa uelewa wangu mdogo sana wa mambo ya bunge na sheria pia ( mimi si mwana sheria wala mbunge) huyu AG wa serikali yetu sijui aliwezaje kuwa jaji na kuteuliwa pia kuwa AG. Anavyojibu alivyokuwa anaongea ni wazi kabisa inaonesha hajui kanuni na pia anachokiongea na kuishia na kutoa lugha ya kuudhi wabunge wengine hasa mtoa hoja. AG ni mtu mkubwa sana sikutegemea anaweza kuwa hivyo.
Kabisa! huwezi kumlinganisha Lissu na Werema. Sujuwi nani alimteua Werema, jamaa lina uwezo mdogo sana ndio maana alishindwa hata mtihani wa uwakili!