Bungeni - Highness Kiwia (Ilemela) atoa semina kwa Wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bungeni - Highness Kiwia (Ilemela) atoa semina kwa Wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 21, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Willium Lukuvi
  akifuatilia mjadala wa Bajeti Bungeni mjini Dodoma jana

  Mbunge wa Ilemela (Chadema) Highnes Kiwia ambaye aliiponda bajeti hiyo na kuipongeza bajeti iliyotolewa na wapinzani akisema ndiyo iliyopaswa kutekelezeka.

  "Bajeti mbadala ilipaswa kusomwa na positive mind kwani ikisomwa na negative mind sio tu msomaji ataona giza, bali atatumbukia gizani," alisema Kiwia na kuongeza:

  "Sisi tunachofanya sio kubeza mafanikio, ila tunasema mafaniko yaliyopo hayaendani na wingi wa rasilimali tulizonazo, hatusemi hakuna kilichofanyika. Nyerere alisema, ili kuwa na maendeleo tunahitaji viti vitatu; watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora hakutaja fedha.

  "Alisema (Nyerere) hatuwaondoi wakoloni kwa sababu tunachukia rangi zao, ni matendo yao. Sasa mkoloni wa leo ni ufisadi. hakuna namna Tanzania tukaondokana na umaskini kama hatuwezi kuondoa ufisadi."

  Mbunge huyo ambaye ametishia kuikwamisha bajeti hiyo aligeukia sekta ya umeme akimtaka waziri Ngeleja kuongeza kasi ya utendaji wake ili huduma hiyo iwafikie watu wengi zaidi kuliko ilivyo sasa. "Namwambia ndugu yangu, Ngeleja, watu hawataki mahesabu ya Megawati, wanataka umeme," alisema.


  Mwananchi
   
 2. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  safi kabisa nakubaliana nae 100%
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Rais Kikwete huko Malasya amesema afrika nchi nyingi afrika ni maskini sababu ya kukosa pesa za misaada ili kuendeshea miradi ya maendeleo. Anapingana na itikadi za hayati Nyerere kwamba ili tuendelee tunahitaji watu ardhi, siasa safi na uongozi bora kama alivyowakumbusha wabunge mheshimiwa Mbunge wa Ilemela. Ina maana Rais wetu anachojua maendeleo huletwa na pesa? Walioanza kuendelea walipata wapi pesa? Watu, ardhi, siasa safi na uongozo bora ndio msingi wa maendeleo, eti tunahitaji pesa ili tuendelee na pesa zinaishia mifukoni mwa viongozi wa serikali maana yake kukosa uongozi bora.
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kobe akinyamaza anatunga sheria, huyu jamaa amekuwa kimya mda mpaka nikasahau jina lake tofauti na mwenzake wenje. safi sna timu ya CDM
   
 5. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kiwia...............
   
 6. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mkuu hawa jamaa wa CDM ni Noma woote leo nimemshuhudia na Mh. Machemli ni hatari kwa wazembe na ni wajasiri full data and focused
   
 7. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hiyo ndiyo inavyotakiwa,wabunge wengi waipongeza bajeti wakati kwenye majimbo yao kuna matatizo yanayowakabiri
   
 8. M

  Madenge Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hizo pesa za misaada hata wakimmwagia kama mvua kama uongozi wake hautabadilisha mienendo yao hakutakuwa na maendeleo yeyote. Pesa si msingi wa Maendeleo!
   
 9. A

  Anold JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Kwa hili la Tanesco sikubaliani na kiwia kuwa hawana walilofanya. Tanesco ya miaka iliyopita siyo hii ya leo nafikiri bado baadhi ya watu wamebaki na historia, Tanesco ya sasa inafanya kazi zake kwa mpangilio unaoeleweka, sikutarajia hata siku moja kuwa nitakuja kuwasha umeme wa Tanesco ila nataka nikuhakikishie kuwa nilipofanya mchakato wa ufuatiliaji nilishangaa jinsi Tanesco walivyokuwa wanafanya shughuli zao kwa uhakika kiasi cha mtu kama mimi kupata huduma hiyo bila kutoa chochote ndani ya week tatu toka nilipe kiasi cha pesa kilichohitajika, awali nilikuwa natumia jenereta, kwa siku tatu petrol ya sh.10,000/= sasa hivi hiyo elfu kumi napata uniti kama sikosei zaidi ya hamsini ambapo nazitumia kwa zaidi ya week tatu au mwezi kabisa, sasa jamani ni kweli hawajafikia hicho kiwango kinachotakiwa ila kwa sasa wanajitahidi tuwatie moyo matatizo mengine yako nje kabisa ya uwezo wa Tanesco.
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Highnees Samson Kiwia, Hometown (Kibosho)
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na kinachojilia kauli za wabunge wa Chadema kwamba watu makini wenye mtazamo makini kwa ajili ya kujenga taifa makini. Hoja na kauli zao zinapenya na kunyong'onyeza, ukweli, hali halisi ya maisha na kueleweka hata kwa mtu ye yote. Si hoja ya kisiasa ila ukweli wa hali halisi ya maisha yalivyo. Imefika sasa kila mtu anasema CCM tuiweke kando, wamechoka na tumewachoka, wakae kando wapumzike waone jinsi na wengine wanavyofanya ili wapate kuwanyooshea vidole. Huu ndio mchezo wa siasa wenye kuleta tija kwa taifa.
   
