BUNGENI, DODOMA: Mbunge ahoji kwanini Askari Polisi wana vitambi vikubwa hadi kushindwa kufanya mazoezi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
MBUNGE wa Kuteuliwa, Abdallah Bulembo, amehoji bungeni mjini Dodoma kwa nini baadhi ya askari polisi wana vitambi vikubwa

Bulembo alitoa hoja hiyo jana alipokuwa ananchangia mjadala wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka ujao wa fedha.

Alihoji sababu za baadhi ya askari kuwa na vitambi vikubwa, akidai vinasababisha washindwe kufanya mazoezi ya kiaskari.

Mbunge huyo pia aliishukia Idara ya Uhamiaji akidai imekuwa ikihangaika na wahamiaji haramu wanaopita kutoka nje huku ikiwalinda walioko ndani ya nchi.

Alisema pamoja na idara hiyo kufanya kazi nzuri, imekuwa ikishughulikia sana wahamiaji na hasa wale wa kutoka Ethiopia.

Bulembo ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hadi mwishoni mwa mwaka jana, alisema wakati wakifanya hivyo, wamekuwa wakiwalinda wahamiaji ambao wamo ndani ya nchi na wengine wameishi zaidi ya miaka 20 sasa bila kuwa na vibali maalum.

Alisema hali hiyo ni hatari kwa kuwa wengine wamekuwa wakilindwa na watendaji toka idara hiyo na wanaendesha shughuli zao bila wasiwasi

“Inashangaza kuna baadhi ya wahindi wapo humu nchini zaidi ya miaka 20 na wanajulikana lakini mnawaacha na badala yake mnawakamata kina Bashe ambao wamezaliwa hapa nchini,” alisema.

Bulembo pia alizungumza kuhusu utendaji wa Kikosi cha Usalama Barabarani akieleza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wabunge kutumia ubunge wao kama kinga dhidi ya kikosi hicho wanapofanya makosa ya barabarani.

Alisema ni vyema kikosi hicho kikafanya kazi yake kama ilivyopangwa na si kuogopa pale kinapowakamata wabunge.

“Kama mbunge kafanya kosa, kamata peleka mahakamani. Ubunge siyo kinga ya kufanya makosa na wala isiwe kuwatishia askari wa barabarani, waacheni wafanye kazi zao,’’ alisema.
 
Hili la wabunge kutumia ubunge kuvunja sheria za barabarani lipo, mfano kuna hiace zimeandikwa R Meta pamoja na nyingine zinazomilikiwa na polisi zinazosafiri kati ya Muheza na Tanga. Wakati magari mengine yakitakiwa kuishia stand ya Kange zao zinafika hadi stand ya mjini na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.
 
wabunge wa CCM............... mjinga mmoja naye alihoji kwanini mwanaume wa kwenye nembo ya taifa amevaa wigi akasahau kuhoji kwanini amevikwa sketi pia........:D:D:D:DHAWA NI WABUNGE WA CCM... TUWAPIGIE MAKOFI TASAVALI
 
Kumbe ni mbunge mwanaume wa kuteuliwa, ccm wanapenda dezo sana, upinzani hakunaga mbunge mwanaume wa kuteuliwa
Ni CCM tu wanaume wanateuliwa.... hawa tunawaita DUME SURUWALI.. huku upinzani kila mwanaume anakula kwa jasho.... akina Maige, na huyu aliyetema pumba upinzani wangesubiri miaka 100 kuwa wabunge
 
basi hapo ndo jiwe anapenda vilaza kama hawa akiona hoja kali za kina bashe anashupaza shingo kama kuku yupo kibla
 
Kwa hili la vitambi hata Mimi huwa nawaza sana... Utakuta askari polisi hasa wanawake yuko km gunia la mpunga!! Hivi kikinuka kweli anawezaje kuhimili mikiki tens wale wa barabarani ndo wanatia fora asee...yaani ni shiidah!!
 
wameshiba rushwa, ndio maana waalimu hawana vitambi lakini askari+wanasiasa wana vitambi kama tyres za vitz
 
Wahamiaji haramu ni wengi sana hasa mikoa ya mipakani mfano ukienda Kagera karibu kila shule binafsi ina waalimu wa Kiganda wasio na vibali maalumu vya kuishi nchini wala kufanya kazi. Wengine ni wajasilia mali japo hawalipi kodi
 
Back
Top Bottom