mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Unngeanza wewe na familia yako kama mnayo bajeti na ni kwa kiwango gani mnaitumia kufanikisha malengo ya mipango yenu.Leo Juni 11, mwaka huu 2020 nasikiliza bunge la bajeti na kupata taarifa ya deni hili. Naomba kwa wataalamu wa mambo kunielewesha kuhusu namna ambavyo deni la taifa hutokea na sababu zake. Mbali na hapo naomba kufahamishwa kuhusu ulipaji wa deni hilo na athari zake kwa kila mwananchi wa nchi hii.
Swali: Hivi ni kweli idadi kubwa ya Watanzania wanao uelewa kuhusu bajeti na matumizi yake au ni baadhi yao tu? Kama ni baadhi yao basi tujue ni namna gani ya kumfanya mwananchi wa kawaida kupata uelewa ili kuondoa sintofahamu na kuwafanya Watanzania kuwa aware na nchi yao.
Naomba kuwasilisha kwa wataalamu...