Bungeni: CHADEMA wana hoja Hotuba ikishahaririwa iinakuwa siyo ya Upinzani tena bali ya Ofisi ya bunge

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,560
Tumeshuhudia mawaziri vivuli Joseph Mbilinyi na Peter Msigwa wakigomea kusoma bungeni Hotuba za kambi ya upinzani kwa madai kuwa zimehaririwa.

Nimejaribu kufuatilia kidogo na kugundua kuwa Chadema wana hoja ya msingi kwani kazi za maofisa wa bunge si kuhariri Hotuba ziwe za upinzani au zile za kamati za bunge.
Hotuba ikishahaririwa inapoteza uhalisia na kuwa ni kitu kingine tena hasa pale inapohaririwa na mtu wa itikadi nyingine.

Napingana na Chadema katika mambo mengi ya msingi lakini katika hili nawaona wana hoja.

Niishie hapo
Maendeleo hayana vyama!
 
Ndio maana kuna kuchezea box la kura ili bunge zima lijae wanaccm, jiwe anachotaka ni mawazo ya aina moja. Na wabunge wa ccm kwakuwa wengi wanaingia bungeni kwa kubebwa na serikali, ni dhahiri wote wataunga mkono kila kiletwacho na serikali. Huo ujinga ndio kakataa CAG kuabudu utashi wa jiwe natokea yake kaishia kudhalilishwa.
 
Ukiona wanahakiki Hotuba ujue kwamba wao hawataki kukosolewa, na hiyo ni moja sifa za serikali ya kiimla,,huwa hawapendi kukosolewa kabisa, Kwenye Dna zao hakuna suala kukosea. Wao ni miungu watu,,ingewezekana wanaweza hata kuwawekea maneno mdomini ya kuongea.
 
Ndio maana kuna kuchezea box la kura ili bunge zima lijae wanaccm, jiwe anachotaka ni mawazo ya aina moja. Na wabunge wa ccm kwakuwa wengi wanaingia bungeni kwa kubebwa na serikali, ni dhahiri wote wataunga mkono kila kiletwacho na serikali. Huo ujinga ndio kakataa CAG kuabudu utashi wa jiwe natokea yake kaishia kudhalilishwa.

Wabubge kadhaa wa ccm wameshapata matatizo na serikali ya chama chao. Wengine waliokuwa wakifanya kazi nzuri kuifanya serikali ikae sawa sawa sasa wamenyamaza.

Hivyo sidhani kama uko sahihi kuwa kinachotafutwa ni mawazo ya aina moja tu. Kwanzaa hilo haiwezekani. Lakini la msingi zaidi ni kwamba watu wote bila kujali vyama vyao, makundi ya jamii, imani zao, usomi wao nk. wanyamaze; serikali pekee ndiyo yenye haki ya kuongea.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom