Bungeni, Dodoma: Jerry Silaa ataja sababu tatu zilizopelekea kutofika Kuhojiwa

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
893
1,000
Kutopewa hati ya wito ni miongoni mwa sababu zilizotajwa na mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa ashindwe kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuendelea na shauri la tuhuma za kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Sababu nyingine alizotaja ni kufiwa pamoja na kuugua jambo ambalo amedai kuwa, isingekuwa rahisi kwake kuhudhuria shauri hilo.

Akizungumza mara baada ya kutoka kwenye kikao hicho leo Ijumaa Agosti 27 2021, Silaa amesema alipohojiwa kwa mara ya kwanza Agosti 24, 2021 alimaliza utetezi wake.

“Kamati niliijulisha siku hiyo hiyo ya Jumanne asubuhi kuwa nilifiwa na kwa hali ya kawaida ningeomba hudhuru nisije niliona kwa picha ninayoiona hapa hata ningewaambia wasingenielewa,”amesema.

Pia, amesema suala lingine ni kiafya na kwamba alikuwa asafiri kwa ajili ya kuhudhuria shughuli za mazishi na kwamba, kama ilivyo kwa wengine hata yeye aliona wito wa kuitwa kupitia kwenye mitandao.
 

Iboya2021

JF-Expert Member
Dec 1, 2020
1,406
2,000
Ni majitu ya hovyo sn haya CCM
1630059517950.png
 

UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
12,835
2,000
Kama CCM kwa CCM hawatendeani haki vipi kwa wapinzani? maana hana imani na hii kamati
Upinzani gani tena si mnasema hili bunge la ccm? sasa habari za upinzani zinakujaje mbona unataka tuanze kusumbua akili kwa vitu visivyokuwepo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom