Elizabeth Dominic
Platinum Member
- Dec 7, 2007
- 4,555
- 3,649
Watanzania mnapenda sana mazingaoombwe; mnafurahia sana sanaa ya majukwaani a.k.a sanaa ya maonesho! Hivi, mkiulizwa ni kipi ambacho kimesemwa leo na wabunge wa CCM kilikuwa hakijulikanai 2006? Jibu " leo wamezungumza vizuri sana, wameonesha makali yao".
Tukiuliza huu ukali unatofauti gani na ule uliooneshwa na wabunge wa CCM kwenye Richmond mwaka 2008? mtasema yeah ule ulikuwa ni kwa ajili ya Lowassa?
Tukiuliza ukali huu unatofauti gani na mjadala kama huu mwaka jana au mwaka juzi? mtasema ndio lakini safari hii mmoja wao kasema mafisadi "wanyongwe" kana kwamba ni mara ya kwanza mtu kussema hivyo bungeni!!!
na CCM wanajua sanaa wanawapa wananchi kile wananchi wanataka!!! Kitu pekee ambacho wamewanyima wananchi ni mabadiliko!!!
Ni kweli, tumekuwa mashabiki mno!
Naona kuna tofauti kidogo hapa, ndio yanayosemwa ni yaleyale lakini sasa toka pale Mh Mdee aliposema wasiishie kulalamika tu tumeona tone imebadilika kidogo.
Sisi Wananchi tuchukue hili tupress hapo hapo, tuelimishwe kanuni zinazoelekeza nguvu ya wabunge kuwajibisha Serikali, tuwa hold accountable kwa kutotumia nguvu hizo wakipata pressure toka kwetu, watatimiza wajibu.