Bungeni kwawaka moto, ripoti za kamati zaibua mjadala mkali!

Watanzania mnapenda sana mazingaoombwe; mnafurahia sana sanaa ya majukwaani a.k.a sanaa ya maonesho! Hivi, mkiulizwa ni kipi ambacho kimesemwa leo na wabunge wa CCM kilikuwa hakijulikanai 2006? Jibu " leo wamezungumza vizuri sana, wameonesha makali yao".

Tukiuliza huu ukali unatofauti gani na ule uliooneshwa na wabunge wa CCM kwenye Richmond mwaka 2008? mtasema yeah ule ulikuwa ni kwa ajili ya Lowassa?

Tukiuliza ukali huu unatofauti gani na mjadala kama huu mwaka jana au mwaka juzi? mtasema ndio lakini safari hii mmoja wao kasema mafisadi "wanyongwe" kana kwamba ni mara ya kwanza mtu kussema hivyo bungeni!!!

na CCM wanajua sanaa wanawapa wananchi kile wananchi wanataka!!! Kitu pekee ambacho wamewanyima wananchi ni mabadiliko!!!

Ni kweli, tumekuwa mashabiki mno!
Naona kuna tofauti kidogo hapa, ndio yanayosemwa ni yaleyale lakini sasa toka pale Mh Mdee aliposema wasiishie kulalamika tu tumeona tone imebadilika kidogo.
Sisi Wananchi tuchukue hili tupress hapo hapo, tuelimishwe kanuni zinazoelekeza nguvu ya wabunge kuwajibisha Serikali, tuwa hold accountable kwa kutotumia nguvu hizo wakipata pressure toka kwetu, watatimiza wajibu.
 
Watanzania mnapenda sana mazingaoombwe; mnafurahia sana sanaa ya majukwaani a.k.a sanaa ya maonesho! Hivi, mkiulizwa ni kipi ambacho kimesemwa leo na wabunge wa CCM kilikuwa hakijulikanai 2006? Jibu " leo wamezungumza vizuri sana, wameonesha makali yao".

Tukiuliza huu ukali unatofauti gani na ule uliooneshwa na wabunge wa CCM kwenye Richmond mwaka 2008? mtasema yeah ule ulikuwa ni kwa ajili ya Lowassa?

Tukiuliza ukali huu unatofauti gani na mjadala kama huu mwaka jana au mwaka juzi? mtasema ndio lakini safari hii mmoja wao kasema mafisadi "wanyongwe" kana kwamba ni mara ya kwanza mtu kussema hivyo bungeni!!!

na CCM wanajua sanaa wanawapa wananchi kile wananchi wanataka!!! Kitu pekee ambacho wamewanyima wananchi ni mabadiliko!!!


Mzee Mwanakijiji. Ninakushukuru sana umesema vizuri. Binafsi sikufatilia bunge la jioni hivyo nilikuwa na hamu ya kujua kilichojiri. Kadri nilivyo zidi kupia uzi huu nilijawa sana na mshangao kwa jinsi wachangiaji walivyo onyesha kuhamasika gafla na hivyo kusahau historia ambayo hata muongo mmoja haijatimiza. Hii ndio Tanzania tuliyonayo na taswira halisi itaonekana kwenye vichwa vya magazeti ya kesho.

Umesema vema katika setence yako ya mwisho.Hakika wabunge wa CCM na serikali yao wanajua wanachofanya. Nikiungana na wewe, sioni chochete zaidi ya uigizaji.
 
kwa kweli naona wabunge wote wamekuwa kitu kimoja katika kukosoa matumizi ya serikali nimefurhishwa sana kwa hili. CCM tafadhalini chukueni kwa makini ushauri wa Mhe Godfrey Zambi. 2015 mtapata shida sana kuomba kura kutoka kwa wananchi msipokuwa makini aliyosema Mhe Zambi yatatokea yaani chama chenu kinaweza kisipewe tena redhaa ya kuongoza serikali.

Unawapenda? Kanywe nao chai.

 
[ QUOTE=Makupa;3726101]wabunge ccm kazeni kamba cdm watakosa cha kuongea[/QUOTE]

Stuka!! Usiwe kubwa jinga,Wanaoikosoa ccm yako wana damu ya Chadema.

 
Rais yuko Brazil
Waziri wa fedha yuko marekani
Waziri wa maji yupo marekani Waziri wa madini yupo Brussels
Waziri Mkuu yupo eneo la bunge lakini sio ndani ya bunge

Kaogopa kuingia, wenzie hawapo. Ungekuwa wewe ungefanyaje? Kuwa kiongozji nchi hii huhitaji kuwa na akili nyingi, ndiyo maana hao wote wapo na wanapeta.
 
Kila Ukimaliza Kusali Jitahidi Kumwingiza Mtu mmoja kwenye kundi la wanamageuzi, awe mjomba,shangazi, jirani nayeyote aliyekaribu!! Kama kwa sasa wanamageuzi wapo 2,000,000. Kila mtu akiweza kuongeza Mmoja then Jumla yake itakuwa 4,000,000. na kama katika hawa wakiweza nao kupata mtu mmoja kila mmoja jumla yake itakuwa 8,000,000!! Anza sasa bado Hujachelewa!!
 
Kana kwamba waliamua kuweka kumbukumbu kwenye hansard za bunge, wabunge hao wawili ambao ni wa CCM wamesema hadharani kuwa CCM ikipita mwaka 2015 ni bahati.

Alianza Ester Bulaya wakati wa kuchangia report ya CAG kwamba kama madudu yenyewe ni haya basi vijana sasa hivi wako zaidi ya asilimia 50 lakini kufikia 2015, jeshi la vijana litapanda kuwa asilimia kubwa na watafanya maamuzi yao kuondokana na uzembe huu.

Zambi yeye alieleza wazi kuwa uchafu na ufisadi kama huu unaotamkwa kwenye report ya CAG ndiyo ambao wapinzani wanausoma kwa makini na kwenda kuwatangazia wananchi jinsi serikali ilivyo ya kifisadi. Zambi alieleza isivyo rahisi kuwapinga wapinzani kwa ukweli huo na hivyo amesema si rahisi CCM kurudi madarakani 2015 kwa mtindo huu.

Ameongezea kwamba kama CCM itapenya tundu la sindano la mwaka 2015 basi isitarajie 2020 kupenya kamwe.

Usingeweza kuamini kwamba wale ni wabunge wa CCM wanaongea haya mbele ya nchi nzima na wapinzani wakiwemo humohumo. Mtizamo wangu ni kwamba wamechoka na wanaona kwamba kuanguka hakukwepeki na hivyo walau kuwe na rekodi zinazoonyesha kwamba walijaribu wawezavyo kuonya tena kuonya bungeni lakini chama chao kikapuuza.

Source:
Majadiliano ya report ya CAG leo April 18, 2012 kuanzia saa 11 jioni na yatakayorekodiwa kwenye hansard.
 
godfrey zambi.may be ataongea point even though kafulila caught him begging mdudu haramu

Huyu nae alijifanya mpambanaji wa ufisadi kumbe ni mchumia tumboni; na anajua wazi kuwa amekalia kuti kavu hakuna jinsi ya yeye kurudi mjengoni 2015 , hata hivi 2010 aliponea chupuchupu kwasababu ya kuchakachua!!
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom