Bunge,wabunge na maneno yasiyo rasmi na ya kihuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge,wabunge na maneno yasiyo rasmi na ya kihuni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Madela Wa- Madilu, Jul 4, 2012.

 1. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ndugu wana JF na WaTanzania kwa ujumla.
  Nashangaa na sikubaliani na namna Bunge letu Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linavyo endeshwa na jinsi Spika wa Bunge na Wabunge watumiavyo maneno ya mitaani yenye kujaa kejeli, dharau,matusi na ukosefu wa nidhamu kwetu wa Tanzania tulio wapa dhamna ya kuwepo pale.

  Wabunge na heshima zao wamekuwa wakisimama na kuongea maneno yenye kila aina ya Ukosefu wa adabu, ubabe, majigambo na kejeli katika kuchangia hoja zao. Aidha wamekuwa wakiongea maneno ambayo hata huko mitaani hutumiwa na kundi fullani tu la watu ambao kwa ujumla huitwa WAHUNI.

  Spika naye amekuwa akitumia maneno hafifu,dhaifu na yenye kubeba matusi ndani yake kama vile Bunge lake ni la mipasho ya Mapashkuna Mapapa na Mateja wa Unga. Spika wa bunge amekuwa akiruhusu wabunge kutoa hoja huku ndani yake wakibanabana maneno yenye kila Uchuro na ushambenga katika Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kibnume kabisa na kanuni na taratibu za Bunge.

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa makusudi amelishusha hadhi Bunge tukufu na kulifanya kuwa mahali pa kurumbana katika kumtafuta nani ni mgani mzuri wa matusi na misemo ya matusi, katika kundi la watu wa lika moja.

  Kwanza kabisa Spika mwenyewe binafsi kajishusha hadhi hadi na kuwa na hadhi iliyo chini ya MONITA wa darasa la Pili katika shule ya watoto watukutu. Pili kashusha hadhi ya Bunge zima na kulifanya kuwa mkusanyiko wa Wahuni wchovu.

  Kuna maneno mengi ambayo si matusi yanatumika Bungeni kinyume kabisa na taratibu za bunge. Maneno haya hutumika yakiwa na nia ya kueleza tofauti za umri, jinsia, mahusiano, mwonekano, sifa na nafasi katika jamii. Maneno haya yanweza kutumika katika mmaelezo ya taarifa fulani bila kuvunja kanuni. Hata hivyo, maneno haya yatumiwapo kum address mbunge yanavunja kanuni na taratibu za Bunge. Kwa muda mrefu sasa maneno haya yamekuwa yakitumika bungeni kiasi kwamba sasa yanaelekea kuwa msamiati mpya unaokubalika bungeni.

  Spika amekuwa akitumia neno kaa chini bila Staha wala heshima Bungeni. Mbunge anaambiwa akae chini kwa mahusiano ya Bwana na Mtwana bila kujali Utukufu wa Bunge na ukweli kwamba sisi wananchi tunafuatilia vikao vya Bunge kwa ukaribu sana.

  Utamsikia ; Kaa chini! Nimesema kaa chini! Kaaaaaa chiiiiiini!!!!! Kaaa chiiiini Hivi kwa nini hukai chiiiiini! Unawashwa nii wewe KAAAAAAA CHIIIIIIIINI?????


  Sijui ni kanuni ya ngapi ya bunge letu tukufu inamruhusu spika wa bunge kumwambia mbunge aliyechaguliwa kwa kura kaa chini UNAWASHWA!!!!!!.
  Kuwashwa nini makalio?
  kuwashwa mwili?
  Kuwashwa na nia ya kutoa hoja na ufafanuzi??

  Neno kuwashwa ni neno lisilo na staha hata kidogo ndani na nje ya bunge.Neno hili linazidi kuto kuwa na staha hasa litokapo kinywani mwa spika au mbunge mwenye wadhifa wa kuendesha kikao chochocte ndani ya Bunge.

  Sasa kibaya Zaidi wabunge kadhaa wanapiga makofi kwa nguvu na kukenua meno kingedere ngedere katika harakati zao za kukubaliana na Spika kutumia neno la kihuni KUWASHWA. Wenzetu hawa wanao pigia makofi neno KUWASHWA kwa kuamini ni neno sahihi na pengine ni kijembe maridhawa cha kisiasa sijui vichwani mwao wanawaza nini?

  Binafsi namuona Spika ni mhuni fulani,ni mbabe na analeta maneno ambayo hata huko mtaani hutumiwa na Mateja waliobobea tu.

  Sioni mtu na adabu zake kwa mfano Mwalimu darasani akitumia neno kuwashwa kwa mwanafunzi wake anayeuliza maswali mengi.
  Sioni Mume akitunia neno kuwashwa kwa mkewe. Sioni shangazi akitumia neno kuwashwa kwa mjomba.

  Ujasiri wa Spika kutumia neno KUWASHWA ndani ya Bunge tukufu linalofuatiliwa kwa Ukaribu na watanzania wengi anautoa wapi??
  Ni Jeuri ya chama chake?
  Jeuri ya mtanifanya nini?
  Ni kushiba madaraka na utukufu?
  Ni Mtu aliye hovyo na asiye na staha kapewa kiti bungeni???


  Nimekuwa pia nikisikia wabunge, mawaziri na Spika wakitumia maneno yasiyo rasmi wakati wa ku address wabunge wenzao.

