Bungeni kumewaka moto-mgomo wa madaktari

umekurupuka!!!!!!!!! hatuuoni moto wala zimamoto, bunge limeridhia 'kwa kupitia "kanuni" za bunge' serikali iendelee kuwaua kwa kuwanyima watanzania huduma za afya kwa kushindwa kutatua mgogoro wake na madaktari. nilitarajia wabunge watoke nje ya ukumbi kususia mjadala wowote ikiwa ni hatua ya kuungana na wananchi wanaowawakilisha.
 
Mama makinda kaniuzunisha sana......huyu mama hana huruma,sio mama,hana utu,hana ubinadamu kwa kifupi namfananisha na dizaini ya wauaji wa albino.....

attachment.php
 
umekurupuka!!!!!!!!! hatuuoni moto wala zimamoto, bunge limeridhia 'kwa kupitia "kanuni" za bunge' serikali iendelee kuwaua kwa kuwanyima watanzania huduma za afya kwa kushindwa kutatua mgogoro wake na madaktari. nilitarajia wabunge watoke nje ya ukumbi kususia mjadala wowote ikiwa ni hatua ya kuungana na wananchi wanaowawakilisha.
Sijaona kidude cha Like
 
Je unafahamu mamlaka ya Bunge?

Je Bunge linaweza kuwalipa Ma Dr Mishahara yao na stahiki zingine wanazodai?

Je wabunge hawaamini kamati yao ya huduma za jamii?

Kwanini wasiwe na subra kupata ukweli sahihi? kabla ya kutaka kukurupuka?

Fikirieni mipaka ya bunge kimamlaka kabla kujadili suala hili.


Madaktari wanatambua fika kuwepo kazini kwa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii. Kwa kuwa Madaktari Bingwa (tegemeo lililobakia) wameanza pia mgomo...ni jambo la busara kwa Bunge kulijadili suala hilo na kuchukua hatua za dharura kumaliza mgogoro huo. Madaktari wana hoja nyingine pia si POSHO tuu kamma wananchi wanavyoaminishwa.
 
Jamani kwanini Bunge lisimame wakati kamati yake ya huduma za jamii inalishughulikia suala hilo? Kwanini wabunge wasiwe na subra kusubiri majibu ya kamati?

Labda tujiulize wanataka kujadili nini kuhusu kadhia hiyo? au wanataka wavute muda na kuongeza posho.

Tafadhali wa Tz mnatakiwa kujua muda ni mali sana.

Nawapa pole wale wanaoshabikia issue hii ya mgomo.

Mkuu issue sio kuongeza muda bungeni.tatizo madactar bingwa jana wameanza kugoma muhimbili pamoja na kua kamati hiyo haijarudi ila hali inakua mbaya zaidi.inamaana kua mdactar hao kugoma itabidi muhimbili ifungwe.na hivi sasa wagonjwa wanafukuzwa.itakuwaje waisubiri tume mpaka irudi wakati hali imeshakua mbaya kiasi hicho?kweli bi mkubwa anaroho chafu
 
jk asife, apate busha ashindwe kufaa suti alizohongwa!!!!!!!

hahaahhaa.........apate busha?!!!!!......yawezekana wewe unatamani ule utabiri wa TB JOSHUA utimie huku bongo!! haha
 
Katika hali ya kawaida, si vyema kujadili jambo ambalo tayari linashughulikiwa na kamati ya bunge. Katika hili speaker yuko sahihi pamoja na ukweli kwamba suala hili linahitaji suluhu ya haraka kunusuru maisha ya watanzania.
 
Sijui wabunge wa CCM wanatambua madhara ya huu ubabe wa Spika kuhusu mgomo wa madaktari? Mabunge yenye speaker anayeelewa nafasi ya bunge sio tu angeruhusu mjadala bali hata kama wabunge wangekuwa likizo angeitisha bunge mahususi kujadili swala nyeti kama huu mgomo wa madaktari. Tofauti na sector zingine mgomo wa madaktari unahatarisha uhai wa raia. Kamati ya bunge ingepewa jukumu la kutafuta kiini (enquery) kwa madhumuni ya kuhakikisha suala kama hilo halitokei tena huko mbele na sio hiki anachosema mama Makinda. Bunge lilipaswa kujadili hatua za dharura kwa haraka.

Kwa upande mwingine ubabe wake unazidi kuwapandisha hasira madaktari. Hiyo kamati itakuwa na wakati mgumu sana kupata suluhu.

Kama nilivyosema response ya mama Makinda itawamaliza wabunge wa ccm. Na tofauti na zama za RTD sasa hivi every move anayofanya huu mama iko iko live, wananchi wanaona, wanaelewa na mbaya zaidi wameshakuwa na fikra kuwa ccm kwa msaada wa speaker wameamua kuwatelekeza wananchi!

Je wabunge wa ccm wana uwezo wa kujiondoa kwenye hili tope?
 
Wameomba bunge lisitishe kila kitu wajadili inshu ya mgomo coz watu wengi wanakufa baada ya maspecialists kugoma

Yaani sipati:photo::photo: kuna mambo ya dharura ambayo yanapashwa kjadiliwa na kupata mwafaka hata usiku wa manane, sasa hawa kila siku ndiyo hoja yenyewe mara oooo kamati ishughulikie,
 
Kuna Mbunge amesimama na kunukuu vifungu na pia taarifa ya habari na mazungumzo yake na wafanyakazi Wa Muhimbili kuwa madaktari bingwa wamegoma na wagonjwa wakitolewa wodini. Amelitaka bunge kuahirisha shughuli zote za Leo na kujadili Hali tete ya afya za watanzania. Wabunge wote walisimama kuunga mkono, Mh spika a.k. a Bi Kiroboto akawaamuru waliosimama, kaa chini! Ikasikika
Sauti kuomba mwongozo akakataa, nyingine ikisema taarifa, akakataa na kumuita Ngeleja aanze kutoa hoja ya gas issue huku wabunge wakitoka nje mmoja baada ya mwingine

Waliotoka nje ndo wameonesha uzalendo,...
ningependa kuwafahamu.
 
Natamani watanzania wangepata uchungu kama nilio nao mimi sasa hivi,tungekwenda Muhimbili
tukawachukua wagonjwa tukawapeleka ikulu,halafu tungeona huyu jamaa wa Magogoni kama
angeendelea kukaa kimya na huyo bi Mkora kama angeendelea na vikao vyake bungeni"
AGHHH!!!! JAMANI WA TZ tupunguze upole hii imekuwa too much sasa!!
 
Back
Top Bottom