Bungeni: Felix Mkosamali amlipua Pinda

QinetiQ

Member
Feb 28, 2014
33
70
Akiwasilisha Makadirio ya Bajeti Wizara ya Ujenzi Kambi ya Upinzani Bungeni jana jioni, Mh. Felix Mkosamali Amemlipua Waziri Mkuu Mizengo Pinda nanuukuu :
MAGARI YANAYOZIDISHA UZITO, MIZANI NA UHARIBIFU WA BARABARA

Mheshimiwa Spika, Uamuzi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuruhusu malori makubwa ya mizigo yaendelee kuzidisha uzito wa mizigo, umetajwa kuwa ni hatari na utaisababishia Serikali hasara ya mamilioni ya fedha.
Hasara hiyo inatokana na uharibifu wa barabara za lami ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa cha malori yanayozidisha uzito wa mizigo kinyume na kanuni 7 (3) ya Sheria ya Usalama Barabarani ya 2001.

Mheshimiwa Spika, Matakwa ya sheria Sheria Na. 30 ya 1973 na kanuni Namba 30 ya 2001 iliyotangazwa kwenye Gazeti la Serikali tangazo Namba 30 la tarehe 9 Februari , 2001 iliyoanza kutumika tarehe 24 Januari 2001 inafafanua uzito wa magari unaotakiwa. Kipengele cha saba cha sheria hiyo kinaeleza magari yote yenye uzito kuanzia tani 3.5 na kuendelea na aina ya makosa ya uzidishaji uzito, ambapo kifungu cha 2, 3 na 4 vinafafanua matumizi ya uzito uliozidi asilimia tano.

Mheshimiwa Spika, Waziri wa ujenzi Mhe. Magufuli aliwahi kunukuliwa akisema ataendelea kusimamia sheria ya barabara namba 30 ya mwaka 1973, hadi anaingia kaburini kwa kuhakikisha hakuna magari ambayo yanazidisha uzito na kuharibu barabara. Namnukuu Mh John Pombe Maghufuli“Nchini Ujerumani, uzito wa magari yote ni tani 40, Uingereza tani 40, Ufaransa tani 40, Urusi tani 38 lakini Tanzania tani 56, wakati mwingine tunakamata hadi tani 96,” alisema,Magufuli.

Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, ujasiri wa Dk Magufuli ulizimwa na amri ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliyetengua agizo la waziri huyo na kuamua kuruhusu magari yenye uzito uliopitiliza kuendelea kuharibu barabara.

Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa barabara unatumia gharama kubwa na hata ukarabati wake umekuwa ukitengewa mabilioni ya fedha za walipakodi kutokana na uharibifu unaofanywa. Mathalani katika bajeti yake ya 2013/14, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, ilitenga kiasi cha Sh bilioni 314.535 kwa ajili ya mpango wa matengenezo ya barabara kuu na

Barabara za Mikoa

Mheshimiwa Spika, Kiasi hicho cha fedha ambacho ni zaidi ya robo ya bajeti nzima ya wizara hiyo kwa mwaka, kinatosheleza kujenga barabara mpya ya lami yenye urefu wa kilometa zipatazo 315, kwa makadirio ya kilometa moja kugharimu Sh1 bilioni. Katika mwaka huu wa fedha, bajeti nzima ya Wizara ya Ujenzi ni Sh trilioni 1.226 .

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inapenda kuelewa hivi katika kuingilia tatizo hili la amri iliyotolewa na Mhe. Waziri mwenye dhamana ya barabara kulikuwa na mashauriano au ilikuwa ni wakubwa kuvuana ngua hadharani? Katika utendaji wa namna hii je watanzania watarajie tija kutoka kwa Serikali yao? Baba wa taifa aliwahi kusema serikali makini ni yenye kuwa na kauli moja na uwajibikaji wa pamoja(collective responsibility).

