Bunge wa Ujerumani kutotoa hifadhi kwa nchi za Magharibi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Bunge la Ujerumani Bundestag jana limepiga kura ya kukataa kuwapa hifadhi ya ukimbizi raia wa mataifa ya Tunisia, Morocco, Algeria na Georgia na kuzitaja kuwa ni nchi salama.Hata hivyo uamuzi huo lazima upitishwe na Baraza la Wawakilishi Bundesrat, ambako chama cha upinzani Greens kimesema kitaupinga. Ni hatua inayoongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Horst Seehofer, ikiwa ni sehemu ya kujaribu kudhibiti wahamiaji kuingia nchini humo. Uamuzi wa 2015 wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wa kuwafunguliwa mipaka mamia kwa maelfu ya wakimbizi, umechochea ongezeko la uungwaji mkono wa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia katika uchaguzi wa mwaka jana. Kutangazwa nchi hizo kuwa ni salama kutapelekea kuwa rahisi kukataa maombi ya hifadhi ya ukimbizi ya raia wake.

DW
 
Shukrani kwa taarifa mkuu
 
Hawa Bundestag nao wajinga; kwani magaidi wa Tunisia, Morocco, au Algeria kupata pasi za kusafiria za Libya au Syria ili waweze kuingia Ujerumani ni issue? Mbona simple tu.
 
Back
Top Bottom