Bungeni Dodoma: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akosa Mbunge wa kumuuliza swali la papo hapo

Habari wanajukwaa, ni utaratibu wa kawaida wa kila Alhamisi Wabunge hupata nafasi ya kuuliza maswali kwa Waziri Mkuu na kupatiwa majibu ya moja kwa moja hasa kuhusu mambo nyeti yanayopaswa kupatiwa majibu ya haraka toka serikalini.

Ila hali imekuwa tofauti katika Bunge hili na hali hiyo imedhihilika leo wakati wa kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu nimemsikia naibu Spika, Dr Tulia, akitangaza kuwa leo hakutakuwa na kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu kwa sababu hakuna Mbunge hata mmoja aliyejiandikisha kumuuliza swali Waziri Mkuu, makubwa haya!

Nikikumbuka Bunge lililopita, nilikuwa naisubiria kwa hamu sana siku ya Alhamisi kumuona kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati huo, kupata wasaa wa kumuuliza Waziri Mkuu juu ya sensitive essues. Pia kulikuwa na Wabunge wengine wakina Heche, Mnyika, Msigwa na n.k (mnisamehe kwa kumention waliokuwa Wabunge wa CDM tu kwa sababu hao ndio waliokuwa wanauliza sana maswali - so lirahisi kuwakumbuka) nao walikuwa "Wanamshambulia" Waziri Mkuu kama nyuki kwa maswali ya kina.

Bunge hili hali ni tofauti, yani katika Wabunge wote wale zaidi ya 300 eti wamekosekana hata watatu wakumuuliza waziri Mkuu kuhusu ata ule uchunguzi alioagiza mh. Raisi, Mh. Samia, ufanywe pale BOT katika pesa zilizotoka kuanzia mwezi January hadi March umefikia wapi?. Au kuuliza serikali inampango gani kuwashawishi "waliokimbia" nchini wakati wa utawala wa Mwendazake warudi waje kujenga nchi sasa kwa kuwa mambo ni "swali", kweli jamani?. Hii imenisikitisha sana kwa kweli!, Je nini kimepelekea kuwepo kwa hali hii?

Walasam.
atapataje wa kumuuliza swali angali wabunge wote ni vilaza wanaowaza ni saa ngapi wakasaini ili wachukue posho zinazotokana na kodi za wananchi wakazile na kunya?
 
Ukiona hakuna swali ujue kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa.
Hakuna wa kuuliza maswali
Sababu hao wabunge walipatikana kwa promotion,wanaogopa kuachwa kwenye uteuzi 2025 hivyo wamegeuka washangiliaji.
 
Bunge DHAIFU
Habari wanajukwaa, ni utaratibu wa kawaida wa kila Alhamisi Wabunge hupata nafasi ya kuuliza maswali kwa Waziri Mkuu na kupatiwa majibu ya moja kwa moja hasa kuhusu mambo nyeti yanayopaswa kupatiwa majibu ya haraka toka serikalini.

Ila hali imekuwa tofauti katika Bunge hili na hali hiyo imedhihilika leo wakati wa kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu nimemsikia naibu Spika, Dr Tulia, akitangaza kuwa leo hakutakuwa na kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu kwa sababu hakuna Mbunge hata mmoja aliyejiandikisha kumuuliza swali Waziri Mkuu, makubwa haya!

Nikikumbuka Bunge lililopita, nilikuwa naisubiria kwa hamu sana siku ya Alhamisi kumuona kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati huo, kupata wasaa wa kumuuliza Waziri Mkuu juu ya sensitive essues. Pia kulikuwa na Wabunge wengine wakina Heche, Mnyika, Msigwa na n.k (mnisamehe kwa kumention waliokuwa Wabunge wa CDM tu kwa sababu hao ndio waliokuwa wanauliza sana maswali - so lirahisi kuwakumbuka) nao walikuwa "Wanamshambulia" Waziri Mkuu kama nyuki kwa maswali ya kina.

Bunge hili hali ni tofauti, yani katika Wabunge wote wale zaidi ya 300 eti wamekosekana hata watatu wakumuuliza waziri Mkuu kuhusu ata ule uchunguzi alioagiza mh. Raisi, Mh. Samia, ufanywe pale BOT katika pesa zilizotoka kuanzia mwezi January hadi March umefikia wapi?. Au kuuliza serikali inampango gani kuwashawishi "waliokimbia" nchini wakati wa utawala wa Mwendazake warudi waje kujenga nchi sasa kwa kuwa mambo ni "swali", kweli jamani?. Hii imenisikitisha sana kwa kweli!, Je nini kimepelekea kuwepo kwa hali hii?

Walasam.
 
Ndio maana Spika kila leo anamtaja Mbowe

Ukweli wanawamisi wanaowaita wapinzani, wanamisi challenge na mawazo yao wanapishi purukushani ndani ya mjengo.
 
Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson amesema, leo kulikuwa na kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, lakini hakuna mbunge hata mmoja aliyejiandikisha kwa ajili ya kumuuliza Waziri Mkuu.

Nchi yetu ina matatizo mengi kuanzia elimu, afya, maji, haki za binadamu, ajira nk. Haiwezekani wawakilishi wote wakose hata kitu kimoja cha kuihoji serikali.

Kama taifa tuna hasara kubwa lkn wabunge wataendelea kunufaika na posho za vikao na usishangae kesho wakasema siku za vikao vya bunge hazitoshi na posho iongezwe wakati hawana hata swali moja la kuihoji serikali, haya ni matumizi mabaya ya pesa ya mlipa kodi.

Kama wameishiwa maswali tusisikie wanataka muda wa bunge uongezwe kama kero zimekwisha warudi majimboni.
 
Kama taifa tuna hasara lakini wabunge wataendelea kunufaika na posho za kikao na usishangae kesho wakasema siku za kikao cha bunge hazitoshi na posho iongezwe wakati hawana hata swali moja la kuihoji serikali haya ni matumizi mabaya ya pesa ya mlipa kodi.
 
Back
Top Bottom