Bungeni, Dodoma: Jerry Silaa ataja sababu tatu zilizopelekea kutofika Kuhojiwa

fundimchundo

JF-Expert Member
Jul 23, 2010
416
1,000
Wacha watafunane kwanza
Revolution eat their own children.
CCM ilikosea sana kuvuruga Uchaguzi Mkuu uliopita.
Sasa wanaanza kuumana meno wao kwa wao, huku Upinzani ukiendelea kukomaa mioyoni mwa Watanzania.
Tumesikia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Kaijage, akitoa wito Tume yake ipewe makucha, badala ya kupewa Maagizo na Mwenyekiti wa CCM-Taifa.
Na huu ni mwanzo tu.
Hivi sasa, mahali popote Tanzania, ukifanyika Uchaguzi huru na wa haki, chini ya Tume Huru ya Uchaguzi, CCM hawawezi kupata hata Kiti kimoja cha Ubunge.
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
9,489
2,000
Kutopewa hati ya wito ni miongoni mwa sababu zilizotajwa na mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa ashindwe kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuendelea na shauri la tuhuma za kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Sababu nyingine alizotaja ni kufiwa pamoja na kuugua jambo ambalo amedai kuwa, isingekuwa rahisi kwake kuhudhuria shauri hilo.

Akizungumza mara baada ya kutoka kwenye kikao hicho leo Ijumaa Agosti 27 2021, Silaa amesema alipohojiwa kwa mara ya kwanza Agosti 24, 2021 alimaliza utetezi wake.

“Kamati niliijulisha siku hiyo hiyo ya Jumanne asubuhi kuwa nilifiwa na kwa hali ya kawaida ningeomba hudhuru nisije niliona kwa picha ninayoiona hapa hata ningewaambia wasingenielewa,”amesema.

Pia, amesema suala lingine ni kiafya na kwamba alikuwa asafiri kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za mazishi na kwamba, kama ilivyo kwa wengine hata yeye aliona wito wa kuitwa kupitia kwenye mitandao.
Mbunge wangu anatuchanganya....

Kwani kuuguliwa ,kufiwa na kuumwa hakutakiwi kutolewa TAARIFA?!!!

#SiempreCCM
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom