Waandishi wa Magazeti ya Mwananchi, Nipashe na Mtanzania wahojiwa na Kamati ya Maadili ya Bunge, waonywa

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Kamati Maadili ya Bunge imewahoji Wahariri na Waandishi wa Habari wa Magazeti ya Mtanzania, Mwananchi na Nipashe kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu mwenendo wa kikao cha Kamati hiyo kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 34 (1) (f) & (g) ya Sheria ya Kinga za Bunge.

DOr00e6WkAMW22H.jpg
DOr00H9WAAUr1SW.jpg

----------

UPDATES>> 17, NOV. 2017

Spika wa Bunge, Job Ndugai awaonya wahariri wa magazeti ya Mtanzania, Mwananchi na Nipashe na kuwataka waliombe radhi Bunge ndani ya siku 5 kwa kosa la kutoa taarifa zinazohusu mwenendo wa kikao cha Kamati ya Maadili ya Bunge

..Na kwanini mwenendo wa vikao vya kamati hiyo viwe SIRI?

..wabunge wamechaguliwa na wananchi, hivyo kila wanachokifanya ni kwa niaba ya wapiga kura. kwa msingi huo wapiga kura wanatakiwa kuwa na taarifa za shughuli zote zinazofanywa na wabunge ikiwemo taarifa za vikao vya kamati mbalimbali za bunge.

..kama kamati inajadili mambo yanayohusu taarifa za SIRI ZA USALAMA WA TAIFA then kuna ulazima wa vikao vya namna hiyo kuwa vya siri, lakini vikao vingine vyote vinatakiwa kuwa vya wazi.
 
Sijaelewa?! Kwanza mpaka hizo taarifa zinafika kwenye vyombo itakuwaje iwe siri tena?
 
..Na kwanini mwenendo wa vikao vya kamati hiyo viwe SIRI?

..wabunge wamechaguliwa na wananchi, hivyo kila wanachokifanya ni kwa niaba ya wapiga kura. kwa msingi huo wapiga kura wanatakiwa kuwa na taarifa za shughuli zote zinazofanywa na wabunge ikiwemo taarifa za vikao vya kamati mbalimbali za bunge.

..kama kamati inajadili mambo yanayohusu taarifa za SIRI ZA USALAMA WA TAIFA then kuna ulazima wa vikao vya namna hiyo kuwa vya siri, lakini vikao vingine vyote vinatakiwa kuwa vya wazi.

Kama kuna sheria inakataza basi hakuna kufanya hilo jambo, ni kinyume cha sheria. Kama sheria hiyo ni mbaya fanya taratibu hiyo sheria irekebishwe, huo ndio weledi unaotambua utawala wa sheria. Kupinga sheria kwa kuivunja ni ujinga tu kama kumfuata na kumzonga mwamuzi wa mpira wa miguu wakati tayari ameshaamua jambo
 
Back
Top Bottom