Bungeni Live: Marekebisho ya Katiba: Malumbano Yamemalizika!

Mhe. Anna Kilango amesimama kukubali marekebisho hayo, hivyo ameliondoa rasmi lile pingamizi lake. Makofi.

Sasa Mhe. Spika analihoji bunge lote!
 
Wanaofiki waseme ndio, ...Ndioooooooooooo!.

Wasioafiki waseme sio, siooo!.

Spika: "Waliofiki wameshinda!"!. Bunge linaendelea!.
 
huu upande unaong'ang'ania MaDC wawepo una kitu gani nyuma ya pazia? why them, of all the people? intimidation tu, watu washindwe kutoa mawazo yao freely
 
Ole wao CCM wa influence Katiba iwapendelee wao as a ruling party, then waje washindwe 2015 na Chadema ndio wawe ruling party. CCM watalia na kusaga meno!
If they are smart, new katiba iwe as neutral and beneficial kwa nchi na si ruling party.
 
mtu wa kwanza anayepaswa kulaumiwa endapo katiba mpya itakuwa na matatizo ni ANNA KILANGO MALECELA
 
Wanaofiki waseme ndio, ...Ndioooooooooooo!.

Wasioafiki waseme sio, siooo!.

Spika: "Waliofiki wameshinda!"!. Bunge linaendelea!.

simply

muswada wa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba umepita
 
AG, ametoa hoja ya muswada ukubaliwe, Spika amelihoji bunge kwa mara ya pil;i amelihoji bunge na wameafiki, na sasa muswada umesomwa kwa mara ya tatu na kupitishwa moja kwa moja.

Spika anawashukuru wote!.
 
Prof Majimarefu hajapiga kelele za 'HAPANAAAA' ile kuuuubwa kuliko ya wenzake wote hapo mjengoni?

Mhe. Anna Kilango amesimama kukubali marekebisho hayo, hivyo ameliondoa rasmi lile pingamizi lake. Makofi.

Sasa Mhe. Spika analihoji bunge lote!
 
Hapo umeeleweka Pasco,ila nijavyo mimi DED anafanya kazi chini ya DC kwa vyovyote vile hapa atakayekuwa anafinal say katika hili atakuwa DC

Kama kuna DED anaefanya hivyo, atakua hafahamu ToRs ya kazi yake. Yeye anapaswa kuwajibika kwa waziri mkuu kupitia TAMISEMI, sasa iweje DC amchachafye?!?
 
Mbona vurugu sana bungeni? Malumbano yaameisha vipi ingali upinzani haukubaliani na marekebisho ya kamati ya bunge uliyokutana jana usiku...


Mungu wangu Tundu Lissu ana mwambia mwanasheria mkuu hajui kiingereza dah!

Acha uongo, hutizami TV pekee yako.
 
Final Update.
Muswada umepita!.
Kesho muswada huo unaletwa rasmi DSM na kulazwa ofisi ya bunge DSM. Jumatatu asubuhi, Katibu wa Bunge, Dr. Thomas Kashilila atabisha hodi Ikulu, na kuukabidhi rasmi.
JK atausani fasta fasta hata Jumatatu hiyo hiyo ili tangu J.4 uwe sheria.
Barua za mialiko kwa wadau kupendekeza majina ya wajumbe zitatolewa.
JK atateua wajumbe 14 kutoka bara na 14 kutoka Zanzibar pia atamteau M/Kiti na Katibu, jumla watakuwa 32.
Wataapishwa Ikulu.
Tarehe 01/03/2012 Tume ya Kukusanya Maoni Itaanza Kazi!.

Asanteni na Kwaherini.

Pasco.
 
Back
Top Bottom