dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof Mussa Asad amewasili bungeni, Dodoma kuitikia wito wa kufika katika kamati ya maadili
CAG tayari kwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kuhusu madai ya kudhalilisha Bunge, inadaiwa alisema bunge ni dhaifu.
UPDATES:1115HRS
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad akiwa tayari amefika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge Muda huu mjini Dodoma kuhojiwa kufuatia kauli za kudhalilisha Bunge akiwa ziarani nchini Marekani.
UPDATES: 1500HRS
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Emmanuel Mwakasaka, amesema kamati yake imemaliza kumhoji Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad na ametoa ushirikiano mkubwa. Hata hivyo, amesema kamati bado inaendelea na uchambuzi na wakikamilisha watalipeleka suala hilo kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Dodoma. Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge leo Jumatatu Januari 21, 2019 saa 8 mchana imemaliza kumhoji Mdhibiri na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu kauli yake ya “udhaifu wa Bunge.”
Wakati CAG akiondoka saa 8:47 atika viwanja vya bunge, maofisa mbalimbali waliwazuia waandishi wa habari kumhoji chochote.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka amesema atawaeleza waandishi wa habari kilichojiri katika kikao hicho.
CAG Assad aliyeteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, Desemba Mosi mwaka 2014 ameitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa wakati alipokuwa akihojiwa na kituo cha televisheni cha idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa (UN) akiwa New York, Marekani alikokuwa akihudhuria mkutano.
Alitumia neno “udhaifu” wa Bunge alipokuwa akieleza sababu za kutofanyiwa kazi kwa ripoti zake ambazo zimekuwa zikibainisha ufisadi.
Prof. Assad(CAG): Nitaitikia wito wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge - JamiiForums