Bungeni: Bajeti Kuu ya Serikali Mwaka wa Fedha 2021/22

Msitegemee jipya zaidi ya kodi za kukamuana na kuongeza ukubwa wa budget(makadirio), budget ambazo kila mwaka hawafikii malengo kwenye makusanyo.

Hawabuni wala hawatengenezi vyanzo vipya zaidi ya kucheza na vyanzo vile vile miaka yote( pombe, kodi za bandarimi, n.k).

Ubunifu wa miradi mipya hauendani na ongezeko la vyanzo vya mapato matokeo yake budget hazitekelezeki.

CCM imefeli sana katika swala zima la ubunifu wa vyanzo vya mapato.

Safari hii covid ndio itakuwa wimbo kwenye hii budget na kulalamika wahisani kutotekeleza ahadi zao.
Ndugu Slip hapo umelaumu tu bila kutoa ushauli kwa maoni yako ungependekeza vyanzo vipi vya mapato viongezeke na ungependa mbinu gani mbadala itumike ili kufikia malengo katika ukusanyaji wa kodi?
 
Heri ya asubuhi wanajamvi wenzangu, ni matumaini yangu mu buheri wa afya na kwa wale wanaoumwa Mwenyezi Mungu awajalie nafuu ya haraka.

Bajeti Kuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kuwasilishwa leo Juni 10, 2021 Bungeni katika Bunge la Tanzania jijini Dodoma saa 10:00 jioni na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.​

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Nchemba ameeleza kuwa Bajeti ya mwaka huu ni Bajeti ya kimkakati na ikumbukwe kwamba uwasilishaji wa leo utakuwa ni wa kwanza kwa Serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Moja ya watu waliopewa mwaliko maaalum wa kushuhudia uwasilishaji huu Bungeni ni wajumbe wa Kamati Kuu (KK) ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi.

Matangazo ya moja kwa moja ya uwasilishaji wa Bajeti Kuu kwa mwaka wa fedha 2021 - 2022 yatarushwa na televisheni ya Taifa (TBC) na vyombo vingine vya habari vya nchini Tanzania.
#BajetiYaKimkakati
#BajetiYetuMaendeleoYetu
#BajetiRafikiNaShirikishi
#KaziInaendelea​

View attachment 1813921
View attachment 1813920
Hii sio budget ya kuendesha ccm
 
Wanapunguza kodi ya makampuni ya kubet ili waongeze idadi ya makampuni hayo hivyo Watanzania kushiriki kwa wingi na kupoteza pesa zao!!!! Badala ya kupunguza kodi kwa Wafanyakazi. Mnaoshiriki kubet STUKENI muokoe pesa zenu.
Hapo hapo wameondoa kodi ya smartphones, now zitaingia kwa vurugu mtindo mmoja.
 
IMG-20210610-WA0118.jpg
 
Vurugu ztakazo lipuka sasa huko barabaran...sipat picha side mirrors zetu ztakavyovunjwa...yaan hawa mbwa watatamba sana huko..yaan ile kujibenua wanavyofanyaga..itakua mara 10

Na pia wategemea kumwagwa mchuzi kwa road sana.
 
Nimeskiliza kwa umakini aisee..kuna maeneo kibao kodi zmefutwa au kupunguzwa pakubwa sana...

Tembeeni kifua mbele..najua weng hawajaskia fatilieni kwa umakin

Imports nako kumeguswa huko...wameongezewa kodi kwenye baadh ya bidhaa ambazo hazina mantik na sis wenyew tunauwezo nazo...ingawa wamegusa nukta tuu....

Bidhaa nyiiing sana kutoka nje zingekua discouraged kwerikweri yaan karib na marufuku..yaan wawek kodi huko kias kwamba mtu akiwaza kuagiza toothpick from china aone hiiii.....

Nauhakika bidhaa hizo zingenyongonyeshwa vijana weng wangechangamkia fursa na tatzo la ajira lingepungua sana..imagine fagio znatoka china...nguo ..viatu hata vya kawaida tu,pads za wadada..handkerchief ,mafuta ya kula(imagine wazuie kabisa..utaona had vijana wa kidimbw wanaenda lima alizet),sukari,mapazia..hadi vidude vya kuanika nguo jaman,na takataka kibaoo zimejaa huku mitaan ambazo tunauwezo nazo wa kutengeneza....

