Bungeni leo: Martha Mlata; Kanumba alitakiwa awe na Bodigadi na hakustaili kuishi Sinza

Dadio

JF-Expert Member
Mar 14, 2012
359
42
Mbunge huyu alipokuwa anachangia hoja kuhusiana na sheria juu ya haki za wasanii na kazi zao. Alsema maeneo aliyokuwa anaish marehemu kanumba ni uswahilin hatari kwa Jk pamoja na Pm na wengneo.

Aidha aliongeza kuwa msanii huyo alpaswa kua na bodgad wa kumlnda.
 
Yeye kama mbunge anaishia wapi? singida au london?
 
Ukumuuliza mtu mwenye akili timamu achague kati ya maisha 'huru' au kuzungukwa na mitutu kumlinda mpaka chooni atachagua maisha 'huru'. Lakini kwa sababu maisha 'huru' yanakuwa kwenye majaribu basi mtu analamizika kuzungukwa na watu wa miraba minne tena waliobeba salaha.

Kanumba hakuuwawa na majambazi, hakuvamiwa na watu asiowajua. Bodyguard anahitajika kama mtu anaona kuwa usalama wake unaweza kuwa hatirini. Huyu Martha Mlata anataka kutuambia kuwa Kanumba amekufa kwa sababu hakuwa na bodyguard? Au kwa sababu wanaona wenzao wa Hollywood na Nollywood wamezungukwa na mabaunsa basi Mlata anaona naye aige. Asilolitambua ni kwamba huko kwa hao ma-star mambo ni tofauti kabisa - kiusalama.

Kwa vyoyote vile, Kanumba amekufa katika mazingira ya scandal. Bahati ni kwamba msiba umevamiwa na wanasiasa kwa sababu zao wenyewe hivyo kipengele cha scandal kinafifia. Ni marehemu Kanumba na huyo binti wa miaka 17 (or 18) ndio wanajua nini kimemuua na pengine hali ingekuwa hivyo hivyo hata kama alikuwa anaishi Oysterbay.
 
Huyu huko bungeni sio mahala pake anafaa kuimba kwaya tu huko kwao Singida!! Hivi ccm hawaoni aibu kuwa na wabunge wa hadhi hii wanaodhani ni lazima wafungue vinywa vyao hata kama midomo yao inanuka?
 
Huyo ndiye mwakilishi wa wananchi na lugha zisizofaa. Wanaoishi Sinza si binaamu wa kawaida? Je Sinza nani anstahili kuishi huko? Je Martha Mlata anao walinzi wangapi kwa sasa? Au kajisahau hata jukumu lililompeleka mjengoni? Ni bahati mbaya sana lakini ebu tuendelee kusikiliza yatokanayo:yell:
 
yy ana mlinzi? uzunguni ni wapi uko ambako w2 hawafi? kweli bunge limevamiwa
 
Huyu Mbunge sijawahi kumsikia akiongea la maana, Ona leo tena ameropoka..

Kuna uhusiano gani kati ya kifo cha kanumba na kuishi uswahilini na kutokuwa na Bodigadi?
Ina maana yeye aligombea ubunge ili ajiwezeshe na asiishi uswahilini?
Je hawa wengine wanaoishi uswahilini hawana haki ya kuishi pengine?
Kwamba Kanumba alitakiwa asiishi uswahilini na awe na Bodigadi, kwa hiyo nini kifanyike?
kwamba tumfufue ili tumuondoe uswahilini kisha tumpatie mabodigadi? Halafu?

Hiki Kibibi sijui niaje aisee!! Yaani hapa kina entertain matabaka wazi wazi!!
Danm!!!
 
Hata haya haoni na umama wote ule anadiriki kutamka pumba hizo?? Kwahiyo bodyguard angeingia hadi chumbani kumlinda kanumba akiwa faragha na madem zake.
 
Mbunge huyu alipokuwa anachangia hoja kuhusiana na sheria juu ya haki za wasanii na kazi zao. Alsema maeneo aliyokuwa anaish marehemu kanumba ni uswahilin hatari kwa Jk pamoja na Pm na wengneo.

Aidha aliongeza kuwa msanii huyo alpaswa kua na bodgad wa kumlnda.

Maneno kama haya yanakuonesha UZUZU wa wengi wa wawakilishi wetu Bungeni:-(
 
  • Thanks
Reactions: kui
Back
Top Bottom