  Mfano Maneno ya MH Mwigulu Bungeni ni maneno yenye utovu wa nidhanu Bungeni, kwa wabunge na kwa wa Tanzania kwa ujumla. Aidha kauri zake ni za kujidharirisha yeye mwenyewe binafsi na hakukuwa na haja yeyote kutoa personal reference ya namna ile ili kujenga hoja. Wabunge wanao pigia makofi hoja yenye kubeba matumizi mabovu ya lugha inaonekana jinsi ambavyo wapo pale kushangilia mipasho ya kishankupe kuliko kujenga na kujadili hoja kiyakinifu " Jana nimemfundisha Kaka na leo namfundisha dada nitafundisha mpaka lini"

  Sijawahi kusikia mbunge yeyote akitoa kauri dhaifu kama hii mbele ya Bunge kisha spika kukaa kimya bila kutoa onyo au kumwomba afute kauri zake za kihuni zilizo kinyume na taratibu za bunge. Maneno haya yanamfanya Mwigulu kuwa Mhuni fulani pia yanamfanya Spika wa Bunge kuwa Mhuni vile vile kwa kuruhusu Uhuni Bungeni.

  Bungeni hakuna Kaka Dada, binamu shemeji wifi mchumba bwana mdogo, kichaa, jambazi,wakuja, mkubwa, mdogo, form six, darasa la saba, under graduate, graduate, ngumbalu au neno lolote lenye kubeba sifa zisizo za kibunge.

  Sijawahi kumsikia mbunge yeyote Bungeni akimwambia Mzee Sita kwamba jana mkeo Magreth alisema so and so. au Mama sita kuambiwa Mume wako tulimwambia aongelee jambo hili.
  Sijaona mtu akimwambia Mama Anna Kilango kwamba Mume wako John Malecela amekwisha jibu hilo.

  Ni utovu wa nidhamu kutumia maneno kama, kaka, dada yake, mchumba wake au mdogo wangu na bwana mdogo. Nidhamu ya Bunge na heshima yake kamwe havitadumishwa iwapo maneno haya yataendelea kutumiwa.

  Kitazuia nini Wabunge wengine kuanza kutumia maneno kama Mama huruma, Changudoa, Mzee kiweke, Zipu haifungi,Hailali, MH++, chakula ya wote, Mb*%lo mkononi na Ch*%pi mkoni kuaddres wabunge wengine wanao hisiwa kuwa na vijitabia????????????? Kitazuia niniii?

  Sasa akina John Mnyika wakisimama na ku maddress mtu yeyote anayewaita bwana mdogo kwa maneno kama.

  Shaibu Edward Lowassa unahusika moja kwa moja na tatizo la mgao wa umeme au Ajuza Stella Manyanya na double vyeo vyako vya &^%$pi huwezi kumwita Dr Ulimboka Hitler. Si utazuka mtafaruku wa pata shika nguo chanika Bungeni??

  Mbunge anasimama katika Bunge tukufu na kutuia maneno yasiyo rasmi,hata kama si matusi, bungeni na hata maneno ya kihuni na kuachwa aendelee kuongea?? Utaratibu huu wenye udhaifu mkuu unatupeleka wapi??

  Mdogo wangu hapo umepotoka- Sahihi; MH Mnyika hapo umepotoka au MH Mnyika, mbunge kijana hapao umepotoka.

  Afadhari uewahi kabla vichaa wako hawja simama- Sahihi ;Afadhari umewahi kabla ya wabunge wako machachari hawja simama

  Mdogo wangu nakuheshimu- Sahihi; MH Lisu nakuheshimu

  Nyie wabunge wa upinzani heshimuni mvi- Sahihi; Ninyi wabunge wa upinzani heshimuni hoja zinazotolewa na wabunge wa muda mrefu

  Usilete mambo ya form six hapa- Sahihi ; tafadhari wabunge fuateni taratibu na kanuni za bunge

  Spika wa Bunge na baadhi ya wabunge wakongwe wanadhani kwamba UMRI na VYEO serikalini ni mtaji wa Kuboa Bungeni kwa hoja zao mfu.
  Umri si kigezo cha heshima pale Bungeni. Hoja ya mtu haiheshimiwi eti kwa sababu ana mvi nyingi kichwani aua ana umri mkubwa. Hakuna hoja kama mimi umri wangu ni sawa na baba yako au babu yako. Cheo cha mtu pale Bungeni hakimfanyi awe sahihi katika hoja yake wala si kinga ya kuto hojiwa kwa undani juu ya kauri zake katika hoja.

  Bunge ni lazima litumie lugha ya staha wakati wote. Hii si hiari ya mbunge au spika.
   
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  "Mwenye uchungu na taifa hili aende hospitalini akajifungue"
  Hii ni moja ya kauli ya mbunge flani, ila Naibu spika Ndungai alipoombwa muongozo wa kumtaka mbunge huyo afute kauli hii inayoudhi, nilisikitika sana pale Ndungai aliposema kuwa kauli hii haina matatizo kwasababu ni kweli wenye uchungu wanapaswa kwenda kujifungua.
  Hivi ni kweli neno hilo lenye muktatha wa kitabibu tena linalomlenga mwanamke anayehitaji kujifungua baada ya kubeba mimba kwa miezi tisa ni sahihi kweli kutumiwa kwenye muktatha wa kibunge tena kum-adress mwanaume ambaye pia hata kwenye muktatha wa kitabibu hana uwezo wa kubeba mimba na kujifungua??
  Hivi tukisema spika ni moja ya sababu ya uchochezi wa matumizi ya maneno yasiyo rasmi bungeni, anna makinda atasimama na kusema wanachafuliwa na kusema habari hizi ni za kipuuzi kama alivyodai hapo awali????

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
Loading...