Bungeni Live: Marekebisho ya Katiba: Malumbano Yamemalizika!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,441
113,450
`Wanabodi,

Ule mjadala wa jana kuhusu marekebisho ya sheria ya marekebisho ya katiba, Yale Malumbano ya jana kuhusu matumizi ya ma DC au ma DED umemalizika rasmi!.

Makubaliano hayo yamewakubali wote wawepo, ma DED na ma DC wawepo, ila tume imepewa mandate ya kuwatumia yoyote kati ya hao pale itakapoona inafaa!.

Kuliibuka tena malumbano ambapo Lissu aliibua tifu upya, AG, akamkomalia kuwa mbona jana alikubali, mwisho KUB, Mhe. Freeman Mbowe alikubali kufunika kombe mwanaharamu apite kwa kukubali yaishe. Muswada ukapita!.

My Take!.
Muswada umepita!.
Kesho muswada huo unaletwa rasmi DSM na kulazwa ofisi ya bunge DSM. Jumatatu asubuhi, Katibu wa Bunge, Dr. Thomas Kashilila atabisha hodi Ikulu, na kuukabidhi rasmi.
JK atausani fasta fasta hata Jumatatu hiyo hiyo ili tangu J.4 uwe sheria.
Barua za mialiko kwa wadau kupendekeza majina ya wajumbe zitatolewa.
JK atateua wajumbe 14 kutoka bara na 14 kutoka Zanzibar pia atamteau M/Kiti na Katibu, jumla watakuwa 32.
Wataapishwa Ikulu.
Tarehe 01/03/2012 Tume ya Kukusanya Maoni Itaanza Kazi!.

Asanteni

Pasco.
 
Umeisha kwa utaratibu upi watabaki ma DC au ma DED au wanatolewa wote iweke vizuri post yako huku Bupandagila Shinyanga umeme hatuna.
 
Msemaji wa Kamati ya Sheria na Katiba, Mhe. Angela Kairuki, ametoa taarifa ya kumalizika kwa utata huo. Mwanasheria Mkuu amefafanua, na sasa Mhe. Tundu Lissu anasema athari za marekebisho hayo!.
 
Makubaliano hayo yamewakubali wote wawepo, ma DED na ma DC kuitisha mikutano. Lissu ameshauri its a confussion, ameshauri wote waondolewe, Tume iitishe mikutano yenyewe. Waziri Lukuvi ameshauri ni busara wote wawepo!.
 
Bado sijakuelewa! Mkuu Pasco wala si kawaida yako kujikanyaga kanyaga katika maelezo yako leo kuna nini hapo newsroom?

Au ni hawa vijana wako akina Meena ndio wanakupotezeshea frequencies huko bungeni?
 
Mbona vurugu sana bungeni? Malumbano yaameisha vipi ingali upinzani haukubaliani na marekebisho ya kamati ya bunge uliyokutana jana usiku...


Mungu wangu Tundu Lissu ana mwambia mwanasheria mkuu hajui kiingereza dah!
 
Mwasheria Mkuu anafafanua, kuwa tume ina mandate ama ya kuwatumia, au kutowatumia. AG anamshushua Lissu kuwa yeye na Mdee, walikuwepo jana mpaka hiyo saa 6 usiku, na hakupinga!
 
Hapo umeeleweka Pasco,ila nijavyo mimi DED anafanya kazi chini ya DC kwa vyovyote vile hapa atakayekuwa anafinal say katika hili atakuwa DC
 
Bila ma DC, CCM wanajua kabisa katiba itakuwa haina chao(na ndicho watanzania tunataka) na wakiwatoa majimboni kura hakuna kwani wamekuwa wakitumika sana kuwanadi wabunge hata kwa kuwatisha watendaji kuhakikisha fulani anapita.
 
AG anasema, jana mambo yalipopamba moto, KUB alimfuata na kukubali compromise, na wote walikubali. Sasa KUB, Mhe. Mbowe sasa anazungumza!.
 
Mwanasheria mkuu anafafanua anasema kifungu kilichoongezwa hakiilazimishi tume kuwaweka maDC na DED
 
Mhe. Mbowe anahitimisha kuwa KUB inatambua umuhimu wa ma DC kama wawakilishi wa serikali, ila pia inatambua kwa uchungu role ya ma DC katika kuibeba CCM!.

"Tunakubali yaishe!", tunafunika tuu kombe ili mwanaharamu apite!, japo itakuja kutu cost huko mbeleni!.
 
KUB, anawasihi wabunge wa upinzani, tukubali yaishe, twendeni tukatengeneze katiba ya nchi, katiba ni muhimu kuliko vyama vyetu!

Anashangiliwa na bunge zima!.
 
Sasa anaongea Wasira, anampongeza Mhe. Mbowe kwa ku compromise, give and take ndio decent politics!.
 
Back
Top Bottom