Bunge/Waziri Mkuu: Limulikwe genge la kifisadi, rushwa linalojiita ni kamatakamata ya magari jijini Dar kwa visingizio vya kudhibiti uhalifu barabara

mkys

Member
Apr 3, 2012
31
18
Waheshimiwa wawakilishi, viongozi wa taifa, hoja hii inafikishwa kwenu kwa kile kinachoonekana kuwa hakina mfuatiliaji jijini Dar. Hiki ni ile kero inayowasibu madreva wa magali binafsi inayosababishwa na genge la kamatakamata ya magari barabara za mitaa ya jiji.

Hili genge huibuka na kupotea, na kuna wakati limewanyanyasa waendesha pikipiki likiwazuia wasiingize pikipiki mjini kati pasipo kibali maalumu, wakati baadhi ya wakazi mjini ni wamiliki na watumiaji wa aina hiyo ya usafiri kwa shughuli za kila siku.
Kwa sasa kuna genge kamatakamata kwa magari kwa visingizio vikubwa viwili:

1, Kuegesha gari isivyotakiwa kisheria,
2. Kufanya shughuli za u-taksi bubu ati inakosesha mapato serikali.

Kinachoendelea kuuhalisia ni kuwa dreva atasimamisha gari lake mahala fulani barabarani kwa dakika zipatazo mbili hivi aidha akitelemsha mtu au kitu na au kwa shughuli yeyote ya kibinadamu ndani au nje ya gari. Mara ataviziwa kiuvamizi akidaiwa yuko hatiani na chini ya ulinzi kwa kosa la kuegesha gari kimakosa. Genge litaweka lock kwenye tairi iwapo dreva atajaribu kukataa kusudio lao.

Genge humlazimisha dreva akubali amefanya kosa kwa vitisho vya kuletewa break-down ilikokote gari hadi yadi zao zilizo pale Halmashauri ya Ilala kwa gharama ya mwendesha gari - dreva mtuhumiwa. Watamtajia gharama ya adhabu ya faini isiyopungua T.sh.300000/= kabla hata hajafikishwa yadi na ofisi zao zilizo chini ya miti. Watampa mhanga mazingira ya kutoa rushwa ili wamalizane. Dreva akikataa watamlazimisha apeleke gari yadi akitahadhalishwa kuwa iwapo gari litafika yadi halitatoka hadi amelipa faini. Ujumbe hapa ukiwa ni bora amalizane nao tu mapema kwa unafuu wake. Akifikishwa yadi wanagenge huingia mapokezi na dreva huletewa fomu yenye kosa tayari akishinikizwa ajaze majina yake na saini yake tu na papo hapo kuhukumiwa kuwa "gari halitoki hadi melipa faini".

Iwapo mtuhumiwa atajitetea kuwa hana hela hiyo, wao humshawishi kwa lugha ya kinafiki kuwa awapigie simu ndugu, jamaa, rafiki zake kwa msaada wa hela hiyo. Huu ni utapeli wa wazi kabisa. Ni ngenge fulani linalofanya wizi kwa wakazi wa jiji likiwa ndani ya mazingira ya taasisi halali ya serikali.

Cha kushangaza ni kuwa wahusika wana ushauri tofauti tofauti kwa tukio moja. Mmoja atakwambia tafuta 150000, mwingine 200000, mwingine kiasi kilichoandikwa kwenye fomu ili ulipe uweze kutoka. Hadi wao wenyewe wanadiriki kumwambia mtuhumiwa kuwa ndani ya yadi hakuna MUNGU kwa hali ya mamlaka ya ukomoaji na unyanyasaji wa kifisadi waliyojivisha ndani ya genge hilo.

Iweje kundi lenye mfumo huu wa kilaghai linyamaziwe hivihivi tu liendelee kuwaumiza watu na kuvunja shughuli zao za kila siku?
Nini kilicho nyuma ya pazia kuiona tabia hii yenye unyanyasaji, ukatili, unyang'anyi, utapeli, wizi mficho, rushwa, ufisadi, dhuluma ikiendelea bila kudhibitiwa?

Genge hili lina sifa si ya kulea tu bali vilevile ya kukuza na kuwaambukiza wana-jiji kuiamini itikadi ya wizi, unyangh'anyi. Wana jiji wanaliona genge linaishi kwa dhuluma na ma-deal fisadi viongozi wakilitizama tu.

Iweje wao nao wasifanyiane vilevile kwa namna tofauti. Kama sehemu ya kisingizio cha pili, genge huwakamata madreva wanaopitia wasafiri kwenye vituo vya mabasi asubuhi muda wenye uhaba wa usafiri kwa miundombinu duni iliyopo ati wanafanya biashara ya U taksi bubu. Genge liko tayari kumfuatilia dereva aliyepakia watu watatu wawahi ofisini kwa kumbambikizia kosa hilo na suluba za kifisadi zilizotajwa hapo juu ili atoe rushwa. Hutumia kigezo cha kuikosesha serikali mapato. Hata kama wamempa dereva kila mmoja T. sh. 1000, au 2000 kila mmoja, haiingii akilini kulifikiria hili kama pato la kuikosesha mapato serikali wakati gari limetumia mafuta na linahitaji service liweze kumudu mahitaji ya mtumiaji.

Pamoja na kuiweka hii hoja mezani, ingeoneka bora kama jiji lingefahamishwa kuwa watu wasipande lift kwa usalama wa madreva kwa genge hili.

Ingeliwafaa wananchi wakifahamishwa ni kwa vipi kupakia vichwa vitano ndani ya gari kwa gharama isiyozidi T.sh. 10000 kunamfanya dreva aonekane ni mwenye taksi bubu naalipe faini T.sh.300000 kugomboa gari lake.

Ingefaa vile vile wananchi wajue ni kwa vipi genge lina mamlaka yakimahakama kwa uporaji huu mchana kweupe. Tuiombe serikali ilichunguze hili kuona uhalali wa uwepo wa genge hili dhalimu.

Nawasilisha.
 
Poleni sana... Nilidhani zile issue za Yona zimerudi tena...

Kumbe hapa issue ni kupakia watu asubuhi endapo wanaelekea unapoelekea wewe...
 
Back
Top Bottom