Bungeni Live: Naibu spika akataa hoja ya Lissu kuzungumzia kuzama kwa meli

Weka hapa Update!

katika kutengeneza mazingira kukwepesha ombi la Lissu juu ya kutoa hoja ili kujadili ajali ya meli iliyotokea juzi, AG- Werema ametumia kauli tata na ya matusi ikiashiria kwamba Lissu japo ana nywele lakini huwezo wa kufikili hana. jambo ambalo limezua mjadala hasa baada ya Lissu kuomba utaratibu na kumtaka Naibu Spika amwamulu AG-Werema afute maneno yake na Naibu Spika kakataa kukubaliana na Lissu; kuona hivyo Lissu kahamua kutoka nje kitendo hicho kimeitikiwa na baadhi ya Wabunge.
 
Sijawahi kuona mkurya wa ajabu kama huyu Werema.Halafu ninaanza kupata wasiwasi na kile kiti cha spika,nadhani mtu akikaa pale akili kidogo haifikiri vizuri,badala ya busara kuongezeka, busara inapungua.Ngoja nisiendelee maana akili yangu imetibuka kweli nisije kujiharibia siku.
 
Hii ni kauli ya Mwanasheria Mkuu Bungeni kwa TUNDU LISSU.

Kauli hii imepelekea Lissu na wabunge wengine wa CDM kutoka nje ya Bunge.

Naibu spika amepinga Mwanasheria mkuu hajasema hivyo, na wabunge wa CCM wanapiga makele wakidai Lissu hakumsikia mwanasheria mkuu vizuri.

Tutafuka?
kwa mfumo huu ni dahahili hatuwezi kufka
wao wakisema sawa wenzao wakisema si sawa
 
Lissu anawachokonoa nao wanalipuka Alijua tu hawawezi kukubali ila taarifa itakuwa imeenda kwa watanzania wote kwamba kwa mara ya pili imekataliwa. Chuki kwa wazanzibari inazidi.

Baraza la wawakilishi lenyewe halijajadili hoja ya ajali, nyie bunge la muungano ndio mnajifanya mnajua sana kuliko wale wenye msiba wenyewe
 
yani wamekataa hoja ya lissu ya kujadili janga la meli kwa technicalities eti hakuiwasilisha kama kanuni za bunge zinavyotaka.Job anamtetea mwanasheria mkuu wa serikali eti hakusema maneno ya maudhi,
CDM,CUF ndo naona wametoka
 
Hivi wale wabunge wa CCM kutoka Zanzibar wamebaki ndani? Au wanasubiri UAMUSHO wawasemee.
 
ndg yangu, hao wanaweza kutoa rushwa hata huko darasani, hata wasipoingia darasani utakuta mbao za matangazo zinaonesha wameshinda mitihani

Lisu anajua sheria na ana hoja mara ishirini zaidi ya Werema.atake asitake hata wakiingia darasani Lisu atamuacha mbali sana Werema.
 
kwa kifupi naibu spika kachemsha kwa kukataa hoja ya lissu kwa ksisingizio kuwa amekosea kaununi kuwa hakutoa hoka.this is nonsense kwani hata kama amekosea kanuni angeweza kutumia common sense wakajadili jambo hili la msingi
 
Hivi kwani hili la kuzama kwa meli limeshapelekwa mahakamani fasta? Werema kilaza, Lukuvi kilaza, spika ndo wadhaifu balaaa!!!
 
Ubabe,matusi,na umbumbumbu wao bungeni ndiyo mtaji na fimbo yetu nje ya bunge na katika viwanja na majukwaa ya kisiasa.pole sana serkali yangu pole sana mwanasheria mkuu utamsinda lissu bungeni kwa wingi wa wanaccm lakin hutamshinda lissu nje ya bunge kamwe nakuapia
 
Baada ya kushuhudia malumbano hayo, sasa nimeamini, poasi na shaka kabisa kuwa serikali yetu ni mwoga mkubwa wa hoja.

Hivi kuna ubaya gani kulijadili suala hili? tena, katika mjadala serikali ingepata mawazo mazuri kutoka kwa wabunge jinsi ya kushughulikia masuala haya
 
katika kutengeneza mazingira kukwepesha ombi la Lissu juu ya kutoa hoja ili kujadili ajali ya mali iliyotokea juzi, AG- Werema ametumia kauli tata na ya matusi ikiashiria kwamba Lissu japo ana nywele lakini huwezo wa kufikili hana. jambo ambalo limezua mjadala hasa baada ya Lissu kuomba utaratibu na kumtaka Naibu Spika amwamulu AG-Werema afute maneno yake na Naibu Spika kakataa kukubaliana na Lissu; kuona hivyo Lissu kahamua kutoka nje kitendo hicho kimeitikiwa na baadhi ya Wabunge.

Ni kweli alichosema mwanasheria mkuu wa serikali, Lissu ana nywele ila akili aweza kuna hana, hilo ni tusi kwani ? mbona vichaa wana nywele ila akili hawana ? acheni kujitafutia umaarufu kwa kupitia misiba
 
Lissu anawachokonoa nao wanalipuka Alijua tu hawawezi kukubali ila taarifa itakuwa imeenda kwa watanzania wote kwamba kwa mara ya pili imekataliwa. Chuki kwa wazanzibari inazidi.

Aisee nakubaliana na wewe ameyaingiza mkenge yakajileta
 
Tatizo la CCM ndiyo hilo KUPINGA kila Hoja inayoletwa WAPINZANI. Hiyo MINDSET ndiyo inamtesa leo Spika Anne Makinda juzi alipokataa hoja Hamad Rashid.

Even my STD I hero knows that Tundu Lissu is clever than Werema

Nilikuwa naangalia bunge wakati mwanasheria mkuu anamtetea spika juu ya uamuzi wake wa kukataa ombi la Tundu lissu kutoa hoja ya kuahirisha bunge ili kujadili ishu ya ajali ya meli. Kwa kweli kwa uelewa wangu mdogo sana wa mambo ya bunge na sheria pia ( mimi si mwana sheria wala mbunge) huyu AG wa serikali yetu sijui aliwezaje kuwa jaji na kuteuliwa pia kuwa AG. Anavyojibu alivyokuwa anaongea ni wazi kabisa inaonesha hajui kanuni na pia anachokiongea na kuishia na kutoa lugha ya kuudhi wabunge wengine hasa mtoa hoja. AG ni mtu mkubwa sana sikutegemea anaweza kuwa hivyo.
 
Inaboa sana, zaidi ya watu miamoja wamekufa, watu wanakataa kujadili hoja kibabe tu. Hivi hawajui kama tunawaona live na kuwadharau maradufu? watu gani nyinyi msio na machungu na ndugu zenu? kila kitu mnaweka maslahi ya kisiasa mbele. Hivi mngepigwa bomu hapo nje msingejadili kwasbb nyepesi kwamba hoja haijaungwa mkono? Mlevi bwana akilewa baada ya kuepuka ngumi kwa kuwa uwezo umepungua ye ndo kwanza anamchokoza baunsa. Yani kama hamjui hii tabia ya kuzuia zuia na kufichaficha inayojengeka ndo inaongeza hasira zaidi.
 
Back
Top Bottom