Mheshimiwa Spika, aidha kambi rasmi ya upinzani inamtaka waziri mkuu alithibitishie bunge kwamba yeye na marafiki zake na viongozi wa CCM wanamiliki maroli pia wana share katika makampuni mbalimbali na hivyo ndo maana imekua rahisi kwa yeye kuruhusu uzidishaji wa mizigo katika maroli na kuunga mkono uharibifu wa barabara zetu zilizojengwa kwa jasho la walalahoi ili yeye na marafiki zake wazidi kuneemeka na kukubali uhalibifu wa barabara kwa maslai yao binafsi na maroli yao
 

kiwososa

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,124
1,500
Jamani mtamuua bure huyu mzee Mfipa wa watu achene amalize muda wake akapumzike!!! huyu mzee mara zote yeye anatumikaga kama mbuzi wa kafara tu maana amepewa mamlaka kwa mkono wa kulia kasha akanyang`anywa kwa mkono wa kushoto. mbaya zaidi anatumika kutetea dili zote za wakubwa zake na ndugu/jamaa/washikaji wa wakubwa zako kwa hasara yake mwenyewe!!!! kwa mimi binafsi kwa muda huu huyu mzee wangu Pinda amekuwa waziri mkuu ni afadhali kabisa hicho cheo kingefutwa kwa muda then baadae kirudishwe kuliko kilivyotumika vibaya kipindi hiki.Mzee wangu Pinda namuheshimu sana na ninamfahamu utendaji wake wa uadilifu siku nyingi sana ila hapa amekengeuka kwa kukubali kutumika vibaya.I`m off!!!!
 

OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Ukiona mpaka wanao wa kuwazaa kabisa wanakitifua ujue baaaaas tena!!!!!!!!!!!
 

isambe

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
2,169
2,000
Hivi ile kampuni ya MULTIMODAL TRANSPORT , mmiliki wake ni nani? , naona ghafla imeibuka na MAN TRUCKS MBIIICHI.
 

Mahebe

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
320
195
Nilijua uko siku Pinda atashughulikiwa na angalau hapa wapinzani waneona , safi sana.
 

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,700
2,000
Pinda anafanya biashara ya kusambaza nafaka kwenye maghala ya chakula nchini ....Mbunge wa Sumbawanga Aeshi ndio msimamizi wa mradi huo......
 

Popompo

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
409
170
ccm hawajazoea kuambiana ukweli,kesho utasikia UVCCM wana maandamano ya kupinga waziri mkuu kakosewa adabu!Ahsante Mkosamali ila mmechelewa sana kumpa pinda za uso,
 

kill

JF-Expert Member
May 21, 2013
1,830
0
pinda amepinda kama jina lake anavunja sheria makusudi kwa sababu ni waziri mkuu ni aibu kubwa sana kwa serikali ya ccm mawaziri kupishana kauli kwenye jambo moja pinda alishasema serikali imechoka sasa unategemea nn
 

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,873
1,500
ccm hawajazoea kuambiana ukweli,kesho utasikia UVCCM wana maandamano ya kupinga waziri mkuu kakosewa adabu!Ahsante Mkosamali ila mmechelewa sana kumpa pinda za uso,

Afadhali iwe maandamano kupinga KUKOSOLEWA lakini kitachosema ni kwamba UVCCM WANAPINGA MHE. WAZIRI MKUU KUTUKANWA! CCM katika KAMUSI yao KUKOSOLEWA = KUTUKANWA!
 

Nanyengo83

New Member
May 13, 2014
2
0
Yaani hawa jamaa wanatufanya sisi misukule yao kwa kuwalimia wao wanavuna kiurahisi. Hebu angalia ssa kodi zetu walala hoi zinavyotumika kwa manufaa ya wachache. Ama kweli sheria zimetungwa ili zivunjwe. Hapo huyu mzeeni akalime mahindi kwao.
 

measkron

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,784
2,000
Hivi ile kampuni ya MULTIMODAL TRANSPORT , mmiliki wake ni nani? , naona ghafla imeibuka na MAN TRUCKS MBIIICHI.

Mkuu hii nchi inaendeshwa kihuni tu na Mie nimeiaikia nikawa najiuliza maswali lazima atakuwa na kigogo mmojawapo tu
 

TONGONI

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
1,038
1,500
Sio uharibifu wa barabara tu bali pia inachangia kwa kiwango kikubwa ajali za barabarani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom