=========
Habari waungwana,
Leo aliyekuwa mbunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, marehemu Dkt. Elly Macha anaagwa bungeni. Mpaka sasa watu kadhaa wametoa salam ikiwemo mama Sitta na wengineo.
Kwa sasa anaeongea ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Freeman Mbowe na anamshukuru sana balozi AshaRose Migiro kwa kuwa karibu na marehemu kipindi cha ugonjwa alipokuwa akipata matibabu Uingereza pia kusimamia shughuli zote kwa marehemu akiwa huko. Anasema marehemu amemuacha mama yake mzazi na mtoto mmoja.
Anaeongea kwa sasa ni naibu spika wa bunge, Dkt Tulia Ackson na anaelezea shughuli nzima ya kuupokea mwili na kuupeleka Dodoma na wote waliohusika. Tulia anasema marehemu alikuwa mnyenyekevu na anatambulisha ndugu wa marehemu ambao ni mtoto wake na ndugu mwingine.
Kassim Majaliwa: Tunajua ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu lakini sie ndio tunapatwa na huzuni, sina mashaka na wasifu uliosomwa mbele yetu, marehemu ni mwenzetu ambae leo ametutoka. Tunatambua mchango wake, nafasi yetu kubwa sasa ni kumuombea mwenzetu.