Bungeni Dodoma: Nape ashinikiza Serikali kuunda Bodi ya Korosho, asema Kaimu Mkurugenzi amepewa kazi kubwa kuliko uwezo wake

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye ametaka kuundwa kwa Bodi ya Korosho ambayo haijakuwepo kwa miaka mitatu akihoji, nini lengo la Serikali na zao hilo?

Akiwa Bungeni amesema, "Zao ambalo linaongoza kuingiza Fedha nyingi za kigeni Nchi hii mwaka wa tatu hakuna Bodi. Mkurugenzi yupo anakaimu, na bahati mbaya ninadhani amepewa kazi kubwa kuliko uwezo wake"

Ameongeza kuwa, Kiongozi huyo ameshindwa kazi na kutaka aletwe mwingine akieleza, "Huyu Mkurugenzi anafika mahali akibanwa na wakulima anaanza kujibu majibu ya kiburi"
 
Back
Top Bottom