 12. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yani! yani! yani! CDM MP'S wapo tooooo smart! yani! yani! unaenjoy bunge fleve those jamaa wanapokuwa wakipafomu!
   
 13. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #13
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Ni mbunge wa Kibosho kwani si wa jimbo mojawapo pale rock city?
   
 14. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #14
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Well said wanapafomu wakimaliza miaka yao mitano wanalipwa viinua mgongo vya maana wanakuja kuwapiga porojo wanarudi tena basi their lives goes on na nyie mnabaki na burudani za maneno. Moral of my comment: "action speak louder than words"
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Anold we una bahati na labda unafahamika. Niliomba kuletewa umeme nikajaza form na ikachukua wiki bila hatua zo zote kuchukuliwa na wakati likizo yangu inakaribia nirudi ninakobangaisha maisha. Fundi akaniambie suala nimwachie yeye anajua namna ya kuwapata, na amini usiamini form nilizojaza hazikutumika na fundi siku hiyo hiyo alirudi na mtaalamu mkadiriaji na kesho yake umeme uliwaka. Mambo bado sana tusitetee hilo. Kuna tofauti na wanaangalia nani na kama sura isiyofahamika au jina geni basi ujue utakutana li red light na bahati yako ulipata green light.
   
 16. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Huyu bwana nakumbuka nilikaa naye hapo nyuma kabla ya kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu uliopita pale Arusha aikiwa na muheshimiwa mwenzake ambaye sasa hivi ni mbunge wa Arusha mjini muheshimiwa GodBless Lema kwakweli alinipa hamasa kubwa sana wakati akiniambia anajikita katika kugombe jimbo la Ilemela Mwanza, amekomaa sana na anauchungu sana wa kuliletea jimbo lake maendeleo. Keep it Up Highness Kiwia kwa kutuonyesha vijana kua nasi tunaweza.

  [​IMG]
   
 17. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  I agree with u, but not all MPs. Wanachopigania kufa na kupona Chadema kinaeleweka na kila mmoja hata mwanakijiji anaelewe, ya yale yanayopiganiwa na MPs wa CCM kinaeleweka ulaji tofauti na uwajibikaji. So sera ziko wazi pande zote mbili na hata kushinda kwa wingi wa kura dhidi ya haki inayodaiwa ni ishara tosha ya kuiongezea nguvu bendera ya Chadema kupepea. Chama cha magamba wangekuwa na miwani ya kuona mbali wangeshukuru kutekeleza sera ya Chadema kiwani atakayefahamika mtekelezaji serikali yao lakini wamevaa miwani kizai hawaoni mbali na zaidi ya kuona kiza mbele yao na hivo CCM nam iwani yao ya kiza kufifisha rays za energy ya Chadema hali inayowageukia kukzidi kuwapotezea mwelekeo wa gari wanaloendesha kutumbukia mtaroni.
   
 18. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Actions gani unataka Shossi? Wakiitisha maandamano wanaambiwa wanachochea fujo na kuhatarisha amani, wanatupwa lumande na kubambikwa kesi...wakisema fungeni milango bungeni tuchapane makofi ili watu wawe serious wanaambiwa 'wahuni'...wakisema bungeni sio sehemu ya kuuza sura wanaombewa miongozo ya spika eti wanatumia lugha za 'mtaani'...wakirudisha mpambano bungeni wanaambiwa longo longo 'actions speak louder! Wafanyaje sasa?
   
 19. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  nikweli kabisa, kwani wamepewa mingapi na hatuoni chochote
   
 20. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Comments za kibaguzi hizo...
   
Loading...