Mtu anaweza sema ooh kwann msitengeneze hzo bidhaa zikawepo sokon halaf mbongo achague...well

Ni sawa. Unaweza sema hvo kama jicho lako halion kwa ukubwa...

1.Kwanza production cost katika bidhaa za viwanda vya mataifa kama china huwez fananisha hata sku1 na hapa kwtu..
Tukianza kwenye umeme tu.sisi tunatumia umeme wa mafuta+ hydro wao wanatumia nuclear...hata umeme tuu kama bidhaa kwetu ni gharama sana.so lazima production iwe gharama

2.ubora.kwakua sis ndo tunaamua kuanza kujikwamua na pia bado hata wajuz na wataalam hawajajitosheleza na kimitambo na machine bas pia utaalam una gharama pia ambao pia utaongeza production cost ili utoe kilicho bora kwahyo ukiweka bidhaa from china ambayo ina finishing nzur na ya kwetu hapa hautavitendea hak vya kwetu..yatupasa tufunge mikanda. Tutateseka kwa muda ila baada ya miez kadhaa tutakaa sawa..mbona mifuko tumefanikiwa sana kitu ambacho hatukuamin..mifuko bora kabisa na ya bei ya kutupa

3.bidhaa toka nje kule wana advantage za kikod tofaut na hapa..hapa kodi ni nying na ni kubwa sana ambapo mwisho wa siku znafanya bidhaa kuwa ngumu kuuzika sabab gharama inakuwa kubwa so huwes weka bidhaa hzo kwenye kapu 1.

4.morali inapungua pale unapoona tayar kuna bidhaa hyo sokon ambayo ulitaka itengeneza tena kwa bei cheap kabisa.so kuna umuhim hzo bidhaa zinyongonyezwe kabisa.

5.na mengineyo meng....mim sio mchumi wala mtalam wa mambo ya bishara so nmeongea kama layman kabisa...mim ni mwanasayansi..so mtanisamehe kama nmepuyanga.

Ila budget imegusa maeneo meng yenye fursa kwetu sis ambao tunandoto za kujikwamua..sanasana kwenye production..kilimo etc huko kuna unafuu nmeskia sana.tozo zmefutwa na kutolewa kabisa
 
Kabisa..wamefuta na kupunguza kodi maeneo meng sana...yaan kama mtu hajaskia...anaweza akaendelea lipa as usual kumbe mambo yamebadilika...migodin pia nimeskia tena kaongea kwa muda mref sana..kodi kibao zmepunguzwa...so ni muhimu sana
Tusubiri tuone..ni mapema sana
 
Mimi bora nifuayilie Cartoon ya Tom and Jerry kuliko "bwajet" yenu !!! Hakuna lolotr
Hujaskiliza mkuu..achana na stor za vijiwen.ungeskiliza kwanza...kama inakuhusu utaiona ya muhim lakin kama hikuhusu utaona takataka tu..makod kibao yamepunguzwa huko mengne yametolewa kabisa...bidhaa kutoka nje zisizo na mntik wamedhibit ili watu wachangamkie fursa..sasa unasemaje bajet haina maana...au ndo stor za vijiwen zilezile tulizozoea
 
Kuna maeneo kodi haikusanywi
Eneo la wafugaji,maziwa na nyama
Biashara ndogo zisizo rasmi kama mitumba ya nguo na viatu
Biashara za kuku na mayai
Iweje mshahara wa laki tatu ukatwe kodi wakati kuna watu wanafanya biashara kubwa na hawakatwi hata shilingi moja?
 
Pia ile faini ambayo wanapigwa bodaboda/toyo kwa kila kosa moja, imepunguzwa kutoka Tsh 30,000 hadi 10,000
Hapo naona wamepuyanga. .vijana watakufa sana na zaid..tunawajua vzur bodaboda types..akil hawanaga...nilitegemea tozo yao iwe juu zaid...wanavunja sana side mirrors zetu barabaran sabab wana overtake hovyo..yaam itakua shida. Viduku ndo vitaongezeka
 
Back
Top Bottom